Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Usome mwenyewe
---

1719956171453.png
Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWANANCHI
PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
 
Lissu atakuwa kaumia sana, ila Mchungaji naye katumia hasira baada ya kuukosa uenyekiti kanda ya Nyasa. Nina Imani kabisa, atarudi tu tena Chadema... Time will tell...
Aliondoka Juliana na Mwita seuze...!
 
Back
Top Bottom