Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Usome mwenyewe
---

Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWANANCHI
PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Siasa sio uadui,amwache katumia haki yake kikatba,ana uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa na wakati wowote
 
Lissu kaumia sana na Lema alilia sana kuhusu Msigwa kuhamia CCM, ila najua kabisa wazi. Lissu au Lema wanajua kabisa wana uchungu mkubwa ndani ya Chadema hakuna demokrasia ya kweli hasa katika kumpata Mwenyekiti wao au hata wenyeviti wa kanda, ni rushwa sana, ubabe sana na ukitaka kugombea uenyekiti Taifa wa Chadema basi wewe utakuwa msaliti mkubwa sana..!! Ni sbb tu hawana pa kwenda wanakufia na tai shingoni huko huko Chadema..!!
Wacha weee
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amesema kitendo cha Mchungaji Peter Msigwa kuhama Chadema na kukimbilia CCM kimeumiza sana moyo wake kwani amekuwa rafiki yake kwa miaka 20!

Lissu amebainisha kuwa Msigwa ni moja ya watu waliomwongezea chupa ya damu aliposhambuliwa kwa risasi eneo la area D jijini Dodoma.

========

Dar es Salaam. Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na

Kabla ya kuhamia CCM, Msigwa alikuwa akisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake aliyoikata kupinga uchaguzi wa uenyekiti Kanda ya Nyasa kupinga ushindi wa Joseph Mbilinyi maarufu Sugu aliyemshinda kwenye nafasi ya uenyekiti.

Mbali na kukata rufaa, Msigwa amekuwa akimlalamikia Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kupitia mikutano ya waandishi wa habari na mitandaoni, kuwa ndiye chanzo cha kushindwa uchaguzi huo.

Mchungaji Msigwa aliyekuwa akitetea nafasi hiyo alishindwa na Sugu kwa kura 54 dhidi ya 52 za Msigwa. Uchaguzi ulifanyika Mei 29, 2024 na kushuhudia mvutano mkali.

Baada ya Msigwa kutimkia CCM, ikiwa ni siku chache zimepita tangu aliposhiriki ziara ya Lissu mkoani Singida, Mwananchi Digital imemtafuta Lissu ili kupata mtazamo wake juu ya uamuzi wa mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akieleza ni rafiki yake.

Katika maelezo yake, Lissu amesema: “Mchungaji Peter Msigwa amekuwa rafiki yangu wa karibu kwa takriban miaka 20 ambayo tumefahamiana. Tumefanya kazi pamoja bungeni na nje ya Bunge kwenye chama.

“Tumekuwa naye kwenye Kamati Kuu ya chama kwa miaka mingi. Tumekuwa na misimamo ya pamoja kwenye masuala mengi ya kisiasa ya chama chetu na ya nchi yetu. Tumetofautiana kwenye masuala kadhaa ya chama na ya nchi vile vile,” amesema Lissu.

“Hili la kuhamia CCM limekuja kwangu ghafla kama ninavyoamini limekuja kwako ghafla pia. Nilimkaribisha kushiriki nami kwenye ziara yangu ya Mkoa wa Singida mwezi uliopita, na alikuja mara mbili na kila siku aliyokuwa kwenye ziara nilimpa fursa ya kuzungumza na wananchi wetu.”

Akigusia suala la yeye kupata taarifa awali, Lissu amesema: “Hata hivyo, mara zote alizokuwa na mimi hakunishirikisha au kunifanya nifikiri alikuwa na mpango wa kuhamia CCM.”

“Ni wazi alikuwa na mengi moyoni mwake ambayo hakutaka yajulikane. Sasa yamejulikana. Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa. Sikuwahi kufikiria itakuwa hivyo. Hicho ndicho kinachoniumiza moyo,” amesema.

Lissu amewahi kusema Mchungaji Msigwa ni rafiki yake na alikuwa miongoni mwa watu waliochangia chupa ya damu kunusuru uhai wake, aliposhambuliwa kwa risasi Septemba 7, 20217.

Tukio hilo lilitokea alasiri, Area D jijini Dodoma, wakati Lissu akitoka kushiriki mkutano wa Bunge uliokuwa ukiendelea.

Wakati Lissu akieleza hayo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye anaendelea na ziara mikoa ya kaskazini na sasa yupo Mkoa wa Tanga, ametumia kurasa zake za kijamii kuzungumzia siasa za upinzani na CCM.

“Kuwa chama cha upinzani hasa Chadema sio suala jepesi, linahitaji ujasiri wa namna ya pekee. Viongozi wengi wa upinzani na Watanzania wazalendo wa nchi hii wanapitia nyakati ngumu kutokana na uoga wa Serikali ya CCM.

“Marehemu Mzee Lowassa alithubutu kuingia Chadema, japo baada ya muda alirudi CCM.Tunatambua ujasiri wa maamuzi yake. Kitu pekee kitakachiokoa Tanzania kutoka kwenye mikono ya watawala ni ujasiri na uthubutu wa mwananchi mmoja mmoja; tuanze sasa kulipigania taifa letu,” ameandika Mbowe.

Mwananchi
 
Lisu mwenyewe kama anakili kweli..anatakiwa atoke kwenye hiyo kampuni ya wachxga iliyovaa koti la chama cha kisiasa,bora aende ACT wazalendo..Lissu anatumika pale kama punda mbeba mizigo tu..ila bado hajitambui.
Ukisikia dunian kuna makunguru alaf kuna.
RIKUNGURU NDO WWE SASA
LIKAMBALE KWENDA ZAKO
LISU SIO MPUUZI kama wwe
 
Duh! Wewe mpuuzi huna tofauti na mnyama wa porini na heri ungeishi porini kama wanyama wenzio wasio na akili. Binadamu aliyejaaliwa akili, hawezi kuandika ujinga kama huu wa kwako. Sidhani unaelewa hata Katiba ni nini. Ngoja niachie hapo kwani kujadiliana na wewe ni heri kujadiliana na meza au kiti!
Wewe una akili robo nielimishe katiba ni nini sasa kama mimi sifahamu. Unalazimisha kilia mtu aamini unachoamini wewe huo ni ujinga wa hali ya juu. Nimetolea mfano hapo Kenya walipata katiba mpya lakini matatizo yao yapo palepale hakuna kilochobadilika zaidi ya uhuru wa maandamano.

Elewa ndugu usifuate mkumbo wa wana siasa iwe ccm au chadema maendeleo hayaletwi na katiba mpya bali huletwa na kiongozi mwenye uzalendo na uthubutu. Tumeona hiko Arusha kero za wananchi zinatatuliwa na mkuu wa mkoa kwa kutumia katiba hii hii mnayoiita mbovu kwani kabla ya hapo Arusha likuwa haina kiongizi na katiba?. Inahitaji kutumia akili ya hali ya juu kunishawishi kuwa katiba mpya ni tiba ya natatizo ya wananchi na sio kuleta matusi yako hapa.

Mfano serikali kuhamia Dodoma ilitakiwa kufanyika toka miaka ya 70 uko lakini haikuwezekana, bwana la Mwl. Nyerere lilitakiwa kujengwa toka miaka ya 70 huko lakini haikuwezekena, sasa kaja JPM. kafanya haya yote kwa katiba hii hii unaniaminishaje mimi kuwa jatiba ndio muarobaini wetu badala ya kuniamibia kiongozi mzalendo aina ya JPM.

Nakazia tena katiba mpya sio muarobaini wa matatizo ya wananchi kama mnavyoaminishwa na wanasiasa bali ni muarobaini wa matatizo ya vyama vya sisiasa ila mmejifichia kwa wananchi.

Sisi wananchi tukipata kiongozi mzalendo mwenye kalba ya JPM tunajua matatizo yetu na ya nchi yanakwisha sisi hatupo kwa ajili ya kufia chama kama wewe tupo kwa ajili ya nchi na maslahi ya nchi, tena ushike adabu yako usiishi kwa kujipendekeza kwenye vyama wala wana siasa nyie ndio mnaochelewesha maendeleo ya hii nchi.
 
Lisu mwenyewe kama anakili kweli..anatakiwa atoke kwenye hiyo kampuni ya wachxga iliyovaa koti la chama cha kisiasa,bora aende ACT wazalendo..Lissu anatumika pale kama punda mbeba mizigo tu..ila bado hajitambui.
Wewe unaweza kua na akili na maarifa kuliko lissu au unajishaua tu hapa kwavile uipendi chadema.Lissu hana akili za kushikiwa.
 
Wewe una akili robo nielimishe katiba ni nini sasa kama mimi sifahamu. Unalazimisha kilia mtu aamini unachoamini wewe huo ni ujinga wa hali ya juu. Nimetolea mfano hapo Kenya walipata katiba mpya lakini matatizo yao yapo palepale hakuna kilochobadilika zaidi ya uhuru wa maandamano.

Elewa ndugu usifuate mkumbo wa wana siasa iwe ccm au chadema maendeleo hayaletwi na katiba mpya bali huletwa na kiongozi mwenye uzalendo na uthubutu. Tumeona hiko Arusha kero za wananchi zinatatuliwa na mkuu wa mkoa kwa kutumia katiba hii hii mnayoiita mbovu kwani kabla ya hapo Arusha likuwa haina kiongizi na katiba?. Inahitaji kutumia akili ya hali ya juu kunishawishi kuwa katiba mpya ni tiba ya natatizo ya wananchi na sio kuleta matusi yako hapa.

Mfano serikali kuhamia Dodoma ilitakiwa kufanyika toka miaka ya 70 uko lakini haikuwezekana, bwana la Mwl. Nyerere lilitakiwa kujengwa toka miaka ya 70 huko lakini haikuwezekena, sasa kaja JPM. kafanya haya yote kwa katiba hii hii unaniaminishaje mimi kuwa jatiba ndio muarobaini wetu badala ya kuniamibia kiongozi mzalendo aina ya JPM.

Nakazia tena katiba mpya sio muarobaini wa matatizo ya wananchi kama mnavyoaminishwa na wanasiasa bali ni muarobaini wa matatizo ya vyama vya sisiasa ila mmejifichia kwa wananchi.

Sisi wananchi tukipata kiongozi mzalendo mwenye kalba ya JPM tunajua matatizo yetu na ya nchi yanakwisha sisi hatupo kwa ajili ya kufia chama kama wewe tupo kwa ajili ya nchi na maslahi ya nchi, tena ushike adabu yako usiishi kwa kujipendekeza kwenye vyama wala wana siasa nyie ndio mnaochelewesha maendeleo ya hii nchi.
maelezo mengi alafu umeandika ujinga.wewe kenya ulichoona ni maandamano tu.Ata huo uhuru wakuandamana uoni kama ni faidaza hiyo katiba hatua mojawapo yakuifanya serikali yao iwajibike kwa wananchi.Tumia akili zako kufikiria mbali.Walioweka katiba hawakua wajinga na katiba bora ndio msingi wa maendeleo.
 
Usome mwenyewe
---

Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWANANCHI
PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Tamaa sn, Msigwa anatamaa kupita kiasi
 
maelezo mengi alafu umeandika ujinga.wewe kenya ulichoona ni maandamano tu.Ata huo uhuru wakuandamana uoni kama ni faidaza hiyo katiba hatua mojawapo yakuifanya serikali yao iwajibike kwa wananchi.Tumia akili zako kufikiria mbali.Walioweka katiba hawakua wajinga na katiba bora ndio msingi wa maendeleo.
Huna akili wewe Kenya wameanza kuandamana leo baada ya katiba mpya huko nyuma hawakuwahi kuandamana na kuuana hata leo baada ya katiba mpya hawaandamani na kuuana? Nini kimebadilika sasa hapo?
 
Lisu anopoteza muda tu CHADEMA, aelekee ACT kama kweli anataka kuendelea mapambano
 
Tofauti za kiitikadi siyo uadui, ni mitazamo tofauti ya kufikia malengo.
Hujui maana ya falsafa. Hunielewi athari ya falsafa.

Ndio hii inayowafanya naweza kusema nusu ya watendaji wa serikali kuwachukia wanaharakati, wanasiasa na waislam wenye maoni tofauti na wao.

Chuki hizi wanajificha kwa mgongo wa sera, mipango na sheria na kikatiba.

Kesi za ugaidi, kutekwa kwa wanaharakati na watu wasiojilikana ni ushahidi tosha kuna kundi la watumishi wa serikali wenye akili ndogo na uwezo mdogo wa kufikiri kuwachukia makundi ya watu wenye akili tz.

Na kwa opinion ya wengi na opinion yangu kuna wahuni, walevi ndani ya serikali
 
Lissu inaonekana hana washauri wazuri kisiasa na qnatumia sana hisia kwenye siasa kuliko akili.
Kuhusu "washauri wazuri" ninakubaliana na wewe. Hili linaweza kuja kumdidimiza, kwa sababu sasa atakuwa anawekewa mitego ya kumnasa na kumdhoofisha/kumdhibiti, hata huko ndani ya chama chake.

Kuhusu "hisia na akili", haya ni magumu kuyachambua na kuyatenganisha. Sina hofu kuhusu "akili" ya Lissu. Ni mtu mwenye uelewa mzuri wa mambo.
 
Kofia ya uenyekiti itenganishwe na urais utapata majibu ya dhati.
Mkuu, siku kofia ya Mwenyekiti wa Chama kinacho isimamia Serikali ikitenganishwa na kofia ya Urais wa Nchi basi ndio siku itakuwa ya kuanza kuyaona maendeleo halisi ya nchi.
 
Back
Top Bottom