Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu atakuwa kaumia sana, ila Mchungaji naye katumia hasira baada ya kuukosa uenyekiti kanda ya Nyasa. Nina Imani kabisa, atarudi tu tena Chadema... Time will tell...
Ndo tatizo letu ngozi hii, UNAFIKI! Kila mtu anajifahya kuzungumzia 'kuukosa uenyekiti' katika kujaribu kutafuta uhalali wa kumshambulia Msigwa na kufurahisha 'herd' ya nyumbu wa mbowe, lakini kamwe hajuna anayezungumzia hoja za uharamia ulioasisiwa juu kabisa aliokuwa anafanyiwa!! Shida
 
Usome mwenyewe
---

Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWANANCHI
PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Wanatuzuga tu!
 
Lisu mwenyewe kama anakili kweli..anatakiwa atoke kwenye hiyo kampuni ya wachxga iliyovaa koti la chama cha kisiasa,bora aende ACT wazalendo..Lissu anatumika pale kama punda mbeba mizigo tu..ila bado hajitambui.
Acha umbea mtoto wa kiume utasomwa jicho hivi Tundu Lissu akiwa peke yake ni sawa mabasi mangapi ya wajumbe wa kamati kuu ccm? Hata mkijikusanya ccm woote bado uwezo wa Lissu utakuwa mkubwa saaaana more than thousand miles away!
 
Kama nyumbu wenyewe huwa kuna kipindi wanahamia Masaimara kutokea Serengeti sasa ajabu ni ipo mwanasiasa akihama chama? Tatizo la upinzani hasa chadema wanajiona wao ni malaika na ndio wakombozi wa watanzania kumbe hamna lolote zaidi ya kukipigania chama zaidi ya watanzania. Kila siku wao wanapigania katiba mpya kwa ajili ya maslahi ya kisiasa badala kupigania mambo ya msingi ambayo ndio yanagusa maisha ya watu halafu eti wanataka watu waungane nao kwenye maandamano.
 
Ndo tatizo letu ngozi hii, UNAFIKI! Kila mtu anajifahya kuzungumzia 'kuukosa uenyekiti' katika kujaribu kutafuta uhalali wa kumshambulia Msigwa na kufurahisha 'herd' ya nyumbu wa mbowe, lakini kamwe hajuna anayezungumzia hoja za uharamia ulioasisiwa juu kabisa aliokuwa anafanyiwa!! Shida
Sasa mtu kapewa hela za mama abduli unategemea angepata huo uwenyekiti kanda ya nyasa angefanya kazi ya nani? CHADEMA walipewa taarifa zote kutoka ccm wakapiga chini hilo jambazi na sasa limerudi kwa bosi wake alekuwa akimtuma. Watu husema muungwana akivuliwa nguo huchutama sasa yeye kaamua kutimua mbio
 
Kama nyumbu wenyewe huwa kuna kipindi wanahamia Masaimara kutokea Serengeti sasa ajabu ni ipo mwanasiasa akihama chama? Tatizo la upinzani hasa chadema wanajiona wao ni malaika na ndio wakombozi wa watanzania kumbe hamna lolote zaidi ya kukipigania chama zaidi ya watanzania. Kila siku wao wanapigania katiba mpya kwa ajili ya maslahi ya kisiasa badala kupigania mambo ya msingi ambayo ndio yanagusa maisha ya watu halafu eti wanataka watu waungane nao kwenye maandamano.
Wewe ni mpumbav kabisa kwa hiyo katiba haigusi maisha ya watu? Kumbe ndo maana ccm mnakimbilia kwenye utekaji na ulozi, yaani kubwa zima umeolewa kumbe hujui hata bandar imeuzwa kwa kuegemea katiba mbovu halafu wewe hujui kama katiba imebeba maisha yako? Puuumbav kabisa
 
Moja ndio ila c unaona kabisa kuna sura mpya, kwan kwa hapo chini hua wanachapa form ngapi?
Inawasaidia nini wananchi ambao hawana hata uhakika wa milo mitatu?
 
Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”
Duh!

Tundu Lissu, mbona unajishusha chini kiasi hicho?
Huyo naye ni mtu wa kupotezea muda tena kumzungumzia; ili iweje? Kaondoka na nini CHADEMA na sasa kakiwasilisha CCM kinachoweza kukusumbua akili hadi umzungumzie huyo?

Sawa. Kama inabidi, ni maneno mawili matatu na kumaliza kazi basi; na kuendelea na mengine ya muhimu zaidi ndani ya chama.

Na unajua, hakuna lililo muhimu zaidi kwa sasa kama kuiondoa CCM madarakani. Usikubali kupoteza lengo hili kwa hadaa za kushirikishwa ndani ya serikali ya 'Chura Kiziwi' kwa njia yoyote ile. Ni bora kabisa hata kubaki nje ya hiyo serikali , kuliko kushirikiana na shetani.
Chunga namba, unadhibitiwa sasa.
 
..wako wanaCcm wanamchukulia Tundu Lissu kama adui yao.

..ndio maana baadhi yao walijaribu kumuua.

..Na wengine wamegoma kuwachukulia hatua waliotaka kumuua.
Nikitazama ramani za siasa naona hakuna mtu anaye hofiwa zaidi sasa hivi huko CCM kuliko Tundu Lissu.
Labda ajitokeze mwingine baadae, lakini kwa sasa hivi Tundu Lissu ndiye mpinzani anayeleta hofu kubwa huko kwa Bi 'Chura Kiziwi'.
 
Lisu mwenyewe kama anakili kweli..anatakiwa atoke kwenye hiyo kampuni ya wachxga iliyovaa koti la chama cha kisiasa,bora aende ACT wazalendo..Lissu anatumika pale kama punda mbeba mizigo tu..ila bado hajitambui.
Naungana nawe, lissu aende ACT - WAZALENDO!
 
Wewe ni mpumbav kabisa kwa hiyo katiba haigusi maisha ya watu? Kumbe ndo maana ccm mnakimbilia kwenye utekaji na ulozi, yaani kubwa zima umeolewa kumbe hujui hata bandar imeuzwa kwa kuegemea katiba mbovu halafu wewe hujui kama katiba imebeba maisha yako? Puuumbav kabisa
Akili huna wewe umejawa matusi tu, uwe unatumia akili kidogo. Sasa ngoja nikuelimishe kidogo wewe unayeishi kwa kufuata mkumbo wa wanasiasa. Kipaumbele cha wananchi sio katiba kama ilivyo kwa wanasiasa kwa sasa upo hapo? Wanasaiasa wanadai katiba kwa ajili ya uchaguzi na ndio maana Rais Kikwete alipowapa nafasi ya kaunda katiba mpya wanasiasa walivurugana huko bungeni hasa ccm na chadema wote walionekana kulinda maslahi ya vyama vyao kuliko kuweka mambo muhimu ya wananchi. CCM waliiangalia ni mambo gani yawepo kwenye katiba yatakayowafanya waendelee kutawala huku chadema wakitaka katiba ambayo itaweza kuwafanya wao waingie madarakani kiurahisi wanasahau ya kuwa watakaowafanya waingie madarakani ni wananchi na wala sio katiba mpya.

Katiba mpya haiwezi ondoa njaa wala tatizo la ajira, au kuleta maendelo kama mnavyoaminishwa, hayo mambo yanaletwa na kiongozi mwenye uzalendo, maono na utashi. Kenya waliunda katiba mpya kule kwao lakini haijaweza kuondoa njaa na tatizo la ajira kwa vijana na unaona kinachomtokea Ruto huko.

Mnachotaka nyie ni katiba atakayiruhusu maandamano na kwenda mahakamani mkishindwa uchaguzi na huo ndio ukweli, mpo kwa ajili ya kutafuta vyeo, madaraka na kujaza wabunge wengi huko bungeni na wala sio kwa maslahi yetu sisi wananchi hili tuliligundua pale mlipo mpinga JPM kwa kila jambo hata lenye maslahi kwa nchi. Hivi sasa watu wamepoteza imani na nyie ndio maana mama kawapa nafasi ya kuandama kama mlivyokuwa mnadai muda wote mmekosa waandamanaji mmeacha.
 
Sasa ngoja nikuelimishe kidogo wewe unayeishi kwa kufuata mkumbo wa wanasiasa. Kipaumbele cha wananchi sio katiba kama ilivyo kwa wanasiasa kwa sasa upo hapo?
Duh! Wewe mpuuzi huna tofauti na mnyama wa porini na heri ungeishi porini kama wanyama wenzio wasio na akili. Binadamu aliyejaaliwa akili, hawezi kuandika ujinga kama huu wa kwako. Sidhani unaelewa hata Katiba ni nini. Ngoja niachie hapo kwani kujadiliana na wewe ni heri kujadiliana na meza au kiti!
 
Siasa za Tanzania hazitofautiani sana na ligi kuu ya Tanzania, zina msimu wa usajili.
 
Usome mwenyewe
---

Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWANANCHI
PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Msigwa amefuata kanuni za wamarekani hawana Adui wakudumu wala rafiki wakudumu ila wana maslai ya kudumu msigwa alipo ona maslai yake yameisha CDM na wamemjenga kiasi cha kutosha akaamua kuhamia CCM ili akapate maslai mapya nako maslai yakiisha anaweza akaimarisha kanisa lake na huko akaendelea kupata maslai. Kwahiyo ni mru anayepiga mahesabu mazuri kwa ajili ya maslai yake na familia yake. Wenzake wakina Katambi waitara wanakula kuku tu yeye amechelewa angehamia kipindi cha Magufuli huwenda hivi sasa angekuwa mbali kimaslai.
 
Back
Top Bottom