Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Pre GE2025 Lissu kuhusu Msigwa kuhamia CCM: Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na
Lissu atakuwa kaumia sana, ila Mchungaji naye katumia hasira baada ya kuukosa uenyekiti kanda ya Nyasa. Nina Imani kabisa, atarudi tu tena Chadema... Time will tell...
Na inasikitisha kuona jinsi Msigwa alivyotembezwa katikati ya high table, wakati wa kutambulishwa kwenye chama mithili miss Tanzania
 
Kuna huyu
20240703_064541.jpg
 
Huyo hapo analia kujutia upuuzi aliofanya. Kalipwa mamia ya mamilioni lakini hana amani ya moyo
Watu wanasema pesa sabuni ya roho lakini pesa ya Mama Abdul kwa Msigwa imekuwa shubiri hana amani kabisa, ndugu zake wamchunge sana asije akajinyonga kama alivyofanya Yuda baada ya kupokea hela za malipo ya kumsaliti Bwana Yesu.
 
Lissu kaumia sana na Lema alilia sana kuhusu Msigwa kuhamia CCM, ila najua kabisa wazi. Lissu au Lema wanajua kabisa wana uchungu mkubwa ndani ya Chadema hakuna demokrasia ya kweli hasa katika kumpata Mwenyekiti wao au hata wenyeviti wa kanda, ni rushwa sana, ubabe sana na ukitaka kugombea uenyekiti Taifa wa Chadema basi wewe utakuwa msaliti mkubwa sana..!! Ni sbb tu hawana pa kwenda wanakufia na tai shingoni huko huko Chadema..!!
 
Kikubwa amehama baada ya kula mkwanja pesa nzuri hata ingekuwa ni mimi. ila anyamaze kimya akiwa anameza alichokula. pitia tend ya Musukuma
 
Lissu kaumia sana na Lema alilia sana kuhusu Msigwa kuhamia CCM, ila najua kabisa wazi. Lissu au Lema wanajua kabisa wana uchungu mkubwa ndani ya Chadema hakuna demokrasia ya kweli hasa katika kumpata Mwenyekiti wao au hata wenyeviti wa kanda, ni rushwa sana, ubabe sana na ukitaka kugombea uenyekiti Taifa wa Chadema basi wewe utakuwa msaliti mkubwa sana..!! Ni sbb tu hawana pa kwenda wanakufia na tai shingoni huko huko Chadema..!!
Hayo ni mawazo yako je fomu moja ya Rais CCM haiwaumi wengine. Demokrasia ni ngumu sana
 
Usome mwenyewe
---

Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWANANCHI
PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Atakaa sawa tu na yeye asiishi maisha ya maigizo
 
Akili huna wewe umejawa matusi tu, uwe @konyola unatumia akili kidogo.

Sasa ngoja nikuelimishe kidogo wewe unayeishi kwa kufuata mkumbo wa wanasiasa.

Kipaumbele cha wananchi sio katiba kama ilivyo kwa wanasiasa kwa sasa upo hapo?

Wanasaiasa wanadai katiba kwa ajili ya uchaguzi na ndio maana Rais Kikwete alipowapa nafasi ya kaunda katiba mpya wanasiasa walivurugana huko bungeni hasa ccm na chadema wote walionekana kulinda maslahi ya vyama vyao kuliko kuweka mambo muhimu ya wananchi.
100%✓
CCM waliiangalia ni mambo gani yawepo kwenye katiba yatakayowafanya waendelee kutawala huku chadema wakitaka katiba ambayo itaweza kuwafanya wao waingie madarakani kiurahisi wanasahau ya kuwa watakaowafanya waingie madarakani ni wananchi na wala sio katiba mpya.
Yaani☝🏿huo ndio ukweli. Wanaumia chawa wa CHADEMA😂
Katiba mpya haiwezi ondoa njaa wala tatizo la ajira, au kuleta maendelo kama mnavyoaminishwa, hayo mambo yanaletwa na kiongozi mwenye uzalendo, maono na utashi.
100%✓
Kenya waliunda katiba mpya kule kwao lakini haijaweza kuondoa njaa na tatizo la ajira kwa vijana na unaona kinachomtokea Ruto huko.
Hakika
Mnachotaka nyie ni katiba atakayiruhusu maandamano na kwenda mahakamani mkishindwa uchaguzi na huo ndio ukweli, mpo kwa ajili ya kutafuta vyeo, madaraka na kujaza wabunge wengi huko bungeni na wala sio kwa maslahi yetu sisi wananchi
Inatakiwa Watanzania wote wasome hapo Juu☝🏿
hili tuliligundua pale mlipo mpinga JPM kwa kila jambo hata lenye maslahi kwa nchi.
Walimuua. Uchunguzi utafanyika. Na ni lazima ufanyike.
Hivi sasa watu wamepoteza imani na nyie ndio maana mama kawapa nafasi ya kuandama kama mlivyokuwa mnadai muda wote mmekosa waandamanaji mmeacha.
Wananchi washagundua hawa CHADEMA ni vInara wa siasa za majitaka tu. Hawana sera
===================

Kazia hapo hapo Mkuu.

Wanakuelewa hawa manyumbu ila wanajiondoa ufahamu tu.

Na ukitaka kujua ujumbe wako umefika, tizama mitusi yao juu ya ulichokiandika.

Kanyaga piga ua. Kazia hapo hapo. Konyo zao kabisa.
 
Usome mwenyewe
---

Siku chache tangu Mchungaji Peter Msigwa kutimkia Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo akisema: “Kwa kujiunga na maadui zangu wa kisiasa, sasa nitalazimika kukutana naye kama hasimu wake wa kisiasa.”

Lissu amesema hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 ikiwa ni siku nne zimepita tangu Mchungaji Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa kutimkia CCM.

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM Juni 30, 2024 mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWANANCHI
PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Atakaa sawa tu na yeye ipo siku mtamsikia na yeye kahamia ccm
 
Duh!

Tundu Lissu, mbona unajishusha chini kiasi hicho?
Huyo naye ni mtu wa kupotezea muda tena kumzungumzia; ili iweje? Kaondoka na nini CHADEMA na sasa kakiwasilisha CCM kinachoweza kukusumbua akili hadi umzungumzie huyo?

Sawa. Kama inabidi, ni maneno mawili matatu na kumaliza kazi basi; na kuendelea na mengine ya muhimu zaidi ndani ya chama.

Na unajua, hakuna lililo muhimu zaidi kwa sasa kama kuiondoa CCM madarakani. Usikubali kupoteza lengo hili kwa hadaa za kushirikishwa ndani ya serikali ya 'Chura Kiziwi' kwa njia yoyote ile. Ni bora kabisa hata kubaki nje ya hiyo serikali , kuliko kushirikiana na shetani.
Chunga namba, unadhibitiwa sasa.
Lissu inaonekana hana washauri wazuri kisiasa na qnatumia sana hisia kwenye siasa kuliko akili.
 
Lisu mwenyewe kama anakili kweli..anatakiwa atoke kwenye hiyo kampuni ya wachxga iliyovaa koti la chama cha kisiasa,bora aende ACT wazalendo..Lissu anatumika pale kama punda mbeba mizigo tu..ila bado hajitambui.
Lissu asipozingatia huu ushauri wako atakuja kujuta.
 
Back
Top Bottom