Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema hana muda wa kupoteza na kukaa na Mzee Wassira ni kupoteza muda. Amesema hayo wakati akihojiwa katika Kipindi ya Dakika 45 cha ITV baada ya kuulizwa swali kuwa anaonekana namkwepa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wassira aliyesema anamuhitaji Lissu kwenye Mdahalo
Lissu amesema muda alionao na kazi anayotakiwa kufanya, muda ni mfupi sana. Hivyo kama kuna jambo la kujadili basi watajadili na Rais Samia sio Wassira.
Amesema "Tumezungumza na Mzee Kinana mwaka mzima, na Rais Samia alisema tutakachokubaliana na Mzee Kinana na timu yake watakitekeleza, tukajadiliana mwaka mzima kisha wakasema hawataki baada ya kutupoteze muda mwaka mzima. Sasa nazungumza na Stephen Wassira nini? Yeye sio mtu wa kufanya maamuzi, haya maamuzi hayafanywi na CCM wala, yanafanywa na Samia na Serikali yake."
Amemalizia "Wassira atatupotezea muda tu!"