LGE2024 Lissu: Kukamatwa kwa Mbowe iwe fundisho tusirudie kudanganywa danganywa

LGE2024 Lissu: Kukamatwa kwa Mbowe iwe fundisho tusirudie kudanganywa danganywa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sasa Lissu anashangaaje Hawa kumdanganya Adam,

Au Delila kumdanganya Samsoni🤔

Mbona hashangai Yeye kudanganywa na Luwasa walipomsafisha chama kizima kwamba sio fisadi?
 
Huyu mwamba namkubli sana,ila nina wasi wasi siku si nyingi wanaweza wakamuua.
 
ukivuruga ratiba za kampeni maana yake unavuruga shughuli na kazi za wengine wasio husika na kampeni zako.

Lazima wakati kampeni zinaendelea na shughuli za wasio husika zinaendelea kwa amani bila fujo.

kukiuka ratiba a kukaidi maelekezo ni kuchochea vurugu na kuvuruga amani katika eneo husika.

Ustaarabu ni kitu cha bure 🐒
Nani asiehusika anavurugiwa utaratibu? Je amelalamika?
 
Inashangaza sana ni kwa nini CHADEMA na vyama vya upinzani vimejitoa kwenye reli. Huu uchaguzi na ule unaofuata hauna maana yoyote bila kuwa na Katiba mpya. Nchi hii inahitaji kukarabatiwa upya na kuweka misingi mipya ya utawala. Nchi inahitaji kuwekwa kwenye "Reset mode" hadi tuwe na misingi ya utawala wa sheria zitakazowekwa na watu kwa ajili ya watu.

Nini kifanyike?.... 1. Katiba mpya ili uchaguzi wa 2025 uwe na masharti yatokanayo na katiba hiyo mpya.
2. Kura ya maamuzi kuhusu muundo wa muungano wa Serikali tatu, au Serikali moja.
3. Kutengeneza mfumo bora wa kupata viongozi kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi.

Hatujachelewa, hata kama uchaguzi wa Serikali za mitaa utalazimishwa kama inavyoonekana, Uchaguzi wa Rais na wabunge unapaswa kuahirishwa hadi mambo matatu yaliyotajwa hapo juu yakamilike. Utawala uliopo sasa kwa maana ya Rais na chama kinachotawala waendelee kuongoza kama Serikali ya mpito ili kukamilisha kazi iliyoko mbele yetu.
 
Nani asiehusika anavurugiwa utaratibu? Je amelalamika?
hakuna haja ya vyombo vya ulinzi na usalama eti kusubiri uharibifu utokee au malalamiko ya waathirika ndipo vichukue hatua. Hilo litakua sio jeshi sasa.

yaani usuburi uharibifu ndio uchukue hatua? hiyo itaku ni useless na completely nonsense sasa, alaaa 🐒
 
hakuna haja ya vyombo vya ulinzi na usalama eti kusubiri uharibifu utokee au malalamiko ya waathirika ndipo vichukue hatua. Hilo litakua sio jeshi sasa.

yaani usuburi uharibifu ndio uchukue hatua? hiyo itaku ni useless na completely nonsense sasa, alaaa 🐒
Watanzania ni watu waliostaarabika hawawezi kufanya muwazanyo nyie
 
Watanzania ni watu waliostaarabika hawawezi kufanya muwazanyo nyie
vyombo vya ulinzi na usalama vinatekeleza majukumu yao mazito kwa mujibu wa sheria, kanuni na tararibu zilizoko,

jeshi la police halifanyi kazi kadiri ya mawazo yako au ya mwingine. Linasimamia ustaarabu wa kila moja kufanya mambo yake kwa Amani 🐒
 
Yuko sahihi, Mbowe ndio muasisi wa MARIDHIANO FAKE. Alitukosea sana na kuvunja "morale" yetu ya kudai KATIBA MPYA, kwa kweli acha tu avune alichokipanda.
 
Chadema tambueni kwamba mpo vitani, kulalamika tu kwa maneno matupu haitwasaidia kitu. Chukueni hatua madhubuti ili kukomesha udhalimu huo mnaofanyiwa, tumechoka kusikia malalamiko yenu ya maneno matupu miaka yote.


"The right cannot be given as a gift by the oppressor, it must be demanded by the oppressed."

Dr. Martin Luther King Jr.
Hapo ulipo wewe, unalo wazo gani kichwani unaloweza kuwa shauri CHADEMA walifanye sasa hivi kuliko wanavyo fanya.

Huku kuandika maneno yenye hisia bila kutazama hali ilivyo unadhani kutasaidia kitu gani?

Naona unam-'quote' Dr King, lakini haionyeshi kuwa unaelewa alicho kuwa akifanya yeye.

Hayo maandamano pekee; tena ya kuonyesha tu hali mbaya iliyopo uliona matokeo yake yalivyo kuwa; sasa leo wewe hapa unakuja na vimaneno hapa, vitasaidia kitu gani.
Ni kama upo kwenye mpango wa kuwahimiza CHADEMA wajimalize haraka kwa kutotumia akili unako wahimiza wewe wakufuate.
 
Back
Top Bottom