Kwa muda mrefu sana nimewaasa CDM kwamba ni wakati Mbowe aondoke.
Mbowe ameishiwa mbinu hana nguvu za uongozi wala maono mapya.
Mbowe anafahamu chaguzi huleta matatizo kwa vyama vyote, kwa uzoefu wa siku za nyuma na kwingine.
Uchaguzi wa kanda ya nyanda za juu ulikuwa na kila dalili ya kuanza matatizo, haukutakiwa kufanyiwa mzaha.
Ni ima Mbowe alitaka au alikaa kimya ili kutaka. M/Kiti Mbowe alivyosimamia suala hilo ni hovyo sana.
Baada ya Msigwa kuhama Mbowe akijitokeza kutoa kauli '' kuwa upinzani si kazi rahisi''
Ni moja ya kauli za kipuuzi kwasababu alitakiwa azuie madhara na si kuja kudanganya watu na vimameno
Ni maneno ya hovyo kama aliyosema '' Ukraine ipo vitani na Russia lakini wanaongea kuhusu suluhu' akishadidia maridhiano ya kipuuzi yaliyoishia na aibu kwake kwa kutapeliwa kitoto.
Tuhuma za TAL kuhusu rushwa ni kubwa na zinapaswa kuwa addressed. Mbowe kajificha mtifuano ukiendelea.
Alijificha katika chaguzi nyingine hadi akina Lema wakajitoa.
Kwa ufupi kuna kila dalili Mbowe ana '' orchestrate' haya mambo kwa faida anazozijua
Mbowe amekuwa Mwenyekiti kwa miaka 30 hana sababu za kuendelea.
Ikiwa katiba na anataka, Mbowe akubali ushindani na aache kutumiaVijana kuzua '' frustrations'
Mzee Mtei hakukaa miaka 30, Bob Makani hakukaa miaka 30, ' 'MBOWE MUST GO'
Mbowe akiwa Magereza CDM ili imarika kama taasisi tena TAL akiwa nje.
Harakati za katiba zilipamba moto. Mbowe alipotoka na kukimbilia Ikulu kila jambo limevia!
Mbowe ni polazrizing figure, he must go.
Habari za kurudi kwa COVID 19 '' behind the scenes'' Mbowe anaziingiza kiani! Huo ni ukweli
Mnakumbuka aliposema wiki chache zilizopita ''... ni wakati watu wasameheane katika chama..''
CDM kama mnataka chama imara, simameni katika ukweli.
Msitafute mchawi CCM au JF, mkabilini Mwenyekiti na kumwambia ukweli. Thank you for everything, it's time you pack an go.! Mbowe anapasua chama akitumia kikundi cha Vijana wake wasiotaka ukweli.
Pascal Mayalla JokaKuu