Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Rais wa chama cha wanasheria nchini na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ataongoza jopo la mawakili 29 watakaomtetea Wakili Fatma Karume Katika Kesi Yake Ya Kushikwa Mwili Wake Bila Ya Ridhaa, Kuvutwa Kwa Nguvu Na Kusababishiwa Madhara Katika Bega Lake.

Katika Kesi Hiyo Iliyofunguliwa Mahakama Kuu Ya Tanzania, Bi.Fatma Anamdai Fidia Ya Shilingi Bilioni Moja, Inspekta Eugen Mwampondela Wa Kituo Kikuu Cha Polisi DSM. Fatma Karume amshtaki Polisi aliyemzonga Mahakamani, adai fidia ya bilioni moja

Kesi Itakapoanza Kusikilizwa, Mtuhumiwa Atatakiwa Kuwepo Kizambani Kujieleza Na Kujibu Maswali.

My Take
Cross Examination za Tundu Lissu hazijawahi kumuacha askari salama
 
..Kushikwa Mwili Wake Bila Ya Ridhaa, Kuvutwa Kwa Nguvu Na Kusababishiwa Madhara Katika Bega Lake''

Sijui kwa nini vilaza wale hawakupeleka maWP kumshikashika mama mwenzao? mbali na kumshikashika na ''kumtengua bega'', kumtoa ''afisa wa mahakama'' kwenye eneo lake la kazi na ''kumzuia kutimiza wajibu wake'' kwa style ile ni kosa la jinai🙂
 
Kwa kweli huyo askari kakosea sana, Hakupaswa kumshika hivyo, Sasa atajuta ,Mahakamani akieleza ni maagizo toka juu amshike mithli ya Mke wake sijui watamuachia huru?Ifike mahla polisi na Ma DC watumie vyema mamlaka yao vinginevyo watajikuta wanashitakiwa kama watu binafsi, Maana aliyewateua hakuwaagiza wakavunje sheria. Wawe makini
 
Yeyote atakayepeleka kesi ya kipuuzi namna hii kwenye mahakama tukufu na wote watakaomtetea wafutiwe leseni ya uwakili na kunyang'anywa muhuri!

Mahakama ndiyo yenye jukumu la kutoa haki na hivyo ili jambo lionekane ni la kipuuzi mahali ambapo wengine wanadai si la kipuuzi ni muhimu jambo hilo kupelekwa kwenye chombo huru na mahakama ndiyo mahali pake under the circumstance. Upo hapo?
 
Back
Top Bottom