Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Siku hizi chadema makao makuu yamehama kutoka ufipa mpaka kwenye viwanja vya mahakama kila nikijaribu kumzoom Lissu namuona kama harmorapa wa kwenye siasa ambae yupo radhi kujitoa ufahamu na kuzivua nguo akili zake kwa ajili ya kukaa front page kwenye magazeti

Hata siku moja sito mshauri ndugu yangu asome sheria kama wanasheria wanaitwa wasomi ni aina ya Lissu
 
Yeyote atakayepeleka kesi ya kipuuzi namna hii kwenye mahakama tukufu na wote watakaomtetea wafutiwe leseni ya uwakili na kunyang'anywa muhuri!
Huku wananchi kwenye jimbo la Tundu Lissu wakiwa na kero za kufa mtu yeye yuko Dar akifanya mambo ya kitoto kama haya?! Ujinga na uzuzu kabisa..Yazidisha kuaminika kweli ukikosa sera na ilani matokeo yake ndiyo hayaa...
 
Tanzania kuna mambo yanachanganya sana......

Zote kesi za kiuni hizi zimesababishwa na kutumia nguvu bila kutumia akili ......

Matokeo yake ndio haya tunashuhudia vituko toka pande zote sio serikali sio wapinzani......

Hivi kweli kipaumbele chetu ni kesi za kuvutana mabega?

Hivi serikali ya viwanda itapatikana kwa kupoteza rasilimali za nchi kwenye kesi za kiuni kama hizi..

Kulikuwa na haja gani ya kuwa na kesi za Lissu ,Mdee, sijui Mbowe, Bulaya, Kafulila na wengine zaidi ya 10 ndani ya miaka miwili ya utawala wako.........

Ukiangalia kesi zote zinafanana na zinatumia kodi ya nchi.. .....

Kipaumbele cha Rais wa wanyonge ni nini hasa?... .....

Kwanini hizi pesa tusiwape mawakili wetu wapambane kwenye kesi za wahujumu uchumi kama ambavyo tunakabiliwa na kesi nzito ya IPTL?....
 
Sijui kwa nini vilaza wale hawakupeleka maWP kumshikashika mama mwenzao? mbali na kumshikashika na ''kumtengua bega'', kumtoa ''afisa wa mahakama'' kwenye eneo lake la kazi na ''kumzuia kutimiza wajibu wake'' kwa style ile ni kosa la jinai🙂
Na mwanzoni tu alimkumbatia kama mkewe vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeyote atakayepeleka kesi ya kipuuzi namna hii kwenye mahakama tukufu na wote watakaomtetea wafutiwe leseni ya uwakili na kunyang'anywa muhuri!
Mbona wanasiasa wa mlango kushoto wakitoa maoni yao mbele ya hadhara wanafunguliwa mashitaka ya kosa la kufanya uchochezi? Kama hii kesi unaona ni upuuzi basi mliuanzisha nyie hawa mawakili wanaundeleza[emoji16] [emoji16] [emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku wananchi kwenye jimbo la Tundu Lissu wakiwa na kero za kufa mtu yeye yuko Dar akifanya mambo ya kitoto kama haya?! Ujinga na uzuzu kabisa..Yazidisha kuaminika kweli ukikosa sera na ilani matokeo yake ndiyo hayaa...
Mambo ya kitoto hayo ni yepi? Ina maana ww hujui kuwepo kwako hapo ulipo na kwenda uendako kwamba kuna watu walipambana? Mama yako anaenda sokoni bila kushikwa matako kwa kua kuna watu walijitoa kupambana...Kwahiyo unataka police wendelee kuwashikashika wanawake kisa wao police?
Sheria inataka police wa kike ndio awe na mtuhumiwa mwanamke na wa kiume kwa wakiume...
Kinachofanyika pale ni kuweka heshima kwa jinsia na kazi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa chama cha wanasheria nchini na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ataongoza jopo la mawakili 29 watakaomtetea Wakili Fatma Karume Katika Kesi Yake Ya Kushikwa Mwili Wake Bila Ya Ridhaa, Kuvutwa Kwa Nguvu Na Kusababishiwa Madhara Katika Bega Lake.
Katika Kesi Hiyo Iliyofunguliwa Mahakama Kuu Ya Tanzania, Bi.Fatma Anamdai Fidia Ya Shilingi Bilioni Moja, Inspekta Eugen Mwampondela Wa Kituo Kikuu Cha Polisi DSM.
Kesi Itakapoanza Kusikilizwa, Mtuhumiwa Atatakiwa Kuwepo Kizambani Kujieleza Na Kujibu Maswali.


Tusubiri tuone...but the way I see it something big is building up...And whether this will be beneficial to 'Lissu and others' it is something we are 'bound' to know/learn/ hear soon.... Uzuri wa sheria ndivyo ulivyo...ndege mjanja hunaswa kwenye tundu bovu, wahenga walisema
 
Kwa hali hii inaonyesha vijana wa kitanzania na wasomi mmekosa vya kufanya kesi kama hiyo mawakili 29 na inaonyesha ni jinsi gani kuwa mawakili hawajiamini na usomi wao. Wasilete kisingizio cha mshikamano bali ni kutokujiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbele ya bilioni Moja, hata Mimi ningekua wakili ningejiunga kwenye Kesi tena usawa huu wa njaa
 
Back
Top Bottom