Tanzania kuna mambo yanachanganya sana......
Zote kesi za kiuni hizi zimesababishwa na kutumia nguvu bila kutumia akili ......
Matokeo yake ndio haya tunashuhudia vituko toka pande zote sio serikali sio wapinzani......
Hivi kweli kipaumbele chetu ni kesi za kuvutana mabega?
Hivi serikali ya viwanda itapatikana kwa kupoteza rasilimali za nchi kwenye kesi za kiuni kama hizi..
Kulikuwa na haja gani ya kuwa na kesi za Lissu ,Mdee, sijui Mbowe, Bulaya, Kafulila na wengine zaidi ya 10 ndani ya miaka miwili ya utawala wako.........
Ukiangalia kesi zote zinafanana na zinatumia kodi ya nchi.. .....
Kipaumbele cha Rais wa wanyonge ninini hasa?... .....
Kwanini hizi pesa tusiwape mawakili wetu wapambane kwenye kesi za wahujumu uchumi kana ambavyo tunakabiliwa na kesi nzito ya IPTL?....