Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

hopefully jeshi la polisi halikumtuma kufanya aliyoyafanya
apart from kua alipitia mafunzo ccp
Pole yake
kwa arakaaraka naona kesi ya kujibu ipo
 
Lisuphobia disease niungonjwa mpya na unasambaaa kwa haraka sana....dalili ya kwanza ni kuhemka...
 
Ni haki yake Bi Fatma kama anaona ametendewa kinyume na sheria na askari yule, but hii ya mawakili 29 eti kumtetea inadhihirisha namna hawa mawakili wetu wanavyoshindwa kuchambua mambo ya msingi ya kuwaunganisha pamoja. Ningewaona wenye busara endapo mawakili hao 29 wameungana kuwatetea wale wabunge wa CUF waliotemeshwa ubunge na purofeseri anaetambuliwa na msajili wa vyama.
 
Sijui kwa nini vilaza wale hawakupeleka maWP kumshikashika mama mwenzao? mbali na kumshikashika na ''kumtengua bega'', kumtoa ''afisa wa mahakama'' kwenye eneo lake la kazi na ''kumzuia kutimiza wajibu wake'' kwa style ile ni kosa la jinai🙂
Gender haikuwa respected. Kama wakili na mama msomi anadhihakiwa mbele ya kamera kiasi kile, watu wa kawaida itakuwaje sasa
 
Rais wa chama cha wanasheria nchini na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ataongoza jopo la mawakili 29 watakaomtetea Wakili Fatma Karume Katika Kesi Yake Ya Kushikwa Mwili Wake Bila Ya Ridhaa, Kuvutwa Kwa Nguvu Na Kusababishiwa Madhara Katika Bega Lake.
Katika Kesi Hiyo Iliyofunguliwa Mahakama Kuu Ya Tanzania, Bi.Fatma Anamdai Fidia Ya Shilingi Bilioni Moja, Inspekta Eugen Mwampondela Wa Kituo Kikuu Cha Polisi DSM.
Kesi Itakapoanza Kusikilizwa, Mtuhumiwa Atatakiwa Kuwepo Kizambani Kujieleza Na Kujibu Maswali.
Hehe mawakili 29 ndio nasikia leo kuwa kwenye kesi moja tena ya kesi ya kizushi,tii amri ya polisi usibughuziwe ,sasa atageuziwa kibao kwa kuzuia askari asifanye kazi yake
 
Hawa ndio wanasheria wa kitanzania hopeless kabisa, Kupoteza muda bure wa kufanya mambo ya maana
Kesi si ndiyo kazi yao. Sasa kwa kufanya kesi wanapotezaje muda bure? Au hujui kwamba kuna msemo wa Kiingereza usemao "Help your Lawyer, sue somebody"?
 
Hapakuwa na sababu polisi kuhamaki na kumshika mtu ambaye hafanyi kosa kisheria.Pamoja na kuwa hawezi kulipa ,ila kuna funzo tutapata.Kila la kheri Fatma
Maagizo toka juu shida sana wanajikuta hawana namna kutetea serikali ya makinikia
 
Kwa hali hii inaonyesha vijana wa kitanzania na wasomi mmekosa vya kufanya kesi kama hiyo mawakili 29 na inaonyesha ni jinsi gani kuwa mawakili hawajiamini na usomi wao. Wasilete kisingizio cha mshikamano bali ni kutokujiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanamke, anapaswa kuguswa na askari mwanamke, ikiwa ni pamoja na kukaguliwa mwilini, sio polisi mwanaume. Hiyo ni sawa na kumchungulia bafuni. Amwombe tu msamaha nje ya Mahakama yule mama atamsamehe ni muungwana sana Mama yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi mbaya kwa wanaopenda kushikashoka maungo ya watu aka dungadunga au polisi ccm wanapenda udhalilishaji wa kijinsia unashika mwanamke utafikiri maimuna wa kimboka lazima ukutane na gharika
Afande tumbo joto
 
Back
Top Bottom