VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Habari zimenifikia. Kweli jasiri haachi asili. Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu amejipanga na kupangika kufungua kesi ya madai dhidi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu maslahi yake ya kibunge akiwa mgonjwa.
Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya kutibu majeraha ya karaha ya risasi alizoshambuliwa nyumbani kwake Dodoma, tayari ameshakusanya nyaraka mbalimbali zinazoonesha kuwa anatengwa na maslahi hayo ya kibunge huku wengine wakiyapata bila tabu wala aibu.
Taarifa nilizonazo ni kuwa Lissu tayari ameshaanza kuandaa nyaraka za kimahakama za kudai maslahi yake hayo mara tu atakaporejea nchini siku za karibuni. Lissu ameapa kujiwakilisha na kujieleza (kwa maana ya kuendesha kesi yake) mwenyewe ili auanike ukweli kwa umma.
Nabii Tito!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam