Tetesi: Lissu kutua nchini na kesi nzito dhidi ya Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Hahahaa Mzee mwenzangu habari za siku nyingi? Nimefurahi sana kukutana na Lisu juzi yumzima wa afya, watesi wake wako roho juu juu sana
 
Chondechonde Chadema Tafadhali sana,Huyu Mwamba akirudi apewe Ulinzi wa Kutosha.Awe na Ulinzi 24/7 ili awe na Amani na kumkinga na Watesi wake ambao pengine hawajafurahishwa na Kutotimiza Kusudio lao
 
CCM hiyo unayoizungumzia ni ipi?
Hao mazwazwa ya lumumba?
Mkuu kama ni hao bado safari ni ndefu....

Hahhahahahahah,kawaida ulipoingilia mwiba ndipo utakapotokea the same to 'Funza' alipoingilia ndipo atakapotokea
 
Wakati bunge lingelipa dola 20000 (mfano) sasa wakiambiwa na korti walipe dola 100000 itakuwa wamefanya nini sasa? Wamemneemesha Lisu. Wataonekana ni matope tu!
ha ha, mahakama ikiamuru mtu alipwe analipwa hapo hapo!!'unachekesha sana

kuhidhinisha malipo ikulu inahusika,na serikali inaweza ikasema haina hela!!
 
Hata akishinda kesi hawatamlipa; tumshukuru tu Mungu wetu wa rehema kwa kumwinua tena mja wake. Mungu anatupenda, Mungu anampenda Lisu. Hana sababu ya kulipwa labda tu apende kufanya kesi ili kudhihirishia umma uwezo wake.

huu ndo ukweli
 
Habari zimenifikia. Kweli jasiri haachi asili. Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu amejipanga na kupangika kufungua kesi ya madai dhidi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu maslahi yake ya kibunge akiwa mgonjwa.

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya kutibu majeraha ya karaha ya risasi alizoshambuliwa nyumbani kwake Dodoma, tayari ameshakusanya nyaraka mbalimbali zinazoonesha kuwa anatengwa na maslahi hayo ya kibunge huku wengine wakiyapata bila tabu wala aibu.

Taarifa nilizonazo ni kuwa Lissu tayari ameshaanza kuandaa nyaraka za kimahakama za kudai maslahi yake hayo mara tu atakaporejea nchini siku za karibuni. Lissu ameapa kujiwakilisha na kujieleza (kwa maana ya kuendesha kesi yake) mwenyewe ili auanike ukweli kwa umma.

Nabii Tito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Acha kupiga porojo wewe utakuwa umetumwa na Lumumba kueneza propaganda humu
 
Nabii Tito - Jina limenichekesha sana
 
Rais ccm anavunjisha Amani ya watanzania tumkemee kwa nguvu zote.

Swissme
Kwa kuwa na Kanisa Katoliki limeingilia kati na uhakika atajirekebisha penda asipende...,

Maana Kanisa Katoliki sio mchezo watabadilisha hali ya nchi mara moja.
 
Inayoongoza Serikali Ni CCM na si Kanisa Katoliki. Penye Maslahi imani ya Kidini inaekwa Pembeni Kabisa.
 
Hata akishinda kesi hawatamlipa; tumshukuru tu Mungu wetu wa rehema kwa kumwinua tena mja wake. Mungu anatupenda, Mungu anampenda Lisu. Hana sababu ya kulipwa labda tu apende kufanya kesi ili kudhihirishia umma uwezo wake.
Nani kakudanganya..??
Unaijua sheria vizuri wewe...???

Mahakama ikiamuru kulipwa atalipwa mara moja na sio gharama za matibabu tuu..,hata gharama za kuendesha hiyo kesi pia zitalipwa.
 
Mwenye jukumu la kumtibu ni NHIF, serikali ilishamlipia bima, awashitaki NHIF.
Yani hii bima ambayo ukivuka Tanganyika haifanyi kazi, yani hata ukienda hapo Zanzibar inakuwa mfu ndio ikamtibie belgiji
 
Habari zimenifikia. Kweli jasiri haachi asili. Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu amejipanga na kupangika kufungua kesi ya madai dhidi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu maslahi yake ya kibunge akiwa mgonjwa.

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya kutibu majeraha ya karaha ya risasi alizoshambuliwa nyumbani kwake Dodoma, tayari ameshakusanya nyaraka mbalimbali zinazoonesha kuwa anatengwa na maslahi hayo ya kibunge huku wengine wakiyapata bila tabu wala aibu.

Taarifa nilizonazo ni kuwa Lissu tayari ameshaanza kuandaa nyaraka za kimahakama za kudai maslahi yake hayo mara tu atakaporejea nchini siku za karibuni. Lissu ameapa kujiwakilisha na kujieleza (kwa maana ya kuendesha kesi yake) mwenyewe ili auanike ukweli kwa umma.

Nabii Tito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kuna jambo silielewi kuhusu kulipiwa matibabu kamanda Lissu.
Hivi mbunge akiumwa anajipeleka tu kienyeji hospitali yeyote duniani na kuliagiza bunge limlipie?
Nauliza hivi kwa sababu kote huko alikoenda kajiamulia mwenyewe na Mbowe.
 
Nadhani cha msingi Kwanza ingekuwa kumuombea afike / awasili salama nchini na hayo mengine ndiyo yatafuata kwani ya Mungu mengi na Shetani nae ana mipango yake vile vile chini ya jua hili.
 
Back
Top Bottom