Tetesi: Lissu kutua nchini na kesi nzito dhidi ya Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Tetesi: Lissu kutua nchini na kesi nzito dhidi ya Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Kuna jambo silielewi kuhusu kulipiwa matibabu kamanda Lissu.
Hivi mbunge akiumwa anajipeleka tu kienyeji hospitali yeyote duniani na kuliagiza bunge limlipie?
Nauliza hivi kwa sababu kote huko alikoenda kajiamulia mwenyewe na Mbowe.

..kuna mambo nadhani manne ambayo bunge lilipaswa kumhudumia.

1. Usafiri kwenda na kurudi ktk matibabu.

2.gharama za matibabu.

3.posho ya mbunge aliyeko kwenye matibabu.

4.posho ya msaidizi anayemuuguza.

..kwa maoni yangu, serekali inaweza kumshinda ktk hoja namba 1 na 2, lakini sioni jinsi gani watamshinda ktk hoja ya 3 na 4.

..lakini ukumbuke kwamba hukumu yoyote inaathiri maamuzi yanayofuatia. Kwa hiyo wakikataa kugharimia matibabu ya TL Nairobi Bunge litakuwa limejifunga mikono kumhudumia mbunge mwingine nje ya Muhimbili na India.
 
tunaomba asilimia 10 ya ruzuku ya chama awekewe ulinzi kamanda Tundu Lissu ili aendelee kuinyoosha serikali ya bwana maguvu pasipo akili.
Mkuu usiwe na hofu na ulinzi wa Lisu. Huyu mtu Mungu amejiridhihisha naye kulinda. Sema Mungu huwaadhibu wabaya wa watu wake kwa wakati wake. Si ajabu ameandaa kama siyo kutekeleza adhabu ya wapuuzi hawa.
 
Habari zimenifikia. Kweli jasiri haachi asili. Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu amejipanga na kupangika kufungua kesi ya madai dhidi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu maslahi yake ya kibunge akiwa mgonjwa.

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya kutibu majeraha ya karaha ya risasi alizoshambuliwa nyumbani kwake Dodoma, tayari ameshakusanya nyaraka mbalimbali zinazoonesha kuwa anatengwa na maslahi hayo ya kibunge huku wengine wakiyapata bila tabu wala aibu.

Taarifa nilizonazo ni kuwa Lissu tayari ameshaanza kuandaa nyaraka za kimahakama za kudai maslahi yake hayo mara tu atakaporejea nchini siku za karibuni. Lissu ameapa kujiwakilisha na kujieleza (kwa maana ya kuendesha kesi yake) mwenyewe ili auanike ukweli kwa umma.

Nabii Tito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Binafsi ningemshauri aache huwo ujinga asione watu kimya akafikiri wanamuogopa. Akae kimya anajuwa dhambi yake asisumbuwe watu.
 
Itakua vizuri sana wale wale waliokataa asitibiwe na serikali kwa madai watamuua ndio wamlipe
 
Binafsi ningemshauri aache huwo ujinga asione watu kimya akafikiri wanamuogopa. Akae kimya anajuwa dhambi yake asisumbuwe watu.
Pole mkuu wakati mwingine kukiri kumshindwa Lisuni ujasiri. Hamumuwezi na kama mna mipango mingine mtapambana na nguvu ya Mungu yule yule aliyemuokoa mwanzo. Hamko kimya, sema hamna jinsi.
 
ha ha, mahakama ikiamuru mtu alipwe analipwa hapo hapo!!'unachekesha sana

kuhidhinisha malipo ikulu inahusika,na serikali inaweza ikasema haina hela!!

..hili suala linaweza lisifike mahakamani.

..linaweza kujadiliwa na kuamuliwa na wabunge wenyewe ktk kamati yao ya huduma na utawala.

..na huko wabunge wengi wanaweza kuwa sympathetic na situation ya mbunge mwenzao, na pia hawatapenda kutoa uamuzi ambao utawakwamisha ktk matibabu yao huko mbeleni.

..Mahakama ni hatua ya mbali na ya mwisho. Suala la Mh.Lissu ni la BUNGENI zaidi.
 
Pre emptive? Labda bunge la mbinguni?
 
Pre emptive? Labda bunge la mbinguni?

..mara zote TL amekuwa akilitaja BUNGE.

..kwa maana hiyo uwezekano mkubwa atadai haki zake kupitia taratibu za KIBUNGE.

..Ikiwa atashindwa bungeni basi ndiyo atatoka na kwenda MAHAKAMANI.

..Na mimi sioni ni jinsi gani atashindwa humo bungeni, kwasababu suala lake, na jinsi litakavyoamuliwa, litaathiri upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wabunge wote.
 
Hata akishinda kesi hawatamlipa; tumshukuru tu Mungu wetu wa rehema kwa kumwinua tena mja wake. Mungu anatupenda, Mungu anampenda Lisu. Hana sababu ya kulipwa labda tu apende kufanya kesi ili kudhihirishia umma uwezo wake.
Hapana. Hakuna mwenye ubavu wa kukwamisha maamuzi ya mahakama
 
Habari zimenifikia. Kweli jasiri haachi asili. Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu amejipanga na kupangika kufungua kesi ya madai dhidi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu maslahi yake ya kibunge akiwa mgonjwa.

Nabii Tito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Lipi zito kwa Lissu kuwafikisha mahakamani waliomshambulia kwa risasi kwa nia ya kumtoa uhai, na anawafahamu, au kunyimwa gharama za matibabu?

Kama mwanasheria na Mbunge, anajua fika taratibu za matibabu kwa wabunge, je, hilo linastahili kufikishwa mahakamani, au kupeleka hao madai ofisi za Bunge?

Yangu masikio!!!
 
Kuna kitu hapa kikizungumzwa wote mtakaa kimya coz either mnajitoa ufahamu na kujitia uchizi msiokuwa nao au hamjui hivyo mnajikuta mnaandika kishabiki zaidi.
Si vizuri kufurahia madhira ya mwenzio lakini sio vizuri vilevile kutumia madhira hayohayo kuwatia wengine ubaya.
Utaratibu mzima wa kumsafirisha TL kwenda Nairobi ulikiukwa na haukufuata sheria. Ulikuwa wakisiasa kwa dhana kwamba akienda M'mbili wabaya wake watammalizia. Rufaa iliyotakiwa ilibidi wampeleke muhimbili, kwa ubishi wa mbowe wakampeleka nairobi tofauti na utaratibu wa bunge kwamba muhimbili wakishindwa ndio bunge linagharamikia matibabu nje ya nchi.
So msifikiri bunge na serikali wamekaa kimya kwa stori zenu za mtaani mkajua hawana majibu au hawajui wanachokifanya.
Km mnakumbuka jpm alimwambia shein kwanini anamsainia maalim seif check zake za matibabu wakati hata salama hataki kupokea.
Sasa huku jeuri kakutana na kiburi/ makusudi .
Aende tu mahakamani ili vituko viendelee tuchangamke kidogo tupate cha kujadili.
 
Habari zimenifikia. Kweli jasiri haachi asili. Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu amejipanga na kupangika kufungua kesi ya madai dhidi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu maslahi yake ya kibunge akiwa mgonjwa.

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya kutibu majeraha ya karaha ya risasi alizoshambuliwa nyumbani kwake Dodoma, tayari ameshakusanya nyaraka mbalimbali zinazoonesha kuwa anatengwa na maslahi hayo ya kibunge huku wengine wakiyapata bila tabu wala aibu.

Taarifa nilizonazo ni kuwa Lissu tayari ameshaanza kuandaa nyaraka za kimahakama za kudai maslahi yake hayo mara tu atakaporejea nchini siku za karibuni. Lissu ameapa kujiwakilisha na kujieleza (kwa maana ya kuendesha kesi yake) mwenyewe ili auanike ukweli kwa umma.

Nabii Tito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
vipi kuhusu hali ya usalama wake atakaporejea nchini ?
 
Hata akishinda kesi hawatamlipa; tumshukuru tu Mungu wetu wa rehema kwa kumwinua tena mja wake. Mungu anatupenda, Mungu anampenda Lisu. Hana sababu ya kulipwa labda tu apende kufanya kesi ili kudhihirishia umma uwezo wake.

Keasi hazifunguliwi kwa sababu una uwezo wa kukataa kulipa. Kesi zinafunguliwa ili kuweka history, precedence.
 
..mara zote TL amekuwa akilitaja BUNGE.

..kwa maana hiyo uwezekano mkubwa atadai haki zake kupitia taratibu za KIBUNGE.

..Ikiwa atashindwa bungeni basi ndiyo atatoka na kwenda MAHAKAMANI.

..Na mimi sioni ni jinsi gani atashindwa humo bungeni, kwasababu suala lake, na jinsi litakavyoamuliwa, litaathiri upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wabunge wote.
Haupo serious. Bunge liko chini ya ikulu ya Magufull ndiyo maana hata hizo hela hazitolewi. Kesi kupelekwa mahakama ina muhimu wa kutumia utaratibu wa umma nje ya utaratibu wa bunge ambao umeshindikana.
 
Back
Top Bottom