Uchaguzi 2020 Lissu kuzungumzia tozo kwa wajawazito Sumbawanga, ni kweli zipo ndugu zangu CCM au anadanganya?

Uchaguzi 2020 Lissu kuzungumzia tozo kwa wajawazito Sumbawanga, ni kweli zipo ndugu zangu CCM au anadanganya?

å Sijajua kwanini baadhi ya watu wanabisha kuwa huduma ya matibabu katika hospitali za umma ni za BURE na kamwe siyo ZA KULIPIA....

å Sijajua ni kwanini baadhi ya watu wasio na facts wanabisha kuwa elimu ya Msingi na Sekondari Tanzania siyo BURE bali bado wazazi WALIPIA....!

å Tuite jina lolote lile aidha TOZO au KUCHANGIA GHARAMA nk nk lakini ukweli unabaki kuwa, HAKUNA HUDUMA ya ELIMU wala AFYA inayotolewa bure hapa Tanzania....

å Mtu yeyote anayebishia, aende katika hospitali yoyote ya umma akajionee. Tozo ama gharama unaanza kupambana nazo immediately ufikapo mapokezi...

å Kuna hospitali au vituo vya afya ama zahanati kabla ya kuruhusiwa kumwona daktari, lazima ulipe kati ya Tshs. 5,000 na 10,000.... Hii ni nini kama siyo tozo za matibabu?

Hapo bado hujakutana na gharama za dawa na vipimo mbalimbali....

Ni mateso, mateso, mateso tupu kwa wananchi....!!

Tuwe honest, hakuna cha bure tusidanganyane...
 
Mwaka jana mi nimekwenda Muhimbili mke alikua na changamoto kwenye uzazi wamemfanyia operesheni pale mtoto alikua ashafia tumboni, baada ya siku tatu napewa bill ya 2mil nikasema kama hapa ni National Hospital na mtu hana uwezo itakuaje. Ilibidi niparue akiba yangu niwalipe. Wanakwambia usipolipa leo kesho bill ya kulala inaongezeka.

Kitu kilinitatiza dressing ya kidonda walipompasua kwa siku niliona wameandika 50,000 nikasema yani eusol na Spirit na pamba na gloves wanatumia nyingi kiasi gani.

By the way serikali inatakiwa iangalie upya gharama za matibabu sio rafiki kivile kwa mtu asiye na bima.
.pole sana kiongozi
 
å Sijajua kwanini baadhi ya watu wanabisha kuwa huduma ya matibabu katika hospitali za umma ni za BURE na kamwe siyo ZA KULIPIA....

å Sijajua ni kwanini baadhi ya watu wasio na facts wanabisha kuwa elimu ya Msingi na Sekondari Tanzania siyo BURE bali bado wazazi WALIPIA....!

å Tuite jina lolote lile aidha TOZO au KUCHANGIA GHARAMA nk nk lakini ukweli unabaki kuwa, HAKUNA HUDUMA ya ELIMU wala AFYA inayotolewa bure hapa Tanzania....

å Mtu yeyote anayebishia, aende katika hospitali yoyote ya umma akajionee. Tozo ama gharama unaanza kupambana nazo immediately ufikapo mapokezi...

å Kuna hospitali au vituo vya afya ama zahanati kabla ya kuruhusiwa kumwona daktari, lazima ulipe kati ya Tshs. 5,000 na 10,000.... Hii ni nini kama siyo tozo za matibabu?

Tuwe honest, hakuna cha bure tusidanganyane...
TUSILALAMIKE TUNAPOLIPIA SASA
 
wapinzani karibu mtataka na kuoa iwe bureee an bila mahari
 
Lissu hana cha kuahidi, Magu kashafanya vyote! Ana bwabwaja tu hana sela
Watakae mpa huyu jamaa kura,watakuwa hawako Sawa kichwani.Kwa Sera gani alizonazo, maana kila mkutano ni kulalamika tu. Hatutaki taifa tegemezi, omba omba na lalamishi hapa. Tunataka taifa lenye kujitegemea kwa kupiga kazi tu.
 
Lissu akiwa Sumbawanga kadai kuwa wakina mama wajawazito wanatozwa tozo mahospitalini pindi wanapojifungua.

Kuwa mama akijifungua mtoto wakiume anatozwa tozo kubwa kuliko aliejifungua mtoto wa kike. Je, nikweli juu yahaya ndugu zangu CCM, au Lissu anadanganya?

Je, kama nikweli, kwanini tozo zitofautiane juu ya mtoto wakiume na kike? Je, hii ipo kisheria? Au Kuna baadhi ya hospital zinamuhujumu raisi wetu mpendwa JPM?

Kama muheshimiwa raisi anatoa elimu bure, kwa nini asiruhusu wajawazito waachwe kutozwa tozo mara wanapojifungua? Maana anahimiza tufyatue watoto kwa wingi zaidi.

Nataka nifahamu ukweki juu yahili, kama nikweli Serikali imeweka tozo mpaka kwa wajawazito, na kama tozo hizo zinatozwa tofauti kwa mtoto wakike na kiume, kama kuna ukweli wowote.

Bima ya afya kwa kila mwananchi za bei nafuu ndio suluhisho, itaondoa ukilitimba wote wa tozo za hospitalini.
Kaanza lini kuhurumia wakina mama?. Saccos yao inaongoza kwa kuwazalilisha wamama zetu, ndio wapate nafasi kwenye uongozi chama.Mpaka mfichwe chini ya sketi ndio viti maalum vitoke shame on you. Watanzania, Oct tusifanye makosa.
 
Watakae mpa huyu jamaa kura,watakuwa hawako Sawa kichwani.Kwa Sera gani alizonazo, maana kila mkutano ni kulalamika tu. Hatutaki taifa tegemezi, omba omba na lalamishi hapa. Tunataka taifa lenye kujitegemea kwa kupiga kazi tu.
Mkuu mbona mwingine analalamika anatukanwa huku hatuoni matusi.
 
Tozo hizo kama zipo ni zile zisizo rasmi, huwezi kupewa EFD kwa tozo hizo. Suluhuhisho siyo kukanusha kuwa hazipo, bali kufuatilia na kuwachukulia hatua wahusika, maana Lisu amesikia kutoka kwa akina mama.
 
TOZO zipo kila mwana ccm anafahamu hilo.
 
Serikali iweke wazi hizo tozo Sasa. Na wasimame waseme kwa nguvu ileile wanayotumia kudanganywa kuwa kuna elimu bure, wasimame waseme pia kuna tozo za ujauzito.
haitakua siasa kuzungumzia hayo
 
Kuondoa tozo za hospitalini, kuondoa tozo za elfu ishirini kwa machinga, namama zetu wauza genge.

Kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili, hata waliosoma privete . Kushusha makato ya heslb mpaka 3%, kuruhusu wananchi wauze mazao yao seheme yenye bei nzuri, kurudisha fao lakujitoa, kuwalipa stahiki zao wastaafu kwa wakati kama wafanyavyo wabunge kulipwa kwa muda mara baada ya miak mitano.

Hizo nibaadhi ya sera za CDM. Lkn hapa simahala pake,hapa tunajadili tozo zahospitalini,wanazotozwa wajawazito kabla ama baada yakujifungia.
Zipo kwenye ilani au mnaokoteza tu??
 
Back
Top Bottom