Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Kwenye mahojiano na BBC namsikia Lissu anasema kuwa Mbowe aliyeenda jela sie yule aliyetoka. N watu wawili tofauti. Kwamba baada ya Mbowe kupewa alivyopewa amekuwa mkimya, mpole, Mdiplomasia, n.k. Kwamba wale wananchi waliokuwa tayari kuwafia, kuwafuata, kuwasikiliza na kukifuata chama, leo hii hawafanyi tena yale. Mbowe akiitisha maandamamo wananchi hawatikii...
Hivi kweli Lissu ni wa kusema hayo?
Hivi kweli Lissu haoni aina ya siasa inayofanyika nchini?
Hivi kweli haoni utekaji unaoendelea?
Hivi kweli haoni Mauaji yanayofanyika kwa mgongo wa wasiojulikana?
Hivi kweli haoni vijana wa CDM waliopotea hadi leo hawajapatikana?
Hivi kweli haoni vile Dola inavyotisha wananchi?
Ongezeni yenu.
Halafu Leo Lissu anakuja kusema Mbowe ni sababu ya wafuasi kupoa na kukipa chama mgongo. Inawezekana kweli Mbowe ni sababu katika mtizamo chanya. kwamba kwa sababu ya siasa zake, amesababisha serikali na chama tawala kuwa walivyo leo. Wameshindwa kuhimili upinzani na hoja za chadema. Wameshindwa kuhimili upinzani chini ya Mbowe na ndio maana leo tunaona Dola inaingia na miguu yote kunyamazisha upinzani.
Hivi kweli naona mobilizaton ya vikosi vya polisi nchi nzima na kauli za kibabe na za vitisho toka kwa wakuu wa polisi, bado niingie mtaani kuandamana? Aisee...