Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Wakati tunajadili na kuchukua maoni ya wadau hakuwepo leo hii anatujia na porojo!!

HII NI HABARI NJEMA KWA WAZUNGUSHA MIKONO...LISSU KESHAJUA VILAZA WANARAKA NINI...NA ATAWAPA NA KUENDELEA KUWAPA HIKO MNACHOKITAKA. ..

Namkubali Rugemeleza
We mchovu kweli! TAL alishatoa maoni yake na amekuwa akitoa maoni kwa miongo kadhaa. Unataka akatoe maoni gani tena? Amka kumekucha na punde makinikia yatakuwa yakielekea kuchenjuliwa huko igaibuni na hutakaa upate hiyo noah!
 
Nimeshajua Kwanini Wanasheria Wengi Wa Serikali Wanapata Knock-out Nyingi Kwenye Kesi
Kila Kukicha. Hawana Facts Pia Wavivu Wa Kufanya Research
Viva Tundu Antiphas Mughwai Lissu
 
True. Mabogus sana hao jamaa. Instead ya kusimamia ukweli anakwambia nina familia na watoto wananitegemea. Wanaendeleza ule mfumo wa kufikiria matumbo yao tu badala ya maslahi mapana ya taifa.
 
Tundu Lissu amajaliwa kusoma na kuelewa undani wa jambo bila chenga.
Ilitakiwa Raisi Magufuri apate ushauri wake,kwani Lissu hana chembe ya unafiki.
Anajua kueleza jambo gumu kwa umati wakamuelewa kwa urahisi zaidi.
Tundu Lissu is genius.
 
Tundu Lissu kuonyesha yuko vizuri angewapa ushauri wa bure na technicalities ya vipi tutanasuka katika hili
Mkuu Lissu hajaacha kitu,alishasema sema haya ya makinikia tuachane nayo kwanza tuanze na mikataba yenyewe inayotupa mrahaba wa 4% tujitoe kwenye mahakama ya biashara ya kimataifa na ya hapa nchini,tukifanya hivyo ndipo tuwaite tuwaambie hatutaki 4% tunataka mfano 45% watang'aka na kukimbilia mahakamani huko nje watakuta kote tulishajitoa uchaguzi unabaki kwao waendelee au waondoke.
 
Nilitegemea Tundu Lisu kama Rais wa chama cha wanasheria angeongea tofauti na alivyofanya, amejikita ku-criticize kama kawaida yake. Waziri wa sharia alisema kuwa sharia mpya huanza kuwa applied pale inapotungwa na kupishwa (haiendi nyuma), na kuwa kwa mikataba ya madini iliyokwishaingiwa kabla ya sharia hii (miswada ya madini iliyo ktk mjadala) basi itabidi waongee na hao wawekezaji ili kukubaliana na baadhi ya mambo.

Kwa hiyo Rais wa wanasheria baada ya kuisoma hiyo miswada na kuzingatia kauli ya waziri wengi tulitegemea angekuja na hoja za kisheria (kutokana na weredi wa members wa hicho chama) ambazo zingeonyesha au kuhalalisha sharia mpya kutumika hata kwa mikataba ya huko nyuma. Kwa ufupi angeshauri ni nini cha kufanya ili maoni hayo yahusishwe ndani ya sharia kabla haijapitishwa.

Badala yake amekuja kuongea kama watu wengine wa kawaida tu. Hapo ndo huwa nashindwa kumwelewa kabisa Lisu; anapenda kuonyesha makosa na umbumbu wa wengine akijichukulia kama ndo mwanasheria mahiri pekee hapa nchini.
Hutakaa umwelewe.
 
Lissu sio muongo unavyotaka aonekane, ametoa maangalizo ya msingi sana.

Hizo MDA kati ya Serikali na Buliyanhulu na Pangea Ltd umeshaziona ujue walikubalina "Rules of the game" ziwe zipi na marefa wawe akina nani? Kama wawekezaji wakigoma kukaa mezani serikali ikiwafukuza, si itabidi ilipe fidia mabilioni na mabilioni? Ndio baadhi ya anayosema Lissu.
Hujui kitu kaa kimya!
 
Andiko hilo na hoja ya Lissu ni kuona nchi inashindwa ili Lissu apate sifa. Aliyofanya Magufuli na heshima aliyoipata hakuna wa kuichukua. Ninachoona hapa ni kujitambulisha kwa msimamo wa viongozi wa CHADEMA. Wale walioko kwenye migodi na wanaooumia ndio watakaowahukumu vyema 2020 mtaona kama mtapata Jimbo lolote eneo hilo. Tena ni bora asiwe Lissu maana atashindwa vibaya sana.
Hivi kuandika kwa niaba ya CHADEMA au yeye?
 
Mikataba mingapi hapa Tz inasimamiwa na MIGA?au ni acacia tu?kamà iko mingi huoni kuwa ni ujuha kujitoa MIGA kwa ajil ya kampuni moja tu?Wamesema pande mbili zitakaa wafikie muafaka lkn ww bado unakariri MIGA tu.Hii ni vita unapambana na mabepari wa dunia sio mashamba ya mbowe. Mimi nafikiri jpm na kamati yake wanaona mbali mno kuliko mnavodhani.na msijidanganye kwamba hiyo MIGA serikal haiijui zaid ya lisu tu.
Lisu is just one person na ana mawazo yake binafsi na msimamo wake. Kama sisi wengi hatukubaliani naye si tuendelee tu na mipangilio yetu na matakwa ya rais wetu mpendwa mzalendo .Hivi chukua mfano mdogo umepata kiwanja Ruvu unataka kujenga na hela ni zako,mke au rafiki yako akabeza kwamba unajenga shamba huko.Hivi utastop kujenga halafu kila jioni ukirudi utakuwa unagombana na mkeo kwa nini hakubaliani nawe.Kama mwanaume unajenga tu faida atakuja kuona baadaye. Unless kama una shaka na maamuzi yako.Personally naamini kuwa kwenye wengi lazima mawazo yatofautiane ili isaidie watu kufikiri zaidi kuhusu maamuzi yao.Vinginevyo kama kila wakati wote mtakuwa na fikra zinazofanana then probably you are all dead.Mind you development is a results of contradiction/conflicting ideas.
 
Nimesha changanyikiwa toka siku ile waziri prof. Kabudi aliposema marekebisho haya ya sheria ni kwa watakaokuja kuwekeza...
Tena akasema Sheria huwa hairudi nyuma huwa inaenda mbele hivyo makampuni yaliopo tayari yanaendelea na kazi haita yahusu.

Mwenzenu niko full confused
 
Sitaki kusikia tena habari hii ya madini wala makinikia ntakufa kabla ya wakati wangu kwa presha bure.

Bora kusoma gazeti la shi go go tu japo naye snitch
 
Back
Top Bottom