Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amesema kuna mbinu za kuweka mawakala mwaka huu zimekuwa tofauti uklinganisha na miaka iliyotangulia.
Amesema miaka yote wakala anapewa barua ya utambulisho anaenda nayo kituo cha kupigia kura. Kwenye uchaguzi huu Tume ya Uchaguzi ndio inapanga sehemu ambayo wakala atakwenda.
Amesema hali hiyo inaweza leta shida kwa kuwa wakala atapaswa kutafuta kituo chenye jina lake na hivyo kunaweza kutokea uchelewaji wa mawakala kufika vituoni kwa muda watakaotumia kutafuta.
Kutokana na hilo amewaambia wafuasi wake kuwa wahakikishe kura hazipigwi hadi mawakala watakapokuwepo katika vituo vya kupiga kura ili kudhibiti kura zao.