Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Kimeumana CHADEMA, Tundu Lissu amvaa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe baada ya kurejea Tanzania kutoka nchini Ubeligiji.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuulizwa kuhusu alichokisema Mbowe kuwa walishauriana asigombee Uenyekiti CHADEMA, pengine baadae angegombea Urais

Soma, Pia: Mbowe: Ilikuwa ghafla sana Lissu kutangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa

"Kwanza hili niliseme kwa masikitiko, kwasababu si jambo nzuri kusema Mwenyekiti (Freeman Mbowe) amesema uongo, kwenye hili amesema uongo. Tulikutana kwa siku tatu hapa Msimbazi, Kanisani tukipatanishwa, tukizungumza juu ya hiki kinyang’anyiro na kwa siku tatu zote Mwenyekiti alisema yeye hajaamua kugombea nafasi yoyote [kwa siku tatu], Katibu Mkuu John Mnyika ni shahidi…."
 
Wakuu

Kimeumana CHADEMA, Tundu Lissu amvaa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe baada ya kurejea Tanzania kutoka nchini Ubeligiji "Ni Muongo mimi sikutaka kugombea Urais narudia Mbowe ni Muongo"
View attachment 3194110
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu ametangaza nia kuwania nafasi ya urais mwakani na kwamba chama chake kinajiandaa kupata ushindi wa kutosha dhidi ya Rais Samia Suluhu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye anatarajiwa kugombea kupitia chama hicho.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo baada ya kurejea kutoka nje ya nchi alipokuwa kwa mapumziko mafupi baada ya ziara ya chama chake Kanda ya Kaskazini aliyoifanya sambamba na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Lissu alisema kwa sasa chama chake kinaandaa wagombea katika nafasi mbalimbali kwa ajili ya kushinda uchaguzi ujao.

“Nia yangu ya kugombea mwaka 2025 iko palepale nitaitikia wito Watanzania na nitaitikia wito wa chama changu” amesema Lissu.

Alipoulizwa kuhusu kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama chake amesema hana mpango huo na kukanusha uvumi wakuwepo mgogoro kati yake na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kuhusu kuwania nafasi hiyo.

“Nimesema mara mia kwamba sigombei uenyekiti wa chama sasa huo mvutano unatoka wapi ni wa kutengenezwa tu na vyombo vya habari” amesema Lissu.

Source: nipashe Jue 2024
 
Wakuu

Kimeumana CHADEMA, Tundu Lissu amvaa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe baada ya kurejea Tanzania kutoka nchini Ubeligiji.

"Kwanza hili niliseme kwa masikitiko, kwasababu si jambo nzuri kusema Mwenyekiti (Freeman Mbowe) amesema uongo, kwenye hili amesema uongo. Tulikutana kwa siku tatu hapa Msimbazi, Kanisani tukipatanishwa, tukizungumza juu ya hiki kinyang’anyiro na kwa siku tatu zote Mwenyekiti alisema yeye hajaamua kugombea nafasi yoyote [kwa siku tatu], Katibu Mkuu John Mnyika ni shahidi."
View attachment 3194110
Shikamoo TAL 🤣🤣🤣
 
Tatizo la He Say / She Say...; ni ngumu kwa third Party kujua nini ndio nini ?

Pia Haya mambo ya wadau kukutana na kugawana nani agombee nini na nani afanye nini na kwa wakati gani na yenyewe sidhani kama ni vema sana...

Hadi naona shida nianzie wapi kukuelemisha, tafuta taarifa kwanini Lissu aliamua kubadili mawazo na kugombea nafasi ya Uwenyekiti.

Mbowe alijipanga kumfanyia uhuni makamu wake. Alipanga kuanza na kumpoka nafasi ya umakamu kisha kumnyima nafasi ya kugombea Urais.

Lissu akashtuka mapema naye akabadili mawazo, ndio hii imekuwa vita sasa.
Nani ataamini?
 
Wakuu

Kimeumana CHADEMA, Tundu Lissu amvaa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe baada ya kurejea Tanzania kutoka nchini Ubeligiji.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuulizwa kuhusu alichokisema Mbowe kuwa walishauriana asigombee Uenyekiti CHADEMA, pengine baadae angegombea Urais

Soma, Pia: Mbowe: Ilikuwa ghafla sana Lissu kutangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa

"Kwanza hili niliseme kwa masikitiko, kwasababu si jambo nzuri kusema Mwenyekiti (Freeman Mbowe) amesema uongo, kwenye hili amesema uongo. Tulikutana kwa siku tatu hapa Msimbazi, Kanisani tukipatanishwa, tukizungumza juu ya hiki kinyang’anyiro na kwa siku tatu zote Mwenyekiti alisema yeye hajaamua kugombea nafasi yoyote [kwa siku tatu], Katibu Mkuu John Mnyika ni shahidi."
View attachment 3194110
Lissu anafahamu siri nyingi sana. Hizi anazotoa ni just piece of Iceberg
 
Back
Top Bottom