Pre GE2025 Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ivi Lissu si alisema atatimkia ccm kama chadema itaacha misingi yake? Nafikiri anashuhudia ccm ilivyo au tuseme huwa ni njaa tu kufuata vyeo ilhali wanajua yaliyoko ccm
Alikwambia wewe kuwa atatimkia CCM?
Alisema chadema si mama yake hivyo ccm inaweza kuwa ndio mama yake halisi, Msigwa anajua madhila ya ccm lakini katimkia huko huko sasa anavaa kijani na kumsifia mama tu muda wote, Tanganyika njaa ndio shida
 
Amiri jeshi mkuu mpaka sasa yupo kimya? Alafu unajipendekeza kudai eti ni msikivu.

Kwa huu unyama aliofanyiwa Lissu, Mnyika na Sugu kulikuwa na haja ya kujikomba na kujipendekeza?

Nia yako kubwa uitwe Ikulu ili ukalambe asali vizuri huku sisi makamanda tunaumia.

Nimesafiri kwa lori toka Mbeya mpaka huku nilipo. Lakini niliteseka sana. Alafu leo unajipendekeza?
 
Ulikua ukamataji wa kijinga sana na policcm ila yule mwanamke atafute jimbo la kugombea kama anataka kurudi bungeni kwa njia ya kura sio hapo tena. Si aliwatuma wale??
 
Ki ukweli, naumia sana kwa kitendo walichofanyiwa viongozi na wafuasi wa CHADEMA kule Mbeya.
Wale ni wafuasi wa CHADEMA lakini ni Watanzania na ni binadamu kama mtanzania na binadamu mwingine yeyote yule. Wamefanyiwa kitendo kisicho cha heshima kabisa. Wamedhalilishwa sana tena sana.
Hawakuwa na silaha yoyote ile, kwa hiyo kulikuwa na haja gani kuwatweza kiasi kile.
Mimi si mwanachama wala mkeleketwa wa CHADEMA lakini kitendo walichofanyiwa si cha kibinadamu hata kidogo.
Ili kuonesha uungwana, ni muhimu utoke hadharani na uwaombe radhi waliotendewa mambo maovu hayo.
Ndugu zangu wa CHADEMA, poleni sana, Mungu ni mkubwa, kwa hakika atawalipa. Duniani hakuna dhuluma isiyo na malipo kwa mtendwa na mtendaji. Mungu mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…