Lissu: Msigwa alienda kumsubiria Mwenyekiti Mahakama ya Kisutu alipoachiwa huru lakini hakumkuta, akashangaa kumuona kwenye TV yupo Ikulu

View attachment 3203344

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu anasema siku ambayo Freeman Mbowe anaachiwa huru Mchungaji Peter Msigwa alienda na wanachama wa CHADEMA kumsubiria katika Mahakama ya Kisutu lakini cha kushangaza hawakumuona na baadaye walishituka kumuona akiwa ikulu na Rais Samia. Tundu Lissu anasema baada ya Msigwa kuhoji imekuaje ameenda Ikulu bila kuwafahamisha viongozi wengine na nini walichozungumza Mbowe aliaanza kumuona Msigwa kama adui na kushughulika naye hali iliyompelekea kuondoka CHADEMA.

Amesema hayo alipokuwa anahojiwa na Clouds TV
wengi tulishasema siku nyingi sana kwamba adui wa mabadiliko katika hii nchi ni mbowe, hana hata aibu.
 
View attachment 3203344

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu anasema siku ambayo Freeman Mbowe anaachiwa huru Mchungaji Peter Msigwa alienda na wanachama wa CHADEMA kumsubiria katika Mahakama ya Kisutu lakini cha kushangaza hawakumuona na baadaye walishituka kumuona akiwa ikulu na Rais Samia. Tundu Lissu anasema baada ya Msigwa kuhoji imekuaje ameenda Ikulu bila kuwafahamisha viongozi wengine na nini walichozungumza Mbowe aliaanza kumuona Msigwa kama adui na kushughulika naye hali iliyompelekea kuondoka CHADEMA.

Amesema hayo alipokuwa anahojiwa na Clouds TV
Mbowe alikuwa anawakilisha chama hata kule gerezani sio yeye kama mtu binafsi.Hivyo alikuwa na wajibu kuitikia mwaliko wa Rais akiwa na viongozi wachache wa cdm.Mbona mahakamani walikuwa pamoja naye?Kama itifaki haikuruhusu basi Lisu ana mantiki ya kuwa na mashaka na mwaliko
 
Back
Top Bottom