Uchaguzi 2020 Lissu muulize mpinzani wako, ‘Jina lako ni nani?’

Uchaguzi 2020 Lissu muulize mpinzani wako, ‘Jina lako ni nani?’

Mmh! Kwamba Lissu ni tishio kwa Magufuli hata awe akimtaja kwa jina wakati wa Campaigns?

Sijui umri wako mleta mada; iwapo umefikisha 40s, basi, usiendelee kusumbua kichwa. Waliwahi pita akina Mrema, Lowasa. Hii ya huyu bwana mdogo Lissu mbona ni cha mtoto tu. Watanzania wana siasa wanazijua wenyewe. Watajaa kukusikiliza. Watasukuma hadi gari lako ati usimalize mafuta; kwenye kura sasa! Hapo ndiyo yanaanza, Nimeibiwa kura!

Lissu hawezi kumshinda Magufuli na kama bado huamini, subiri hiyo 28, Oktoba 2020.

Hujaeleweka (watajaa kukusikiliza lakini kwenye kura?) Unataka kutuaminisha iwapo mgombea akijaza watu ishara yake ni kukosa? Kwa hiyo rungwe kwa kuwa hajazi watu ndio atapata kura?
 
Magufuli hawezi taja jina la TL kwa sababu anaona Lissu ni mzimu. Risasi 16 lakini ndiyo hivyo bado Lissu anadunda. Sidhani kama anaweza onana na Lissu uso kwa uso bila ya kutetemeka. Ni kama wewe uonane uso kwa uso na mtu wako aliyefariki na kuzikwa zamani.
 
Jana tu nimeangalia hapa Shinyanga, mahudhurio ya wananchi yalikuwa zaidi ya yale ya Lowassa! Hivyo ni ushahidi tosha kabisa Lissu ameteka nyoyo za watu!
Hujui...... Unashangaa nini hata kama ni picha za 2015, lakini si Chadema hiyohiyo.......Sijui.....Kwani tukijifariji ni dhambi?
Screenshot_20200902-223701.png
 
Mara kadhaa nimelinganisha mtanange wa uchaguzi wa mwaka huu na pambano la ngumi kati ya Muhammad Ali na George Foreman.

Leo hii nitagusia jambo ambalo nadhani wengi mtakuwa mmeligundua. Nalo ni hii tabia ya mgombea wa Urais wa CCM, John Magufuli kukataa kata kata kutaja jina la mpinzani wake mkuu, Bw. Tundu Lissu. Sikumbuki kama nimewahi kumsikia Magufuli akitaja jina la Lissu hata siku moja.

Najua kwenye medani za saikolojia, kutotaja jina la adui yako inaweza kuwa ni ishara ya kumdharau na kujaribu kuonyesha kuwa haumuwazii lakini inaweza kuwa ishara ya woga uliozidi kipimo.

Muhammad Ali, bondia maarufu kuwahi kutokea duniani aliwahi kubadilisha dini yake iliyopelekea kubadili na jina lake kutoka kuitwa Cassius Clay. Media na baadhi ya watu walisuasua kuanza kutumia jina lake jipya jambo ambalo kumbe lilikuwa linamkera sana Ali.

Siku moja akawa anapambana na bondia Ernie Terrell. Bondia huyu alikuwa anakataa kumuita Ali kwa jina lake jipya hata walipokutana katika TV Show kabla ya pambano. Ali akamwambia:

"My name is Muhammad Ali, and you will announce it right there in the centre of that ring after the fight, if you don't do it now,". Terrell bado akakataa!

Kilichofuata ni Ali kumchakaza Terrell kwa kipigo cha mbwa koko katika moja ya mapambano ya kihistoria yanayokumbukwa katika mchezo wa ngumi. Ali alikuwa anamchakaza mpinzani wake huku akimrushia maneno ya hasira na kejeli, “Jina langu Nani? What’s my Name?”.

Lissu amekuja katika uchaguzi huu kutoa changamoto ya karne katika medani za siasa. Anajua hilo, wapinzani wake wanajua hilo, na sisi tunajua hilo.

Kuna siku aje amuamuru hasimu wake mkuu, alitaje jina lake sasa au atakuja kulitaja akiwa katika mazingira yasiyo rafiki sana kwake. Itapendeza akimuuliza hilo swali September 07, 2020.
Msimlaumu Rais Magufuli. Haoni sababu ya kumjua wala kutaja jina la Lissu. Hii inamwepushia kumpa kiki Lissu kuwa anatajwa jina na Rais. Na inampunguzia mzigo Rais wetu wa kubalance kwamba akimtaja basi awataje na wengine wote. Mgombea pekee ambaye hata mimi ningependa Rais Magufuli awe anamtajataja ni SIPUNDA HASHIMU RUNGWE!
 
Unakariri maisha hata enzi za ukoloni walikuepo kina Mangi sina Kinjekitilewa vita vya majimaji ,chief mkwawa wakipambania Uhuru wa Tanganyika wakashindwa.Alipokuja Nyerere wakajisemea kama tuliwashinda kina mkwawa je sembuse nyerere kikawakuta
Alikudanganya nani kukufundisha kwamba hao kina mangi walishindwa akaja kuweza nyerere?
 
Saizi tumeamua mkuu tayari mtaani tunahamasishana lisu kura anapata na za kutosha ,ukweli Ni kwamba ccm watu wameichoka wananchi wanaugulia moyoni ndio maana saiz tumeamua hii Ni 2020 kura yangu nampa lisu magu nilimpa 2015 ila hajaitendea haki saiz inaenda chadema
Yangu Nilimpa Lowassa safari hii nampa Magufuri So Bro hakijaharibiKa kitu tumabadailishanaa MAGU ATABAKI KUWA PRESDENT
 
Usiganganyike ndugu. Watu tulazimishwa na waajiri kwenda kwenye mikutano wa CCM ya kampeini. Hujasoma barua ya mkuu wa chuo hapa Dom akisema kuwa wafanyakazi wasiohudhuria watachukuliwa hatua za kinidhamu?

Barua hiyo ilikuwa hapa JF. Usiseme wingi wa watu katika mikutani ya CCM ni kukubalika kwa mgombea wa CCM. Watoto pia wanataka kumwona Rais ambaye wamekuwa wakimsikia kwenye radio na TV. Ni kawaida sana hiyo.

Nadhani haujaelewa nia yangu ya kuweka hiyo video. Iangalie halafu cheki responses za watu wakiambiwa ‘CCM hoyee’. Ni kama watu wako pale lakini siyo kwa ajili ya kutoa support.
 
Mungu amesha amua kwa neno lake Tundu Lissu awe Rais was nchi hii.
Mwenge umezimwa, CCM imekufa, wanapoteana.
Ule Moshi wa kishetani wa kutupumbaza, mwaka huu utawapumbazeni CCM , polisi, TISS, na tume ya uchaguzi
kosa kubwa wamefanya kuzima kafara lao la mwenge
watajuta
 
Mungu amesha amua kwa neno lake Tundu Lissu awe Rais was nchi hii.
Mwenge umezimwa, CCM imekufa, wanapoteana.
Ule Moshi wa kishetani wa kutupumbaza, mwaka huu utawapumbazeni CCM , polisi, TISS, na tume ya uchaguzi
Duh!
Lisu huyuhuyu Tundu?
Ebu acha kumkejeli Mungu kamanda!
 
Mmh! Kwamba Lissu ni tishio kwa Magufuli hata awe akimtaja kwa jina wakati wa Campaigns?

Sijui umri wako mleta mada; iwapo umefikisha 40s, basi, usiendelee kusumbua kichwa. Waliwahi pita akina Mrema, Lowasa. Hii ya huyu bwana mdogo Lissu mbona ni cha mtoto tu. Watanzania wana siasa wanazijua wenyewe. Watajaa kukusikiliza. Watasukuma hadi gari lako ati usimalize mafuta; kwenye kura sasa! Hapo ndiyo yanaanza, Nimeibiwa kura!

Lissu hawezi kumshinda Magufuli na kama bado huamini, subiri hiyo 28, Oktoba 2020.
Wewe umelewa sasa kama hutaamini magufuli anaondoka madarakani subiri hiyo octoba 28 mwaka huu usije ujajinyonga
 
Usiteseke hilo limeshaeleweka singida ulikuwa among top region's alikoenda kuangukia wazazi wa mpinzani kwamba. Mwambieni mtoto wenu aniachie na ninyi nichagueni yeye nitampa ajira. Pengine nimekosea ku kuyarudia maneno ila sipo mbali.

Hilo kiroho ni kukubadili kuwa huyu siyo saizi yangu, sitamuweza, wazee nisaidieni.
Huu uchaguzi una maneno mengi sana ya kwenye kanga.
 
Mmh! Kwamba Lissu ni tishio kwa Magufuli hata awe akimtaja kwa jina wakati wa Campaigns?

Sijui umri wako mleta mada; iwapo umefikisha 40s, basi, usiendelee kusumbua kichwa. Waliwahi pita akina Mrema, Lowasa. Hii ya huyu bwana mdogo Lissu mbona ni cha mtoto tu. Watanzania wana siasa wanazijua wenyewe. Watajaa kukusikiliza. Watasukuma hadi gari lako ati usimalize mafuta; kwenye kura sasa! Hapo ndiyo yanaanza, Nimeibiwa kura!

Lissu hawezi kumshinda Magufuli na kama bado huamini, subiri hiyo 28, Oktoba 2020.

Badilisha akili zako kidogo, maana hata Malawi walisema hivyo. Kupita wakina Mrema siyo kigezo wala sababu ya Lisu kutokushinda uchaguzi.
 
Back
Top Bottom