Obe
JF-Expert Member
- Dec 31, 2007
- 10,083
- 34,850
....kwa vile umeleta mfano huu kwa mfanano wa makubaliano kati ya Tz na kampuni la Dubai, tufanye hivi, barua ya uchumba imepokelewa na ikaazimiwa sasa inakuwa sio barua ya uchumba tena, majadiliano yanakaa kiposaposa na kwa sheria za 'kijamii' hapa pande zote zinafungwa na makubaliano yaliyoazimiwa. Posa hii ndiyo inayojadiliwa sasa maana uchumba umekubaliwa kwa maana ya mutual assent, na anayechumbia keshaleta barua ikaazimiwa (call it expressed valid offer na tumekubali 'acceptance' kama ndugu ---sijaziiona number kwa maana ya DPW watatoa kiasi gani mtoto wetu wamchukue 'capacity', na sisi kama wanafamilia 'bunge tumepima weeee (call it adequate consideration) tukaona huyu mchumba anafaa kuwa kwenye familia yetu. Yuko vizuriSina shida kama tukijadiliana tukijua tunachojadili ni makubaliano (agreement) na si mkataba (contract). Tatizo ninalo liona na kinchoendelea ni kana kwamba kuna mkataba tayari.
Mkuu hebu turudi katika maisha ya kawaidia. Familia A ikipeleka barua ya uchumba kwa familia B hatuwezi kujadili hiyobarua kama ndoa kati ya C NA D kutoka familia A & B respectively. Uchumba siyo ndoa, na barua ya uchumba kabala yajapokewa kukubaliwa na kujibiwa kuwa imekubaliwa hakuna uchumba.
Jirani mnoko na ni mlevi tu tunamjua hatukumshirikisha kwenye tulipopokea barua ila kwenye kujadili kuikubalia barua ya uchumba tukwambia bwanawewe karibu, kaja kilevi na maarifa yake anasema mbona mnataka kuukubali huu uchumba unaosema sio kwamba anamtaka binti yenu tu bali na wadogo zake wa nyumba hii walioko Tanganyika kule kote wanakofanana? Sisi kwa mahaba ya mleta posa aliyevaa kanzu na koti (hivi ni lazima washanga wavvae hivi!!!) tunasema wewe jirani ni mlevi na una nongwa.
Mdau, hapo nilipokoleza, bunge kuazimia maana yake binti ndo keshang'oka na jamaa keshaanza kujilia vya ndani ukirejea kwenye barua yake tuliyoiazimia kaazimia kuwa ataanza kumfaidi mwanetu kimazabemazabe kidogo kidogo kabla hamjamtengenezea sheria.