Lissu na Zitto kuipaka matope na kuisaliti Nchi yake hakujafanywa na mpinzani yeyote Duniani

Lissu na Zitto kuipaka matope na kuisaliti Nchi yake hakujafanywa na mpinzani yeyote Duniani

Sijui Lisu, Godbless na wafuasi wao wanawaza nn vichwani mwao. Hivi uende nje ya nchi kudai haki yako, ukitegemea nchi hizo tajiri ziwape wananchi wako hiyo haki unayoidai bureee bila maslahi!!

Ukweli ni kwamba, Lisu akifanikiwa na mpangomkakati wake huu aliouanzisha, mtasikia mashirika mengi ya serikali, migodi, rasilimali nk vimebinafsishwa . Na hii ndio hasara kubwa ya kuingiza mataifa tajiri kukusaidia kutatua migogoro nchini mwako .

Wafuasi wa Lisu, kaeni mkijua, siku Lisu akiwa raisi, watakaofaidika ni Lisu na vigogo wenzake. Wafuasi wake mtabaki kuwa mashabiki tu na mtaendelea kuminywa na kukandamizwa kuliko utawala huu wa CCM.
 
Themistocles alikuwa ni shujaa mkuu wa Ugiriki kwenye vita dhidi ya Waajemi na alisaidia kuwaongoza kupata ushindi mkubwa ambao utasimuliwa vizazi hadi vizazi. Alivyorudi na ushindi mkubwa mabwanyenye na watawala wa Ugiriki hawakutaka kijana huyu alete changamoto kwenye utawala wao, wakapanga njama dhidi yake. Themistocles kuwa mjanja akaikwepa hii njama na kutoroka nchi. Unajua alirokea wapi ??? : Alitorokea Uajemi kulekule kwa maadui zake wakubwa ambapo alipewa mapokezi makubwa, hifadhi na ardhi.
Mkuu kwa uwezo wa akili ya hawa vijana wa mbogamboga kamwe hawataweza kuuelewa huu mfano wako.
 
Af ndo wanataka et wachaguliwe kuwa viongoz[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Unatofautishaje huyu anaenda nje kuipaka matope nchi yake, na huyu anaenda nje kudai uhuru?

Maana hata Nyerere alienda nje Umoja wa Mataifa.

Sasa Nyerere alienda Umoja wa Mataifa kuipaka matope nchi yake au kudai uhuru kutoka kwa wakoloni?

Na Lissu akikwambia anaenda nje kujipanga kudai uhuru kutoka wakoloni weusi walioiba kura, kwa sababu ndani wameweka katiba dhalimu ambayo hairuhusu kupinga matokeo ya urais yakishatangazwa na hiyo tume ya ma puppet ya uchaguzi, utasemaje?
 
Ndio maana laana zimewaandana, huyu ajali kila siku yule kawa mlemavu wa maisha, na bado, BTW sijui kuhusu tundu lkn najua Zito alilelewa bila ya Baba, hivyo kuna kitu hana au alikosa, ...
Kwa comments hizi, mtarajie watu wawe wazalendo?Kwanini wasione bora hata kushirikiana na shetani kuliko nyinyi?

Leo hii Jiwe likifa au likapata kilema cha Kudumu, watu watashangilia na kubeza kama unavyobeza ulemavu mliomsababishia Lissu.

Nyinyi ni kikundi cha wanyama wenye muonekana wa binadamu mlio tayari kufanya lolote kisa madaraka na kupata uteuzi.
 
Hayo ni matokeo ya Wapinzani kuonwa kama maadui, kunyanyaswa na kuteswa na hata kuuawa, kifupi wapinzani wamenyimwa haki zao zote zilizopo kikatiba, katika hali hiyo unatarajia wafanye nini ??!!.

Mwanasiasa ni sawa na mvuta sigara, kama jinsi ni vigumu kwa mvuta sigara kuacha sigara ndivyo ilivyongumu kwa mwanasiasa kuacha siasa, wamezuiwa kufanya siasa kinyume cha sheria sasa watafanyaje!!!----- wewe badala ya kumlaumu aliyejamba unamlaumu aliyetema mate!!![emoji1787].

Ugali umemwagwa na wao wanamwaga mboga.
 
Kwa comments hizi, mtarajie watu waipende hii serikali na viongozi wake?

Leo hii Jiwe likifa au likapata kilema cha Kudumu, watu watashangilia na kubeza kama unavyobeza ulemavu mliomsababishia Lissu.

Nyinyi ni kikundi cha wanyama wenye muonekana wa binadamu mlio tayari kufanya lolote kisa madaraka na kupata uteuzi.

Jambo niseme mimi, adhabu apewe mwingine?
 
Alitorokea Uajemi kulekule kwa maadui zake wakubwa ambapo alipewa mapokezi makubwa, hifadhi na ardhi.
Ndiyo ukawa mwanzo wa uajemi kuwa imara kivita...( labda na huu ndiyo ujumbe uliotaka kuufikisha kwetu)!

Nitajaribu tena kuifuatilia historia ya mgiriki huyo kama aliwahi kutamka ama kuonyesha nia ya kuitakia mabaya uUgiriki na wagiriki ama kuionyesha dunia kuwa anataka kufuta uwepo wa wagiriki na ugiriki yenyewe!

Ndugu Antipasu katamka na kaonyesha hayo niliyosema/ andika hapo juu dhidi ya watanzania na Tanzania yetu.
 
Lisu na Zitto wanasema hali halisi iliyopo Tanzania. Msemakweli siyo msaliti.
Wapinzani wote Afrika hawajawahi kwenda kwa mabeberu kushtaki akina Lisu na Zitto kabwe Ni wa kwanza

Ukienda Afrika kusini Kuna akina Malema wapinzani hasa ila hawajawahi kwenda nje kushtaki nchi zao ukienda Ghana mpinzani ambaye Ni Raisi Sasa hajawahi kwenda nje kuchongea nchi yake kwa wazungu ukienda Kenya hapo Laila Odinga Ni mpinzani hasa hajawahi kwenda chongea eti Kenya inyimwe misaada pamoja na kupigana wenyewe kwa wenyewe lakini hajawahi nyanyua mdomo kuoandikia jumuiya ya kimataifa iishughulikie Kenya

Ukienda Rwanda Kagame alikuwa mpinzani miaka lakini hajawahi kwenda ulaya akiwa mpinzani kutaka nchi iwekewe vikwazo au akina Museveni pia wakiwa wapinzani enzi za dikteta Idd Amini hawajawahi kwenda ulaya kuomba nchi iwekewe vikwazo au inyimwe misaada

Hata Mandela hajawahi omba ulaya au Marekani waiwekee vikwazo Afrika ya Kusini

Hawa Lisu na Zito Ni vibaraka wa kwanza toka Afrika iwepo kuonyesha usaliti dhidi ya zao kwa wazungu na wamarekani
 
Themistocles alikuwa ni shujaa mkuu wa Ugiriki kwenye vita dhidi ya Waajemi na alisaidia kuwaongoza kupata ushindi mkubwa ambao utasimuliwa vizazi hadi vizazi. Alivyorudi na ushindi mkubwa mabwanyenye na watawala wa Ugiriki hawakutaka kijana huyu alete changamoto kwenye utawala wao, wakapanga njama dhidi yake. Themistocles kuwa mjanja akaikwepa hii njama na kutoroka nchi. Unajua alitorokea wapi ??? : Alitorokea Uajemi kulekule kwa maadui zake wakubwa ambapo alipewa mapokezi makubwa, hifadhi na ardhi.


Kwa mfano hai huyo Themistocles ndiye nani??
 
Sasa Nyerere alienda Umoja wa Mataifa kuipaka matope nchi yake au kudai uhuru kutoka kwa wakoloni?
Tanzania ilikuwa protectorate iliyowekwa na umoja was mataifa kuwa chini ya mwingereza Nyerere alienda kule kuomba Tanzania ipewe Uhuru toka kwa mtawala husika hakwenda kule kuomba Tanganyika iwekewe vikwazo au inyimwe misaada au kumshtaki Gavana wa kiingereza!!!

Usilinganishe akina Lisu na Zitto Kabwe Hili Ni genge la wasaliti wa nchi
 
Usiwe mjinga wa kutupwa, Magufuli ndiye aliye na anayeichafua Tanzania
Kwa matendo yake ya hovyo kuwahi kutokea.
Tuambie humu hayo unayodai ni matendo ya hovyo ya Magufuli
 
Sio makosa ya tume Bali Magufuli na Maharamia WA CCM walitaka sio ushindi Tu Bali WA asilimia themanini na kitu ulitegemea nini?.
 
Hawa jamaa siwatofautishi na SAVIMBI. Lakini wataenda kuabika sana na watakwenda kutubu na kujutia hayo wanayo yafanya.
Kwanini hawawezi kutumia elimu yao vizuri katika kufanya positive decision? Mtu mwenye elimu tunamwaangalia kwenye uwezo wa kufanya decision.
 
Alipinga mabaya ya kwenye migodi kule Mara baadaye akakosana na watawala wa nchi yake akaenda kujiunga na wale wawekezaji wenye migodi kuishambulia nchi yake.
Huko kwa adui wa nchi yake akapewa fedha na makazi ili aishambulie vizuri nchi yake?

Kwa hivyo hapa naona ile kanuni ya a friend of my enemy is my enemy and Enemy of my enemy is my friend. Kwa hivyo unakaribia kusema hii ni official declaration ya kuwa Tundu Lissu is an official enemy of our state?
Because State leaders are there to represent state's interests on behalf of the citizens of that state....so, enemy of our state leader is an enemy of our state's interests.
Therefore,he is an enemy of citizens of that state.

LISSU OFFICIALLY DECLARED AS PUBLIC ENEMY OF UNITED REPUBLIC OF TANZANIA by his supporters..[emoji2]
 
Je wale watanzania waliohusika na Richmond,EPA,Kagoda ,Dowans,IPTL,Richmond na Meremeta waliitangaza vyema Tanzania kunako medani ya kimataifa?
 
Tanzania ilikuwa protectorate iliyowekwa na umoja was mataifa kuwa chini ya mwingereza Nyerere alienda kule kuomba Tanzania ipewe Uhuru toka kwa mtawala husika hakwenda kule kuomba Tanganyika iwekewe vikwazo au inyimwe misaada au kumshtaki Gavana wa kiingereza!!!

Usilinganishe akina Lisu na Zitto Kabwe Hili Ni genge la wasaliti wa nchi
Hata sasa hivi mtawala anayetawala kwa kuiba kura ni sawa na mkoloni tu.

Na mwananchi kama anaona hapati haki ndani ana haki ya kwenda kujipanga nje.

Msimnyanyapae.

Profesa Safari aliongelea habari ya mtu aliyejamba, mwingine akatema mate. Kwa sababu huyu wa kwanza kajamba.

Halafu, watu wakaanza kumsema huyu aliyetema mate. Kwa nini umetema mate?

Akasema mimi nimetema mate, kwa sababu huyu kajamba.

Magufuli kajamba. Wapinzani wametema mate kwa sababu Magufuli kajamba.

Kwa nini mnawasema waliotema mate mnamuacha aliyejamba?

 
Wanakurupuka sana kwenye siasa, hawana maadili, hawana uzalendo kwa Tanzania, Hawawaheshimu Watanzania wanajali matumbo yao tu, Hawana Subira, ni wakaidi, Wabinafsi n.k .

Wangekuwa Wamarekani wangekuwa kuzimu tayari, Wangekuwa China wangekuwa kuzimu tayari, n.k. Tundu Lissu hana la kukifundisha kizazi cha sasa zaidi ya kukiharibu na kukitia najisi.

Haijawahi tokea nchini Tanzania Mgombea akatangaza wazi anaunga Mkono ushoga.
 
Back
Top Bottom