Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

Hivi Lisu ana Kosa gani halali kabisa ukilinganisha na yeye kupigwa Risasi halafu waliompiga hawajakamatwa wala kutafutwa ?
Yani hiyo kesi yake ni kubwa kuliko kesi ya mtu kujaribu kuua ?
Je, kuna mahakama huru ya kumtendea haki au ni mahakama iliojaa majaji na mahakimu makada wa CCM?

Lakini pia tunajiuliza kuwa inamaana hukumsikia Kheri Mwenyekiti wa UVCCM akitoa Tamko la chama kwa Vijana kuwa kwa sasa wameamua kuwa hawatampiga tena risasi Bali watamchoma sindano ya sumu.??
Kwa hiyo mnataka tusubiri mpaka yamkute ya Kolimba, Mzee wa kiraracha, Mzee wa mamvi , Baba mkubwa wa Tanganyika, na baba mkubwa wa Zanzibar?
No ni bora ahame tu nchi.

Kama Trump amepata Urais akiwa na miaka 72 basi hata Lisu ipo siku kizazi hiki kitaamua kufuatilia Rikodi yake na kujua kuwa alikua yupo sahihi na hakuwahi kuiibia nchi kwenye udhalimu wa wakiodhulumu na wanaolindana.
 

..Hakuna mahali nimesema kila anachokisema Tundu Lissu ni sahihi.

..Ila kuhusu nani aliyemshambulia naamini Tundu Lissu yuko sahihi.

..aliyetuhumiwa hajajitokeza na kupinga madai ya Tundu Lissu. WHY?

..pia hakuonekani juhudi zozote za kuchunguza tukio lile. WHY?

..nani ana mamlaka ya kuondoa walinzi area D? nani anaweza kuelekeza uchunguzi usifanyike?

..maswali hayo ndiyo yanayonifanya niamini madai ya Tundu Lissu kuhusu nani alituma magaidi mchana wa Sept 7, 2017.

..Tundu Lissu alijua akirejea atapewa ulinzi wakati wa kampeni. Vilevile alitegemea atashinda Uraisi. Kama ndoto zake zingetimia basi maisha yake yangekuwa salama.
 
Nchi imekuwa ya hovyo kabisa hii!!
Viongozi wa chadema wamekuwa watu ovyo sana, kwani walipokuwa wanaitisha maandamano hawakujitayarisha na yote haya. Sasa lissu angebaki na kufanya juhudi za kukirekebisha chama chake, kuliko kukimbia, na kama kuna ukweli wa maisha yake kuwa hatarini, basi wananchi wengi wangesimama na yeye. Lakini hizi siasa za kuwaingiza watoto wa watu barabaranina wao kujificha hakupendezi
 
Naomba unijibu hoja hii niliyoipost dakika 20 zilizopita kisha na mm nitakujibu maswali yako yote uliyoyauliza hapo juu.

Kama kweli CCM ilikua inataka kumuua Lisu, kwann haikumuua wakati wa kampeini za uchaguzi??

Na ni kwann kila anachosema Lisu wafuasi wake wote ná mataifa mnaamini??
Mtazamo wangu ni kwamba huyu anatumia taaluma yake kujihami na kesi yake na kuionyesha dunia anaonewa.
 
Hivi wewe una uhakika gani huyo Lisu anayoyasema ni ya ukweli au ni firigisu ili kuleta mkangany’iko kwenye jamii yetu??
Ni kweli kwa sababu tuko huku mitaani .
Ni kweli kabisa kuwa watu wanaoishabikia CCM wazo lao ndani na nje ya serikali ni kuwa Lisu auawe ili pasiwe na mtu wa kuwasumbua mana wengi wanawaza kwa karibu kuwa Lisu akiuawa basi mambo yatakwenda vizuri na hakuna wa kuwasumbua na akitokea mwingine naye watamfanya hivyo hivyo.

Inawezekana hata Mkuu wa nchi hajahusika laki pia hakuna tamko la kukanusha Kauli ya mwenyekiti wa UVCCM ambaye alitoa tamko la Chama kwa vijana kuwa watamchoma sindano ya sumu.
Hivi kama alisema hadharani na akashangiliwa inakuwaje kwenye mikakati yao?
Umesahau kuwa hata makamu wa Rais alisisitiza kuwa wao wameandaa watu wa kupiga risasi moja tu.?

Hivi huoni kuwa kuna kila dalili ya kuwa anayosema ni kweli.
Hivi unafikiri adui wa watawala ni nani kama sio yule anayeonekana kuungwa mkono na miongoni mwa watawaliwa?

Hivi unacheza na kumiminiwa risasi 16 ? Kukoswa tu na risasi kunaweza kukakutoa kinyesi sembuse kupigwa hata ingekua moja? Sasa kwa nini asiogope kutishiwa kuuawa ?
 

..wameishapima kina cha maji wameona wananchi hawawezi kusimama na Tundu Lissu iwapo lolote litatokea.

..kama maandamano yameshindikana Unguja na Pemba unadhani yanawezekana huku Tanganyika?

..mimi nadhani maandamano yalitakiwa kufanywa na vijana wa Chadema na ACT na siyo kutegemea wazee kama Maalim, na Lissu, kuwa mstari wa mbele.

..hata CCM wanaofanya unyama na kuiba kura siyo wazee watu kama Magufuli na Mangula, bali ni vijana wa UV-CCM.
 
Una haki ya kuamini kile unachoamua kuamini, maamuzi ni yako.

Hivi Lisu ni wa kwanza kushambuliwa na risasi hapa duniani??

Kama anaona waliohusika kummiminia risasi hawakamatwi kwann asingeita FBI wa marekani wamsaidie kwenye hilo, badala yake alikua akipita nchi tofauti akiiongelea vibaya Tanzania??
 
Well, inawezekana kuwa hivyo.
Kama hilo linawezekana, basi kwa mtazamo wangu Lisu hawezi kua mwanaharakati bila kuwa mwanasiasa. Nitafurahi sana kama ataenda kuendeleza harakati zake huko ubelgiji. Akagombee ubunge au hata uraisi hukohuko ubelgiji sababu inasemekana ubelgiji wanampenda sana na ni mtu mashuhuri sana dunia nzima inamtambua.
 
KIPINDI KILE ALIPOPIGWA RISASI CHADEMA SIWALISEMA WALIOMBA FBI NA SCOTLAND YARD WAJE KUCHUNGUZA SERIKALI IKAKATAA
 
Hujui chochote ngoja nikupashe!!
Hivi unajua ni kwa nini alikua anatumia sana umati wa watu na kuzungukwa Mara kwa Mara na umati Huo!!

Hivi unajua waliokua wanamzunguka ni askari polisi waliokua wamevaa kiraia ili kumlinda wakati wa kampeni?
Unajua kuwa akifa mgombea mmoja wa Urais uchaguzi unaahirishwa na inakua ni gharama kubwa sana kwa nchi?
Hivi unajua kuwa kumuua mgombea wakati wa kampeni kungeweza kuleta visasi vikubwa sana na kuiingiaa nchi kwenye machafuko makubwa mana matumaini ya watu kwa mgombea wao ni mkubwa sana kwa kila chama?

Unafikiri ni kwa nini CCM kupitia Mwenyekiti wa UVCCM Mh.Kheri walitoa tamko la kumchoma Lisu sindano ya Sumu? Hizo hazikuwa njama za kumuua?
Hivi unajua unapotaka kuestablishi utawala wa kidikteta na kujenga hofu kwenye jamii ili watu waufyate mkia mauaji huwa yanafanywa mchana kweupe ili iwe kuwatia adabu wanaojifanya wakorofi?
Unajua Korea ya Kaskazini waziri akikosea anaoigwa Kombora akiwa kwenye gari mchana kweupe?

Unajua hata wakati wa Ukoloni wa wajerumani watu walinyongwa mchana kweupe ili kuwafanya watu watii sheria za mkoloni na kumwogopa mkoloni??

Hivi unajua hata magaidi wanapowateka watu na kuwalazimisha watii sheria zao kitu cha kwanza ni kuwaua wale wanaopingana nao kwa kuwakata vichwa mchana kweupe ili anayejaribu kuwasaliti au kukimbia na kuachana na ugaidi atiwe hofu na kubaki kuwa mtiifu?
Usifikiri kuirudisha Tanzania kwenye mfumo wa chama kimoja na kudumisha fikra za mtu mmoja litakua ni jambo la kuwalisha watu tende na halua ; Tukiamua kurudi huko nyuma kwenye chama kmoja jiandae kuona rangi na harufu ya vimiminika vyekundu vikitoka kwenye miili ya watanzania wengi wanaopinga au kukosoa wakubwa.
Itafikia mahali hata kumkosoa Mtendaji kata itakua ni vigumu kwani jioni watakuja vijana wa uvCCM na kukumiminia risasi na kusepa zao na uchunguzi utafanywa na wakereketwa wenyewe ndani ya vyombo vya ulinzi na kusema kuwa ni majambazi.
Damu za watu hua inalipwa kwa damu ndio msingi wa karma.
Usione hata Rwanda au Uganda wapo pale baada ya waliojiona wababu miaka iliyopita waliwaua watu kwa maelfu na malaki .Damu zikawa zinalilia kisasi.

Walichokosea Wanyarwanda na Waganda kupiga Kagame na Museveni ni kutoweka maridhiano badala yake wanatawala kwa damu tena . Mbaya zaidi watamwaga damu zisizo na hatia. Asil ya Mungu haitawaacha salama wajukuu zao watakapokufa wao na wale waliowaingiza kwa damu. Damu zinazomwagwa inalilia kisasi. Miaka michache ijayo Uganda italipuka na museveni atazeekea kubaya kumbe angeitisha maridhiano angekua amefaulu sana duniani na ahera.
Wamelewa kwa Mali .
Wamelewa kwa madaraka.
Wamelewa kwa ulinzi walio nao!!
Laana ya mwenyezi Mungu iwe juu yao.
 
Anatafuta tena huruma ya wananchi baada ya kuliwa kiboga na wananchi hao hao
 
KIPINDI KILE ALIPOPIGWA RISASI CHADEMA SIWALISEMA WALIOMBA FBI NA SCOTLAND YARD WAJE KUCHUNGUZA SERIKALI IKAKATAA
Kama serikali ilikataa ni sawa tu, kwani Tanzania kama nchi ina maamuzi yake.
 
Wakulaumiwa ni Mbowe mtu mbinafsi kupitiliza.
ACT ni kichanga sana lakini Chadema ni chama kikongwe lakini Mbowe ameshindwa kukijenga kiitikadi na kiimani.Ingekua ni CUF ile ya Lipumba kipindi hiki CCM wangeomba poo.

Hata hivyo ni bora Mbowe na wengine wamenyimwa Ubunge na wakurugenzi mana itasaidia kuwa na misimamo mikali ya kupambana na CCM badala ya kupambana na Magufuli pekee mtu ambaye ana mamiloni ya vijana wa kumsema na kumpigania.
Mbowe miaka mitano bungeni wanamzungumzia Magufuli na udikteta bila kujenga chama chao view jijini kwa kupeleka ruzuku huko kwa kuwalipa hata 50000/- viongozi wa chini. Unajua watu walioshiriki kuiba kura vijijini walipewa sh.20000/-- ,10000/- na 5000/- Kujenga itikadi vijijini ni rahisi sana lakini Mbowe aliamua kujifidia kupitia Ruzuku huku akitaka kujiweka kwenye status yake ya juu kabla ya mali zake kuhujumiwa.
 
Wakuache kipindi cha kampeni wakufate ukiwa umeshindwa ya kweli haya au ndoto zako tu
 
Kuna wengine wanajiona wana hati miliki ya nchi hii na niwabinafsi sana wakidhani wataishi milele na hivyo vyeo pole kamanda Lissu yana mwisho tu
 
Ninaelewa baadhi ya mambo mengi uliyoandika hapo kwenye gazeti hilo la nipashe.
Ila kwa kifupi, Mungu ndio anapanga nani awe kiongozi, dua lako la kuku halitompata mwewe. Pili, kelele za chura hazimnyimitembo kunywa maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…