Lissu ni kibaraka, anatumiwa na mabeberu wanaotaka kuiba rasilimali za Tanzania

Bora kuwa dalali wa Magharibi kuliko kuwa kibaraka wa Wachina..Tumewahi kuona balozi wa China anahutubia mkutano wa ccm,mbona hatuwaoni wazungu kwenye mikutano ya TL? ccm mtaweweseka sana mwaka huu
 
Mwaka huu mtaanzisha nyuzi nyingi sana za uongo na kweli, uzushi na uchochezi, lakini mpaka mtaongea ukweli tu! Lissu ndiye mkombozi wa hapa tulipokwama!
 
Meko ni dalali wa israeli mtoa roho na shetani mleta mateso kwa binadamu.

Bora Lissu dalali wa mabeberu wanaotuwesesha kupata scholarship na misaada kedekede kwa individuals na our country at large.
Mbona sijawai muona Meko huko Israel Kama nilivyomuona Mbeligiji huko Ubelgiji!?
 
Tanzania hii ndiyo Mwalimu Nyerere aliitaka, lakini Watanzania ndiyo tumeshabadilika hata hao CDM ndiyo walewale maana Ubinafsi umesha tutawala kwenye nafsi,kila mtu anataka kula na familia yake tu!!
 
Lissu Kama kweli yeye ni Mzalendo kweli,aingie CCM na ataona baada ya mitano ya Magufuli 2025 CCM watamsimamisha,Kama kweli ana nia ya dhati kuikombowa Tanzania!!
 
Nasikia mgombea wenu ashaanza kuchanganyikiwa. Sasa ilani kaitupa pembeni, anaanza kuahidi vitu anavyoahidi Lissu. Jana kuna sehemu alisikika akisema Mungu oyeee.
 
Lissu Kama kweli yeye ni Mzalendo kweli,aingie CCM na ataona baada ya mitano ya Magufuli 2025 CCM watamsimamisha,Kama kweli ana nia ya dhati kuikombowa Tanzania!!
Maskini hata kuandika Kiswahili hajui.
Ada aliyolipa mzazi wako ni kumtia hasara tu. Kuikombowa maana yake nini?
 
Lissu Kama kweli yeye ni Mzalendo kweli,aingie CCM na ataona baada ya mitano ya Magufuli 2025 CCM watamsimamisha,Kama kweli ana nia ya dhati kuikombowa Tanzania!!
Hatashetani huja kwa sura ya malaika akiwaaminisha watu ni mwema...Lissu ni Sio hata kidogo.

Kuna mambo yanayosababisha watu tuamini kuwa Lisu ni mpango wa Mungu .
JPM aliletwa na Mungu kama alivyokuwa Yohana Mbatizaji aliyetangulia kunyoosha njia ya Masihi.
JPM kazi yake ya inapaswa kukamilishwa na Mpenda haki.

Jiulize ni kwa nini Lisu apigwa risasi 16 kisha apone na kurejea akiwa na akili zake Timamu nila woga.
Hivi yeye halendi kuishi kama hao wengine ambao walishastaafu lakini bado wanapigania maslahi yao?
Kwa nini Mungu aiepushe Tanzania na Korona uchaguzi uendelee bila kuahirishwa. Si ingekua rahisi tu kuendelea na Korona ili Yohana aendelee hata mpaka 2025?
Kwa nini Mungu amrejeshe Lisu wakati Makonda mtumia nguvu za Risasi akiwa amejiuzulu Ukuu wa mkoa kwa hiyari yake ?
Kwa nini Mungu amrejeshe Lisu wakati wa msiba mkubwa wa Mkapa na kuacha nafasi kwa wananchi kumpokea nila kupigwa mabomu na kuumizwa.?
Kwa nini Watanzania wamejawa na Furaha kumuona Lisu bila hata kulazimishwa wala kuahidiwa vyeo kama wengine wanavyofanya ili kuwafurahisha watu?
Kwa nini watu wamejawa na ujasiri walipomuona Lisu na Hofu kuwajaa CCM wenye Mabomu na risasi kwenye maghala yaajeshi wanayotumia kuwatisha watanzania Wenzao?
Kwa nini CCM imepoteza dira ya utu,haki, usawa, umoja shikamano na serikali kutojifungamanisha na dini wakati huu wa uchaguzi?,

Bila shala Mungu ameingilia kati na kuchukua huzuni ya watanzania.

Huwezi kuwaua watu kwa dhulma unayofanya eti unapigania rasilimali zilizoumbwa na Mungu.
Dunia ni ya Mungu na vyote tutaviacha.
Kuua watu,kutesa watu na kunyanyasa watu waliombwa na Mungu kwa sababu ya yale anayotengeneza mwanadamu kwa Kodi zao ni jambo baya sana.
 
Huenda uko sahihi lkn naomba nifafanulie kuhusu
- fao la kujitoa kwa watumishi,
- asilimia 3 - 15 elimu ya juu,
- bei ya mazao ya kibiashara kuporomoka (pamba 2,100 - 880; kahawa 2300 - 1100; korosho nk nk). Mazao ya chakula muhogo 600 - 250);
- hivi sukari inauzwa bei gani kweli

Kwa ufupi huenda hoja yako iko sahihi lkn tujiulize hizi hasira za hawa uliowaita watanzania zinatokana na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…