Tajiri Tanzanite,
Kuliko kutuletea utawala wa kikabila na kidini na kikatili ni bora tu waje hao Mabeberu waweke hiyo mikataba ya siri.
Kwani ni mkataba upi uliowahi kuganywa kwa wazi na hao CCM?
Hivi Huseni anatafuta nini kule Zanzibar?
Hivi mnatafuta nini kama watanzania wanamtaka Lisu?
Ina maana Mabeberu watakuja kumpigia Kura Lisu?
Ina maana wale watanzania wanampokea kwa maelfu ndio Mabeberu?
Hii nchi kama kweli kuna mtawala mzalendo basi ajae na sheria ya kuweka wazi mali za Makada wa Chama cha Mapinduzi na jinsi walivyozipata kuanzaia awamu ya kwanza waliofilisi Mashirika ya umma na vyama vya ushirika na baadae kujiuzia nyumba zote za umma na kila kitu cha umma kwa bei chee na wengine kujimilikisha mali za umma kwa mikopo ambayo haikulipika ipasavyo . Kila kitu maCCM walishakichukua na kukimiliki na familia zao. Usione mavyombo ya dola yakiongozwa na Makada wa CCM kinyume na katiba lakini ni kuwa ni watu walioshiriki kwenye kujimilikisha utajiri wa nchi hii.
Hawana lolote Makada wa CCM walioko kwenye mahakama ,Vyombo vya dola n.k, wote ni wanufaika wa rasilimali na kodi za nchi hii bila huruma.
Wapo tayari kutumia Dola kuua kila mtu wabaki peke yao kwa kisingizio kuwa wao ndio wanaolinda amani ya nchi huku wakijua wazi rohoni mwao kuwa wanalinda wizi wao.
Ogopa watu wanapata madaraka kwa dhulma , uchawi,rushwa ,uzinzi, ahadi za kupeana madaraka na vyeo vyenye maslahi. Watu wanaopeana madaraka wakiwa kwenye mabaa wakiwa wamelewa pombe kichwani. Hakuna Mtawala mwenye huruma na mtu zaidi ya nafsi yake na familia yake. Ndio maana wakishapata wanawapa vyeo watoto wa Dada,shangazi , wajomba ,mashemeji, n.k.
Ndio maana tunataka Lisu naye apate tu aweke sheria Kali na asimamie Katiba.
CCM wanakosa umakini ndio maana tunaibiwa na wazungu.
Kinge kinawapiga chenga matokeo yake hata mikataba inakua ni holela na hawaisomi mana imeandikwa kingereza.
Lisu ndiye jawaba ya hao wazungu mana anaijua sheria na sio mtu wa kudanganywa au kuandika mikataba ya kijinga.
Mungu ndiye nayejua kuwa nani atashinda uchaguzi wa mwaka huu.
Mungu amechoka kuwa chini ya binadamu na kuona mtu anatukuza kuliko yeye.
Lisu angekua anatamaa ya Fedha kama hao wazalendo waliokuwapo miaka yote na wakashiriki kutuibia na kujilimbikizia mali zote za nchi hii na hata Mungu anaona wanavyodanganya midomoni mwao huku mioyoni mwao wakiwa wameficha mali walizochuma kupitia SERIKALI ya CCM iliyotawala tangu Uhuru basi angejipendekeza kwao na kupata nafasi za kujilimbikizia mali kama walivyofanya wengine.
Ogopa mtu anayepigwa risasi 16 halafu bado anasema Yale Yale bila kubadilika.
Hao wengine hawapendi hata kujibiwa tofauti na wanavyotaka sembuse kupigwa risasa hata iwakose wangejenga Chuki isiyoisha.
Lisu ni mvumilivu sana na Mungu anamwona na anpango naye. Hakuna namna kama Mungu amepanga hakuna wa kumzuia na atakayezuia mpango wa Mungu ataaibika milele.
Adamu alipoumbwa na Mungu alipewa amri au Katiba ya kuifuata na sio Madaraja wala mareli na mabwawa.
Adamu Alihesabiwa kuwa amemwasi Mungu pale aliposhindwa kufuata amri au Sheria au Katiba aliyopewa na Mungu .
Tunataka Kiongozi atakayetuongoza kwa haki na mwenye kufuata sheria au katiba ya nchi . Mwenye kutenda haki na asiyembaguzi wala makabila na akijaribu kuwa mkabila basi atakutana na katiba na sheria inayomkataza na kuweza hata kumvua uongozi.
Katiba tuliyo nayo inampa mamlaka Rais kuweza kuweka hata serikali nzima ndugu zake wa familia yake tuu. Na hakuna wa kusema na ukijaribu unapewa kibano cha uhakika. Hii ni zaidi ya Ubeberu. Tumwache Lisu mana hata ujio wake umebadili watu ndani ya CCM walioanza kujawa na kiburi na kumdharau mpaka mungu na ukuu wale kwa kusema kuwa kuna mtu ameikimbiza korona .
Kuhusu rasilimali kuwapa wazungu ni uzushi mana mpaka sasa nchi hii haina kilichobaki .Mpaka Ardhi ya nchi yetu ilyouzwa kwa Mwarabu Kule Loliondo hatujasikia Mzalendo feki yeyote akiizungumzia . Tafakari utagundua kuwa CCM ni kama alivyosema Prof. Lipumba. liyeamua kutumia viongozi wa Dini matapeli na wabinafsi wanaotumia shida za watu kujitajirisha na kujilimbikizia mabilioni ya pesa na Mali za kila aina bila kuwa na uchungu na maisha ya watu maskini na wengine waliwatukana mpaka makadinali enzi za JK kwa sababu tu ya kuuchukia uislama wa JK, leo wanagombea Ubunge kupitia Chama kile kile walichotumia kumtukana JK na kadinali Pengo.