Lissu ni Taasisi inayotembea, tukimpoteza tutapoteza mengi, akosolewe bila matusi

We are here postive impacting leaders not for chama, akizingua na yeye tutamsema pia.
But for now give him.benefit of doubt
 
Hili halina Ubishi kwa sasa mtu anayeweza simama mwenyewe BILA mfumo, au madaraka ! Wanaomfuata lissu hawataki Pesa kwake ni sera tu


Britanicca
Hana hela za kugawa. Anagawa Madini tu.
Tundu Lissu ni kama Chujio, wapenda pesa badala ya utawala bora kwa wananchi wote watajitenga tu. Kwa Lissu hakuna hela za kuchota😆😆😆
 
Kinacho nishangaza ni pale anapopuuza juhudi za Mbowe kukilea chama na kutafuta watu wenye uwezo kujiunga na chama akiwemo yeye Lisu.
Mkuu wewe uko biased, hakuna anayepinga Mchango.wa Mbowe, hata Lissu hakuna mahali amepinga kazi nzuri ya Mbowe, Labda kosa la Lissu ni kutamka hadharani na kuonya yabia zinazoingia mwenye chama kinachoamknima na Wananchi wengi chama safi.

Sasa anapoonya mambo mabaya kama haya kwanini aonekane mbaya? Kwamba Rushwa Kwa Mbowe itakuwa halali kwa kuwa amekilea chama?
 
Alishapigwa Risasi akiwa mwenyewe akaenda Ahela( Purgotory) akawaona wafu, Mungu akamrudisha kwani bado Mision iliyomleta haijatimia.

Sasa sijui unataka kumtisha nini.

Tundu Lissu alismama peke yeke Kwenye Sakata la Migodi 1998 huko Geita kipindi wananchi wakiwa enzi za ujima, nchi nzima ccm. Alikamatwa na Rais Benjamin Mkapa akiwa peke yake, akafungwa peke yake akashtakiwa na akashinda kesi.

Lissu aliporwa ubunge Singida Jimbo lake peke yake enzi za Kikwete, akajisimamia mwenyewe kama shahidi na kama Wakili peke yake akashinda kesi jimbo likarudi, Muulize Kikwete atakwambia habari za Lissu.

Lissu akiwa Recrut JKT alisimama na kumhoji Meja aliyekuwa anaendesha Training Mbele ya Waziri Mwinyi. Hivi unajua Jeshini Recruit kupingana na Trainer unakuwa unajitafutia Kifo? He did it na marafiki zake walijua Mwisho wa Lissu umefika. He defended his aguements and won.

Lissu hajawahi kushindwa for your information
 
Hili halina Ubishi kwa sasa mtu anayeweza simama mwenyewe BILA mfumo, au madaraka ! Wanaomfuata lissu hawataki Pesa kwake ni sera tu


Britanicca
Hahaha hili unalijuaje? Watu wanatafuta pesa kwa viongozi/watawala huanza kama supporter na akichukua madaraka ndio hao wanakuwa machawa na kutusumbua kama ilivyo kwa ccm kwa sasa.

Watawala wanaweza hata wasijue tunanyanyaswa vipi, kwasababu machawa wanatushughulikia kimya kimya kumlinda bosi wao.
 
Yeye ni makamu mwenyekiti, na Chadema wana vikao na mabaraza ya kuzungumza. Anatuambia ili sisi tufanyeje?

Baada ya kueleza kachukua hatua gani kurekebisha hizo tabia zinazoingia kwenye chama?

Na wanaoziingiza kawachukulia hatua gani, au alituambia sisi ndio tuchukue hatua?
 
Huu ndio utaahira wa hicho chama Cha wajinga,inajenga mtu badala ya taasisi siku akizingua chama kina zingua.

Mwisho Kwa hiyo kwake ni ruksa kutukana na kuchagua wengine ila yeye haitakiwi kuchafuliwa si ndio? Upuuzi

View: https://x.com/VisitTanzania1/status/1869806482067468715?t=LlaES2D-6mc03txvubLHQA&s=19
 
hapana
 
Yaani huu ni ukweli ulio wazi, Sijui wanachadema wamekumbwa na nn, yaan lissu kwa sifa zake, wazee wa chadema wangemwomba mbowe amuunge mkono lissu Ili chama kisogee mbele zaidi.Kikubwa waangalie maslahi mapana ya nchi na chama, nje ya hapo muda utasema
 

Umeona mbali sana kiongozi ngoja tuone kama wengine pia wanaona au wanafuata mkumbo tu km jk alivosema watanzania 70% hawana mwelekeo wanaangalia wapi upepo unaelekea na kukikimbia tu kama swala
 
We are here postive impacting leaders not for chama, akizingua na yeye tutamsema pia.
But for now give him.benefit of doubt

Yetu macho.

Amandla...
 
Lisu ni kiongozi mzuri na mwenye maono na anaeipenda nchi yake, lakini apunguze mdomo na ujuiaji mwingi, binaadamu hutakiwi kuropokaropoka kila unachokiwaza.
 
Lisu ni kiongozi mzuri na mwenye maono na anaeipenda nchi yake, lakini apunguze mdomo na ujuiaji mwingi, binaadamu hutakiwi kuropokaropoka kila unachokiwaza.
Umeshaharibu.....umekoment kinafiki. Kuropoka ndio kudanyaje? Acha wivu ana kuzidi akili.
 
Mimi nimeshaapa katu kwa kipindi hiki sitakuwa sehemu ya Chadema iliyo chini ya Mbowe. Nitastaafu rasmi haya mambo ya siasa japo bado sana ila ni bora kuendelea na mambo mengine kuliko kupoteza muda bila matokeo ya msingi.
Na mimi kuanzia kesho panapo uzima eidha nitakuwa mwanachama mpya wa chadema au nitaacha kufuatilia siasa za Tanzania kabisa.

Mbowe ataamua niweje
 
Hili halina Ubishi kwa sasa mtu anayeweza simama mwenyewe BILA mfumo, au madaraka ! Wanaomfuata lissu hawataki Pesa kwake ni sera tu


Britanicca
Wewe ni mpumbavu nilikidharau sana na zile thread zako za eti makonda is dead
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…