Ndicho kitu ninachosema kuwa hilo ni la Mahakama na SIYO la Executive kama anavyodai huyo ndugu mwingine. Tuiache Mahakama ifanye ya kwake hayo ya Lissu yatakuwa "ni kuingilia mhimiri mwingine".
Mahakama yenyewe ilishamwambia DPP akamilishe uchunguzi au awaachie watuhumiwa ndani ya mwezi mmoja.
Hiyo ilikuwa September 14 2019.
Sijui kilichofuatia ni nini hapo.
Labda Mahakama imepata "amri kutoka juu". Kitu ambacho si sawa. Hapo itakuwa executive imeingilia judiciary.
Pia, katika kesi hizi ambazo DPP/ Jamhuri ndiye anashitaki, rais ana uwezo wa kumuagiza DPP kumaliza kesi. Kwani DPP ni sehemu ya executive. DPP anafanya kazi kwa maelekezo ya rais.Hata leo Magufuli akimwambia DPP amalize kesi, kwa sababu hii au ile, au bila sababu, basi rais atakuwa sawa.
Na DPP ana uwezo wa kumaliza kesi, kwa sababu hii, au ile, au bila kutoa sababu.
Sasa unachosema hapo ni kwamba mshitaki aiachie mahakama iamue kesi.
Wakati mahakama ilishamuambia mshitaki alete ushahidi kesi imalizwe, au kama hana ushahidi, watuhumiwa waachiwe. DPP akamilishe ushahidi kwanza.Akikamilisha arudi kuanza kesi upya. Inaonekana DPP hayuko tsyari. Anafunga watu miaka nenda miaka rudi wakati hana ushahidi wa kuendesha kesi.
Mahakamq iliona watuhumiwa kukaa lupango miaka sita bila kuhukumiwa kwa sababu "uchunguzi unaendelea", ni kama wameshahukumiwa kifungo cha miaka sita kabla kesi haijaanza.