Simply I can say; "History is more than the path left by the past 'cause it influences present tmes and equally paints the future times.
Viongozi wa CCM siku zote huwaogopa sana watu wenye akili kubwa, hasa wale ambao wana uthubutu wa kuonyesha mapungufu yao. Hakika uwezo na umahiri mkubwa wa Tundu Lissu katka masuala ya kisheria, ndiyo hasa sababu kuu ya chuki kwake kutoka kwa makada vilaza na mahafidhina katika chama tawala.
Na hii si kwa Lissu pekee yake, bali hata hivi karibuni tulilishuhudia ukweli kupitia misimamo ya ex CAG Prof. Mussa Assad. Nchi inaendeshwa kupitia akili za watu wenye uwezo mdogo mno, kisa eti ni makada waaminifu wa chama tawala.
Wewe ebu jaribu kuchunguza sifa za wateule wengi walioaminiwa kushika madaraka hapa nchini baada ya kifo cha Mwl. Nyerere. Nachelea kusema wengi wao wala hawana sifa wala weledi ya kupewa dhamana hizo.
Hii ndiyo sababu iliyopelea mpendwa wetu Ben Saanane kukutwa na kizungumkuti pale alipoanza kuhoji uhalali wa shahada ya uzamivu yenye kugubikwa na utata mwingi ya mwendazake. Nathubutu kusema kusema Lissu alikutwa na yaliyomkuta na kunusurika kufa kutoka na hofu hii ya ukilaza iliyowajaa makada hao ili kuepuka hoja zake kinzani.