Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Posts
24,386
Reaction score
57,588
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi, asante Mungu umepona.

Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iliyopita.

Tuambie utafanya nini endapo utakuwa Rais, tuambie kwa nini wewe na si Magufuli tena.

Binafsi leo nilitegemea kusikia madini ni nini utaifanyia Tanzania/ Watanzania ambapo Magufuli kafail.

Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.
 
Siku kadhaa zilizopita Niliposema Lissu is not a " Presidential material", kwa wengi sikueleweka. Leo nadhani wengi watakuwa wameanza kunielewa!

Yaani badala ya kujenga hoja kwa wananchi wamchague, " Ni yeye" anaifitinisha Tanzania dhidi ya Jumuiya ya kimataifa. Tanzania ya watanzania tena ya wananchi wenye uwezo wa kumuweka madarakani.

Yaani anataka Jumuiya ya kimataifa ndiyo imuweke madarakani hapa nchini badala ya sisi watanzania ndiyo tumuweke madarakani. Sasa Lissu akisha wekwa madarakani na jumuiya hiyo ya Ulimwengu, atailipa nini!?

Siyo ndiyo, mwanzo wa Lissu kutuuza watanzania kwa mafungu...!!! Kwa hili, leo amepoteza nafasi adhimu ya kuwashawishi watanzania kwa hoja ili wamuweke madarakani.
 
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi,asante Mungu umepona.
Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iloyopita...
Lissu hana sera bali anasubiri Magufuli kesho afungue kampeni, atakachokuwa anaongea Magufuli basi Lissu atakuwa na kazi ya kumjibu. Kimsingi Lissu bado viatu vya Urais havimtoshi
 
Mm pia nilitegemea hilo, kwa kawaida siku ya kwanza ya ufunguzi wananchi wanakua na shauku au morali ya kusikia mgombea atawafanyia nn kama wakimchagua kwenye nafasi husika, kwa hili leo cdm imedhihirisha inakwenda kushindwa vibaya kwenye uchaguzi mwaka huu
 
Mimi ilibidi niache kumsikiliza baada ya kuona anatafuta sympathy kwa audience ila pia amesema tangu awe nominated na chama chake basi alianza kuandaa hotuba ya Kuisoma leo siku ya ufunguzi nao Team ya Chadema iliamua kubadili upepo kwa kuachana na kusoma hio hotuba pamoja na kuacha kuinaugurate manifesto yao ivo nahsi lissu aliambiwa abwabwaje tu vile anaona inafaa ila next time tutegemee hayo unayoyataka, ila at all Chadema unaona kabisa hawako Serious yani kwa maandalizi yale kuanzia high table mpaka podium ni aibu kusikia Eti viongozi top wa Chama ndo wangekuwa wenye ile shughuli yani Very roughly
 
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi,asante Mungu umepona..
mbona kwenye intro remarks kasema clearly kuwa leo hatasoma hotuba ya kampeni yenye sera / ilani?

kasema first things first - and the first things ni kuishiniliza NEC ihakikishe wagombea wote (ubunge na udiwani) walioenguliwa wanarejeshwa kwanza tena bila masharti yoyote.

kasema sasa hivi ni maandamano ya amani nchi nzima na ametaka uungwaji mkono wa jumuiya ya kimataifa.

Nape Nnauye Mwigulu Nchemba na wengine wote mliotangazwa kupita bila kupingwa futeni hizo sherehe zenu - hii ngoma bado mbichi kabisaa!!
 
Siku kadhaa zilizopita Niliposema Lissu is not a " Presidential material", kwa wengi sikueleweka. Leo nadhani wengi watakuwa wameanza kunielewa!
Presidential material yupoje? Maana wabongo aisee mnafurahisha sana kwa kujifanya mnayajua material. Tangu mjue material ya kutengenezea batiki basi imekua nongwa.

Kwa hiyo Presidential material ni yule ambaye anaagiza wakurugenzi kufuta wagombea, kuwateka, kuwabambikiza kesi ili wakose vigezo n.k?
 
Jazba zimemjaa watu hawajajitokeza wamempuuza,
JamiiForums1681771336.jpg
 
Back
Top Bottom