Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi, asante Mungu umepona.

Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iliyopita.

Tuambie utafanya nini endapo utakuwa Rais, tuambie kwa nini wewe na si Magufuli tena.

Binafsi leo nilitegemea kusikia madini ni nini utaifanyia Tanzania/ Watanzania ambapo Magufuli kafail.

Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.
Umekurupuka...jitahidi kukaa kwa kutulia...wewe ni mmoja wa wajenga hoja wazuri...kuwa Neutral...kama ulivyosimama kwenye suala la kuapishwa kwa Mwigulu
 
Ameongea zaidi ya saa nzima
Yaani saa nzima kaongea kuhusu kupigwa kwake risasi,waliokosea kujaza form wakaenguliwa na kupitisha bakuli la kuomba michango,kutoa number ya kuomba michango.
Siyo tuliyosubiria siku kuu kabisa ya ufunguzi wa kampein.
 
Presidential material yupoje? Maana wabongo aisee mnafurahisha sana kwa kujifanya mnayajua material. Tangu mjue material ya kutengenezea batiki basi imekua nongwa.

Kwa hiyo Presidential material ni yule ambaye anaagiza wakurugenzi kufuta wagombea, kuwateka, kuwabambikiza kesi ili wakose vigezo n.k?
Mbona unaongea/kuandika kikike?
Unaushahidi wa Raisi kutoa amri au ushauri huo???
 
Umekurupuka...jitahidi kukaa kwa kutulia...wewe ni mmoja wa wajenga hoja wazuri...kuwa Neutral...kama ulivyosimama kwenye suala la kuapishwa kwa Mwigulu
Ndo uneutral wenyewe huu,Chadema nao wakichemsha tunawasema ili wajirekebishe.
 
Lissu alitamka wazi kwamba hawezi kuomba kura wakati 30% ya wagombea wameenguliwa na pili alisema kwanza ndio anafungua kampeni hana budi kutoa shukrani kwa wale wote waliotia mkono kuokoa maisha yake!! Sasa ataoaje shukrani bila kueleza jinsi walivyo shiriki hao anaowapa shukrani?
Alitakiwa afupishe mengine,ili ajikite kwenye main body. Shukrani alishatuomba siku anatua bongo.
 
Kasema hawezi kuzindua ilani wakati wagombea wote wamekatwa nani ataenda kuitetea iyo ilani kwenye vijiji kata au Majimbo by the way nimemuelewa.
Kwa hiyo anajitoa kwenye uchaguzi au ndio tusubiri fujo, maana kwa maeneo hayo ni sifa yenu kuu baada ya filamu zingine kushindwa??
Naona alikuwa anataka "gari" lake ili aka act hizo movie zao
 
Kweli dada? Mbona sisi tuliopo nnje twaambiwa Tanzania kama Ulaya!?
Ajira milioni 6 zimetengenezwa.
Wakulima wametajirika kwa kupatiwa pembejeo kwa wakati na za kutosha kulikopelekea kuzalisha kwa wingi na kuuza kwa bei nzuri kwenye masoko yaliyotafutwa na serikali.
Maslahi ya wafanyakazi yameboreshwa ndio maana utendaji kazi na nidhamu vimeongezeka.
Mkuu Victoire ,hayo yako umeyatoa wapi?
Hizo ni danganya toto hauoni wakionyesha picha wanaonyesha za Dar tu pale mijini. Waambie wakuonyese za Katavi,Mtama,Magu,Kondoa ndo utajua Tanzania ni kama Ulaya ama la.
 
Presidential material yupoje? Maana wabongo aisee mnafurahisha sana kwa kujifanya mnayajua material. Tangu mjue material ya kutengenezea batiki basi imekua nongwa.

Kwa hiyo Presidential material ni yule ambaye anaagiza wakurugenzi kufuta wagombea, kuwateka, kuwabambikiza kesi ili wakose vigezo n.k?

Usijibishane na wapumbavu mkuu, unapoteza muda wako bure.
 
Campaign is a MARATHON and not a SPRINT VIctoire, We still have 2 months to go before the end game provided that those figisu figisu wanazofanyiwa Chadema na ACT are eliminated otherwise expect and prepare for the worse election that we have seen in our lifetime and there is a possibility so many Tanzanians in Mainland and Island will lose their lives.
So if u have 2 month towards election on 28/10/2020 , hence U have time to make an appeal on those names of saccoss aspirants , whose names were eliminated from the list of would be contestants of this year election due to various reasons and Kishoa ? Also she has time to request NEC to deal with her request on Mwigula Nchemna issue rather than resorting to violence acts
 
Yaani saa nzima kaongea kuhusu kupigwa kwake risasi,waliokosea kujaza form wakaenguliwa na kupitisha bakuli la kuomba michango,kutoa number ya kuomba michango.
Siyo tuliyosubiria siku kuu kabisa ya ufunguzi wa kampein.
kwa kifupi aliongea pumba tupu.

Hayo aliyoongea hayakuwa ya kufungulia kampeini, na mengi alishayaongea mara nyingi sana kila alipokuwa akipata nafasi na huko kwenye mikutano yake ya hadhara ya kutafuta wadhamini maana ni yeye tu aliyetafuta wadhamaini kwa mikutano ya hadhara kinyume cha sheria; kulikuwa hakuna haja ya kuyarudia tena. Ameonyesha kuwa kampeini yake iko driven na grievances zake binafsi kupigwa risasi, siyo driven na grievances na interests za watanzania.

Nakubaliana naye kitu kimoja tu, kuwa mtanzania anatakiwa aishi bila hofu ya kushambuliwa na kupigwa risasi kama alivyofanyiwa yeye, lakini uchaguzi wa rais siyo malipo ya pole ya kupigwa risasi
 
Basi wewe ni muongo, hujasikiliza mwanzo mwisho. Mbona mwanzoni alisema kabisa kuwa hatazindua kwa hotuba kwa sababu ya uhuni tume uliyofanya?
Lakini hela za kuchangiwa kwa uchaguzi anaofanyiwa uhuni na NEC aliomba?? Kwa wananchi
Za nini ??? Je akijitoa kwenye uchaguzi atazirudisha au atazipeleka wapi ???
 
Amesema,atasema siku nyingiene na siyo kwenye vurugu mshenzi ya leo.
Lakini hela za kuchangiwa anao muda wa Kuziomba na Gari lake lilopigwa risasi anao muda wa kuliomba au kulitaka ktk "vurugu mshenzi ya leo "
 
Back
Top Bottom