Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Mwandishi,hili bandiko lako umeanza kuniangusha sasa,nikuulize swali la kizushi,hivi jamaa akikutokea,siku ya kwanza tu anakuahidi ntakupa au mnaanza kwanza urafiki,polepole ndo utamjua utafaidikaje?
Kwako lady victoire[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mwandishi,hili bandiko lako umeanza kuniangusha sasa,nikuulize swali la kizushi,hivi jamaa akikutokea,siku ya kwanza tu anakuahidi ntakupa au mnaanza kwanza urafiki,polepole ndo utamjua utafaidikaje?
Kwako lady victoire[emoji2][emoji2][emoji2]
Dalili ya mvua ni mawingu. Jana ilikuwa ni siku muhimu sana aongee kama Rais yeye atafanya nini ?
 
Kwa Hiyo "presidential material" Ni yule anayefanya kazi ya kubambikizia kesi raia wasio na hatia, kuteka, kuua, kuiba kura, nk??
 
Kama matatizo yalishaisha,la yupo kwenye stuation nzuri why asinipe pesa ?Tunaishi muda uliopo and hoping for the future. The past has already gone,why living the past ?While we know what has passed has passed.
Tundu Lissu kapona ila kuna wengine hawajapona. Na siku zote jitu uuaji huwa haliachi litaendelea kuua tu watu maana linaona ndio suluhisho la kunyamazisha watu.

Suala la kuagiza watu wachukue mabunduki ya kivita kwenda kumchakaza mtu risasi 36 huku akiwa bado yuko kitandani kwa operations 24 unatumia dola yote kupambana naye ni zaidi ya ukatili wa chatu lenye njaa.

Tena binafsi ningekuwa mimi ningependekeza sera ya mwaka huu iwe ni UBINADAMU NA UTU.

Hatuko salama kabisa, we're brutally caged .

Huwezi kuzungumzia maendeleo wakati unaishi na Joka ndani linalouma familia yako kila siku

Wala sishangai ni watu wachache sana ambao ni waumini wa UTU.

Kuna wengine ilimradi yeye yuko shwari HAJALI.

Unasema tunaishi mara moja na wakati huo you're not advocating for right to life.

What a self serving woman
 
Amechemka sana tu,sasa mnajidai eti 24 pages hahaaaa for what?
Mlikua mnamponda Baba wa watu eti hajui kuongea,huko kwenu upepo vipi?
 
Haraka ya nini wewe mwanamke!.
 
Hakuna uchaguzi in saccos voice
 
Hayo material yanatengenezwa kiwanda gani?.,au yanachimbwa mgodi gani?.Nikwambie tu kua acha kudanganya aise.Kwenye nchi hii mtu yoyote anaweza kua rais kama atakidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye katiba,kama wewe huwezi ilo ni tatizo lako binafsi.Vinginevyo niambie ni wapi hayo material yameandikwa.Na je kati ya wagombea waliopo unadhani nani ana ayo material ili tujue sasa endapo atashinda yeye nchi itakua tofauti na ilivyo sasa.Navile vile kwa ujinga na umaskini uliokithiri nchi hii unawezaje kuibeza nguvu ya jumuia ya kimataifa.Nchi haina mfumo wowote ule wakijitegemea alafu unaleta kiburi chakuzarau nchi zinazokusaidia.Acha kujitoa ufahamu.
 
Tundu lissu bado hajatoa sera zake lakini nakwambia atakua na sera nzuri kuliko Jpm na chama chake.Kwasababu yeye ndo anataka kuingia kwahiyo anajua ni mapungufu gani yaliyopo ambayo yameshindwa kufanywa na aliyekuwepo.Ccm na jpm walishatoa sera zao 2015 na wakapata nafasi yakuongoza na yako mambo waliyoyahaidi hawakufanya kwahiyo sasa hivi hawana jipya,watakachokuja nacho ni Kutubadilishia tu KAULI MBIU nakubadilisha badilisha tu maneno kwa porojo nyingi.
 
Ya saccos ni ya saccos na ya waigizaji wazalendo ni ya waagizaji wazalendo.
By the way ktk hii movement umewashirikisha Vyama vingine?? Maana waliwaomba muweke mgombea moja mkawapuuza, sasa mnawaona ni asset na sio liability
 
Mimi nime sikia Kuna maandamano ya Aman na uliza yasha Anza uko ulipo??
 
Wewe utafungwa na CDM!..shauri zako nani kakuambia hiyo ndio Sera yao?!
 
Yeah it is very true.
Jana alipuyanga sana,kuna Mambo anapaswa aongee Mbunge na kuna mambo anapaswa aongee mtu anayetaka kuwa rais wa nchi!

Yeye kutwa kurudia yale yale mpaka tunaogopa sasa km akipewa Nchi kazi yake itakuwa Kulipa kisasa mchana na usiku kucha!!!
 
Ma UVCCM mnajifanyaga mna akili lakini ukweli ni kwamba kichwani mwenu mmebebelea makamasi badala ya ubongo. Ina maana hukumsikia Lissu akisema kwa nini hatatoa hotuba yake ya uzinduzi kama alivyokuwa ameandaa?
Hii sio Mara ya kwanza kwa mgombea wa Cdm kufanya hivyo...
Ilitokea ht kwa EL, mwisho wa siku tuliambiwa Sera tuifuate mtandaoni.
 
Slaa was a great value kwa chadema
 
Ninyi watu ni waajabu sana, watu wakijaa mnasema wamekuja kumshangaa....wasipojaa mnasema wamepuuza....sasa waweje?[emoji3][emoji3]
Na wakijaa Wanasema sio wote watakaopiga Kura hasa ikiwa upande wa Upinzani. Ila wakijaa upande wa Chama Tawala, wote watapiga Kura na ushindi utategemea uwingi wa watu. Tunayumbayumba kwenye kauli zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…