Kama kesho utaongelea unachopanga kukifanya iwapo utafanikiwa kuwa Raisi wa nchi hii licha ya ukweli kuwa hatuna tume huru ya uchaguzi,nakushauri wewe kama mgombea uraisi(iwapo chama chako kitakuteua kuwa mgombea wao) uwe na ahadi zako kama mgombea uraisi na hizi nitazotaja hapa chini ziwe ni sehemu ya ahadi zako kama mgombea wa uraisi endapo hazitakuwa katika ilani ya uchaguzi ya chama chako.
1.Kutoa kifuta machozi kwa waliofukuzwa kwa vyeti feki
Nakushauri utambue mchango wa watu hawa katika Taifa hili kwani ingawa walifanya makosa, ila makosa yao hayawezi kulingana na ya mafisadi kama wa EPA,wahujumu uchumi na wengineo ambao ama wanalindwa au kusamehewa baada ya kurudisha walichotuibia.
Si hivyo tu,wako hata wanasiasa wanaotuhumiwa kufoji vyeti lakini hakuna uhakiki wa vyeti uliofanywa kuwahusu wanasiasa.
Hata katika majeshi yetu, sijui kama zoezi la uhakiki lilifanyika. Kwakuwa kasoro hizi zilizoondoa uhalali wa zoezi zima,ni bora hata waliokuwa watumishi wa umma na wakafukuzwa kwa kuwa na vyeti feki wakalipwa walau kifuta machozi ili kuwapoza na hii doublestandard na kuwashukuru kwa mchango wao kwa taifa hili japo una kasoro.
2.Njoo na ahadi ya kulipa malimbikizo ya salary increment za watumishi wa umma
Wote tunajua kuwa salary increment ya kila mwaka kwa watumishi wa umma ni jambo liliko katika taratibu za watumishi wa umma ila awamu hii limepuuzwa kwa kiwango kikubwa mno hivyo ni bora wewe na chama chako mkaja na mkakati wa kuwalipa watumishi malimbikizo yao yote kwa awamu au vyovyote mtakavyoona inafaa.
3.Njoo na ahadi ya kuondoa makato ya asilima 15 ya mshahara kwa wafaidika wa Bodi ya Mikopo
kamanda Lissu na CHADEMA kama chama,hakuna jambo baya na la kuumiza watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi kama hili kuongeza makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asilima 8 mpaka 15 ikiwa ni ongezeko la karibu asilimia 50 huku mishahara ikiwa ni ile ile kwa miaka mitano kwa watumishi wa umma.
Nakumbuka hata CAG alikemea jambo hili ila si Bunge wala serikali walinyesha kuguswa na jambo hili hivyo tunaomba wewe na chama chako jambo hili liwe ni moja ya kipaumbele chenu kwa kupunguza kiwango hicho mpaka kufikia kile cha zamani au chini ya hapo na ikiwezekana mje na mpango na mkakati wa muda mrefu wa kufuta kabisa deni hili kwa wanufaika wa mikopo hii.
4.Uej na mpango wa kufuta sheria itayotoa kinga kwa Raisi,Spika na Jaji Mkuu
Kwa aina ya Bunge tulilonalo,ni wazi muswaada husika utapita na kuwa sheria.Jambo hili ninahakika linawakera watanzania wengi hivyo nakushauri katika hotuba yako ya kesho uligusie kwa kulikmea na pia uahidi kufuta sheria ya aina hiyo iwapo utafanikiwa kuwa Raisi wa nchi hii japo mazingira ni magumu sana hili kutokea ila wee sema bila kujali uchaguzi utakuwaje.
5.Ongelea kufufua mchakato wa kura ya maoni kukamilisha mchakato wa kupata katiba mpya
Hili sidhani kama mtakuwa mmeliacha katika ilani yenu ya uchaguzi ila bado napenda kuwakumbusha tunahitaji katiba mpya na ile rasimu ifanyiwe marekebisha kadhaa kisha ipelekwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.Naomba sana hili liwe ni moja ya agenda zako hiyo kesho na ninahakika utagusa watanzania wengi sana kwani utawala huu umewafanya watanzania wajionee kwa macho yao ubovu wa katiba tuliyonayo na hatari yake.
6.Njoo na ahadi ya kulipa wakulima wa korosho na wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Nakuomba hiyo kesho kama hujapanga kuzungumzia issue ya wakulima wa korosho,basi ugusie swala hili na utoe ahadi ya kuwalipa wale ambao hawajalipwa mpaka leo.
Vile vile uwakumbuke wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwalipa haki zao kwa wale walio hai na kuwalipa wanafamilia kwa wale ambao tayari wametangulia mbele za haki.
7.Ongelea pia kuwalipa fidia wanaoitwa kangambo katika biashara ya zao la korosho
Hawa ni wale ambao korosho zao zilitaifishwa kwa kigezo kuwa walishindwa walishindwa kuonyesha mashamba huku wakiwa ni wadau wa zao hili la korosho.Kama kuna walioona watu hawa walikuwa wanawanyonya wakulima,basi tulitarajie kuwaona wao wakiwapa wakulima ruzuku au mikopo kuwawezsha kumudu kilimo cha zao hili la korosho na sio wema wa maneno matupu.
8.Njoo na ahadi ya kuanzisha mfuko maalumu wa kusambaza maji mijini na vijijni
Njoo na ahadi na mpango kabambe wewe na chama chako wa kuanzisha mfuko huu na fedha zote zitakazopatikana zitumike kusambaza maji mijini na vijijini.Ikibidi anzisheni tozo maalumu kutoka vyanzo vyovyote mtavyoona inafaa na fedha zitakazopatika ziende moja kwa moja kwenye mfuko huu.
9.Njoo na mpango wa kufuta sheria ya mitandao au kuifanyia marekebisha
Sheria hii inaumiza watu wengi hasa vijana na inatumika zaidi pale tu watu fulani wanapoguswa ila kwa wengine hata wakitukanwa hakuna kinachofanyika hivyo nakushauri uje na ahadi ya kuifuta sheria yote au kufuta vipengele katiki vya sheria hii na adhabu zake.
10.Ongelea kusudio la kuifanyia marekebisho sheria ya vyama vya siasa inayotishia uhai wa vyama vya siasa
Ongea yote hiyo kesho ila usisahau swala la kuifanyia marekebisho sheria hii inayompa mamla makubwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuweza hata kuingia mambo ya vyama vya siasa na hata kuweza kuvifuta kirahisirahisi tu.
11.Njoo na mpango mkakati wa kuiondoa serikali katika uendesha wa shirika la ndege nchini(ATCL)
Ili kuipusha serikali na mzigo wa kuendesha shirika hili,njoo na mpango mkakati wa kuiondoa serikali katika uendeshaji wa shirika hili kwa asilimia mia moja au uje na mpango wa shirika hili kuendedshwa na ubia na sekta binafsi.
Serikali teyari ina majukumu mengi na hivyo mzigo wa kuendesha hili shirika ni vizuri utazamwe upya kwa faida ya shirika lenyewe na Taifa kwa ujumla.
Hayo ni yangu mengine nawaachia wenyewe ingawa inawezekana haya niliyosema yote au baadhi tayari yako katika mipango yenu. Mimi nimongea in case kutakuwa na ambayo mtakuwa mmepitiwa au kuyasahau katika ilani yenu ya uchaguzi mkuu wa baadae mwaka huu ili myafanyie kazi.