Habari.
Inaelekea miaka miwili sasa tangu ndugu yetu na mwanasheria aliyesomeshwa kwa kodi za watanzania alipolitisha taifa kwamba kama likithubutu kubadili sheria na mikataba ya madini basi litakiona cha moto kwa kushitakiwa MIGA na kulipa mabilioni ya faini!.
Ikumbukwe sekeseke la kubadili sheria na mikataba yote ya kinyonyaji kwenye madini lilianzishwa na rais Magufuli baada ya kuona taifa halinufaiki chochote, wapinzani wakiongozwa na Lisu walipinga vikali hatua hii!!
Miaka miwili baada ya kubadili sheria na mikataba hatujashitakiwa MIGA kama tulivyoahidiwa na mwanasheria tuliyemsomesha kwa kodi zetu Lisu!! badala yake tumeanza kuona matunda ya kubadili sheria baada ya kuanzishwa masoko ya madini na hivi karibuni kuna mchimbaji mdogo huko Shinyanga ameuza almasi yake kwa zaidi ya billion 3!
Je kama tungesikiliza ushauri wa LISSU huyo mchimbaji mdogo angeipata wapi hiyo billioni 3?