Uchaguzi 2020 Lissu umati usikudanganye, wengi hawajajiandikisha

Halafu wewe utapata faida asipo pata urais,watanzania sijui hizi akili tunatoa wapi?.au utakuwa unaenda ikulu kunywa chai na Magufuli?
Sio kila mtu anaweza kuwa Rais, kuwa mwelewa. Lissu hata hadhi ya kuwa mwenyekiti wa saccos pale Ufipa hana, kwa jazba zile atamwongoza nani pale sauti ya zege?.
 
Lowassa alipigiwa mpaka deki katika barabara aliyokatiza kule Mwanza ulipo fikra siku ya uchaguzi akabaki akishangaa.

Watanzania ni sawa sawa na “wajumbe”, wanaweza kukukarimu mpaka ukajiona unaishi mawinguni.

Wengi wanaenda kuangalia kama ni kweli jamaa kapigwa Risasi 16 ,
 
Watu wote walio hai waliojiandikisha 2015 mwaka ambao ccm iliangukia pua watapiga kura tena mwaka huu , kwanza hata hujui mwaka huu waliojiandikisha ni wangapi .
 
Ahaaaa ahaaaa, eti Mange Kimambi, kwani Mange alikuwa hapa nchini, na alikuwa anagombea urais? JPM angekuwa karibu na wapiga kura watu wangetekwa, kuuwawa na kushambuliwa kwa risasi?
Tusiandikie mate wino upo tarehe 28 Oktoba.

Tutakuwa mashahidi wa hao wanaotekwa watakavyompa kura nyingi huyo mtekaji.

Huo utekaji upo Russia, Marekani, Congo, Argentina. Dunia nzima wateja ni wapo.
 
Wengi wanaenda kuangalia kama ni kweli jamaa kapigwa Risasi 16 ,
Wengine wanafanya mikutano ya siasa kama sehemu za kukutana na wachumba zao.

Wengine wezi wa simu wapo kazini.

Na wengi wao ni vijana mashabiki tu ambao hata vitambulisho vya kupiga kura hawana.
 
Kama umati ingekua kura basi mafuriko ya Lowassa yangempa urais. Kwa kawaida watu huwa wanajitokeza kwenye mikutano wakati mwingine kusikiliza kuna lipi jipya. Baada ya hapo kila mmoja anakwenda kuchagua kilicho moyoni. Kwa hali ilivyo, magufuli ana advantage kubwa sana ya kushinda kwa mbali sana, kwasbb kazi yake alioifanya kwa miaka 5 kila mmoja ameiona tofauti na Lissu ambae anaahidi vitu ambavyo ukivisikiliza kwa kina havitekelezeki.
 
Unaweza kutaja jambo MOJA tu miongoni mwa yale unayodai "ukisikiliza kwa kina havitekelezeki"?
 
Wavuvi tunamtoa macho lisu kasema anatulipa wahanga wote
Watu wa sekta ya madini wataziba Pengo la kura zenu, maisha yataendelea fresh tu.

Usisahau wale wenye vyeti original waliochukua nafasi ya wale wa vyeti vya stationary, hao pia wataziba Pengo lenu wapendwa wavuvi.
 
Umati wa watu hauwezi kwenda kumsikiliza mtu/ chama wasichokuwa na imani nacho na pia hao wa kusombwa na mikokoteni kwenda kuwaangalia wasanii na wanafunzi wanaofungiwa shule kupelekwa kujaza vichwa ndio wamejiandikisha?😁😂😂hauna hoja kabisa
 
Watu wa sekta ya madini wataziba Pengo la kura zenu, maisha yataendelea fresh tu.

Usisahau wale wenye vyeti original waliochukua nafasi ya wale wa vyeti vya stationary, hao pia wataziba Pengo lenu wapendwa wavuvi.
Uliwaona wangapi unajuwa wavuvi niwangapi nchini tumeungana na vyeti feki+bomoa bomoa mwaka huu sijui mnatokea wapi ni yeye 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…