PreGE2025 Lissu unatangaza Uasi kisha unakana Mahakamani ulikuwa unategemea vyombo vya Usalama vitakaa kimya?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
57,035
Reaction score
46,479
Wanaukumbi.

Unajua kwanini hakuna any Diplomatic Mission kuanzia embassy au Consulate imetoka kusema chochote kuhusu issue ya Lissu,, sababu ni kwamba “kauli zake ni kweli zina viashiria vya ujinai na si siasa pekee..

Lissu unatangaza Uasi kisha unakana Mahakamani ulikiwa unategemea vyombo vya Usalama vitakaa kimya..

Huwezi sema utafanya uasi, kukinukisha na maneno mengine ya namna hiyo katika mazingira tuliyonayo kisiasa na kiusalama halafu vyombo vyetu vya ulinzi vikuchekee tu, ukicheka na nyani unavuna mabua.

Your browser is not able to display this video.
Uasi ni nini, civil disobedience ni nini na uanamapinduzi ni nini?

Ukiwa na serikali dhalimu unaruhusiwa kuiasi au huruhusiwi?

This is not merely a legal matter, there is an ethical matter here, do you know the difference?
 
Unajua Sheria wewe chawa?
 
Mpigania uhuru husimamia kile anachokisema

Lisu tapeli na wanaomsikiliza akili hawana

Fikiria anasema ataamusha uasi akihutubia akifika mahakamani akiulizwa anasema sikusema mimi.Anakana.

Hivi kuna mwanasiasa hapo?

Mwanasiasa wa kweli husimamia alichokisema.Lisu hamna Chadema utasikia huyo ndio Mandela wetu.Mandela alisimamia alichotamka nje na mahakamani akasimama nacho.

Lisu anachosema nje akiwekwa mahakamani anakana Mandela koko huyo
 
Asante nabii mtume Ritz.
JF tududumtu tumo twingi jamani.
 
na hiyo ndiyo hasara ya kukosa hekima na kuropoka ropoka bila mpangilio na kusahau kwamba nchi hii inaongozwa kwa misingi ya kisheria bila kujali kudeka kwako kwakua utimamu wa mwili wako uko kama ulivyo.

Kila mtu afuate sheria bila kujali hali yake.
Na huo ndio ustaarabu 🐒
 
Hata ofsi zote za ubalozi zihamie Mahakamani Kisutu bado hazitasaida kitu. Taratibu zote za kumkamata Lissu zimefuatwa, na amepelkwa Mahakamani ndani ya muda unaotakiwa kisheria. Haki ya kutoa maelezo mbele ya wakili amepata. Na yuko mikono salama huko Segerea akisubiri tarehe ya kutajwa tena.

Wakati wa uchaguzi niliwaambia kuwa Lissu ni MROPOKAJI asiye na busara, siyo mtu anayepaswa kuwa na maamuzi ya mwisho kwenye taasisi yeyote. Lissu ni wa kutumwa tu. Mtamkumbjuka Freeman Mbowe
 
Tutamkumbuka vipi Freeman wakati nae alikamatwa kwa kupanga ugaidi na akawekwa gerezani zaidi miezi 8?.
 
Tafuta taarifa ya wapinzani waliopata urais nchi za Afrika na changamoto walizopitia. Ukichukua risasi 16 na anayotembea nayo na hii kesi ya uhaini sasa nadhani na yeye kakidhi vigezo. Siku zinahesabika za kuingia Mahali Patakatifu.
 
Wapi alisema kwenye matamshi yake kuwa ataamsha uasi?
Unajua hii kesi ni rahisi sana sababu nyie wenyewe mnajichanganya. Mwishow mshindwe ku prove mahakamani na dpp afute kesi kama kawaida
 
Uasi ni nini, civil disobedience ni nini na uanamapinduzi ni nini?

Ukiwa na serikali dhalimu unaruhusiwa kuiasi au huruhusiwi?

This is not merely a legal matter, there is an ethical matter here, do you know the difference?
 
Uasi ni nini, civil disobedience ni nini na uanamapinduzi ni nini?

Ukiwa na serikali dhalimu unaruhusiwa kuiasi au huruhusiwi?

This is not merely a legal matter, there is an ethical matter here, do you know the difference?
Msiklize Lissu. Anavyoelezea uasi.
 

Attachments

  • twidown-video.mov
    18.1 MB
Na ndio sababu “hakutekwa” alikamatwa kwa taratibu zote za kisheria na kupandishwa kizimbani kwa taratibu na muda ule ule wa kisheria na kwa sasa watu wote timamu wanaacha michakato ya kimahakama iendelee.
Mkuu Ritz unapopigania haki za watu usichague watu wa aina gani. Hizi mahakama za hapa bongo sio mahakama ambazo unategemea zitatoa haki kwa mnyonge dhidi ya watawala, ambao ma jaji wanapigiwa simu kuamrishwa nini Cha kufanya. Pia nakumbuka kada Mwenzio Rostam alizibagaza mahakama za Tanzania juu ya utoaji haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…