Lissu Vs Zitto: Nani mkali wa kujenga hoja za kisiasa?

Watu wanashindwa kutofautisha mambo,yani wao mtu akiwa anaongea yale wanayotaka kuyasikia ndio huona ni mjengaji hoja mzuri kumbe tofauti.
 
Umesomeka, all the way from Tandahimba
 
kwanza mdahalo wa Lissu na Magufuli na mdahalo wa Maalim Seif na Mwinyi alafu tuendelee kuanzia hapo.
 
ila kwa zama hizi TL ndio kiboko pekee wa Jiwe...anampa makavu hadi anapanic
 
Mgombea wetu kazi zake zinamuuza
Kuwageuza Watz masikini kuliko alivyowakuta? Udikteta uchwara? Kuteketeza pesa za walipa kodi kwa biashara kichaa ya ndege - muulize faida anayopata kama hatarkuruka kimanga? Matumizi mabaya ya madaraka aliyopewa na katiba - uanzishaji wa miradi ya miundombinu sio jambo baya, ubaya ni kutofuata utaratibu ambao umewekwa na hii hii katiba yetu mbovu lakini aliapa kuifuata. Akiambiwa basi turejee mazungumzo ya Rasimu ya Warioba, anasema yeye hakuahidi mambo ya katiba. Mataga yakisema tubadilishe katiba atawale milele, anapiga tabasamu utafikiri ndio kwanza ametoka Bujumbura.
 
Haapo Messi Vs Ronaldo sema mmoja jazba nyingi, akumbushwe theory of "communication skills" hasa segment ya Oral presentation
 
Binafsi zito kabwe naona kuwa ni mzuri zaidi wa hoja.anauwezo wa kutoa hoja na kujenga hoja katika kila idara ama sehemu na ikawa nzito kweli.

Yaani anafiti kotekote.

Na lissu nae naona yuko vizuri hasa kwenye mambo ya sheria,mbali na sheria naona kama kwenye mambo mengine hafiti kiivyo
 
Wote wawili ni matapeli wa kisiasa tu hawana hoja hata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…