sonofobia
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 1,171
- 4,295
Lissu ameendelea kurusha jiwe gizani.
Safari hii ameikemea rushwa wazi wazi hata iliyo ndani ya chama chake CHADEMA. Lissu hajapepesa macho wala kuangalia sura ya mramba asali.
Wataalam wa mambo ya siasa za kusini mwa jangwa la sahara wanasema huu ni muendelezo wa kukosoa tuhuma za rushwa na wizi wa kura uliofanyika kwenye chama chake.
=======
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amewataka Watanzania kutowakubali Viongozi wanaotoa au kupokea rushwa kwakuwa hawafai, bila kujali Watu hao ni wa Chama kipi au Dini ipi.
Akiongea akiwa Itigi Mkoani Singida leo June 17,2024, Lissu amesema “Watu wanaotoa rushwa na kupokea rushwa hawafai kwenye Uongozi, wawe CCM, wawe CHADEMA wawe Dini yoyote, hawafai kwasababu akipokea au kutoa rushwa atakuuza tu, msikubali Watu wasiokuwa wa haki”
"Watu wa haki, watu wasio kula rushwa, wasiotoa rushwa, wanaotoa rushwa hawafai, wawe CCM, Wawe CHADEMA, wawe dini yoyote, watoa rushwa na wapokea rushwa hawafai kwenye uongozi kwa sababu akitoa rushwa au akipokea rushwa atakuuza tu, atakuuza tu, usikubabali watu wasiokuwa wa haki, usikubali CCM."
Pia soma: Tundu Lissu: Rushwa za CCM kujaribu kuibomoa CHADEMA ni nyingi mno