Pre GE2025 Lissu: Wala rushwa au wapokea rushwa hawafai kua viongozi, wawe CCM au CHADEMA, watauza nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ataach
Ataachaje mwenzio unataka afe njaa!? πŸ˜‚ yupo kazini hapo
 
Ufisadi upingwe na kila mtu
 
Lissu ndio kasema kuna rushwa ya kutisha ndani ya Chadema, mimi nausikaje kwenye ujambazi wa Chadema mkuu?
 
Ta
Tatizo lako, unabadilika badilika sana, tena bila kutegemea!
kama kinyonga eti?🀣

halafu wew unaskia uchungu na kuumizwa kwa uhuru na haki ya maoni ya engine πŸ’
 
Hivi mlimuona wapi Mchaga mpigania haki, wachaga ni wapigania hela. akienda huko ni kwa malengo maalum
 
Huyu Mwamba Mungu amuweke sana
 
Asisahau pia kuueleza umma nini CHADEMA watafanya wakipewa mamlaka mbali na kutuonyesha maovu ya CCM pekee.
Hili liko wazi....kwamba Chadema hawawezi kule Wala Rushwa.....sasa unataka waseme nini ambacho huelewi
 
Huyu Lisu ni mtu wa namna gani? Natamani aweke bayana anahitaji nini? Na akipata nafasi ataifanyia nini nchi hii labda kwasababu uwasilishaji wake wa kukera umenifanya nisiwe mfuatiliaji mzuri wa mawasilisho yake hasa pale anapo weka mbele kutukana kila mtu na kuona yeye pekee ana akili kubwa.
Hatahivyo bado nina hamu ya kumpata kiongozi jasiri iwe kutoka chama chochote ambaye ataboresha kidogo kutoka kwa Tundu Lisu na kuchanganya hitikadi za Mandele,Nyerere,Magufuli,Makonda,jaji Chipeta,Jaji Mwalusanya,Gaddafi. Kwa uchache niliowataja wana vitu vizuri na vibaya lakini tuchukue mazuri yao na kusimamia utekelezaji kwa kuweka yale mazuri kuwa dira ya Taifa. Mfano Mchungaji Mtikila alikuwa anaongea mambo mazito ambayo pia yalihitaji watu sahihi wa kuyasimamia japo kuwa naye uwasilishaji wake ulikuwa kama wa huyu jamaa. Matatizo yaliyomkuta Tundu na Mtikila inawezekana yanatokana na kufanya uwasilishaji wa kukera na kuudhi ingawa katika hoja hizohizo angeweza kufikisha ujumbe kuntu bila kuleta athari kwao.
Nchi hii ni kweli tunahitaji Haki tulipo tawaliwa na wakoloni Haki ya Mwafrika na wengine wachache ilipotezwa tunalojukumu kubwa kuirejesha Haki kwa upana wake mbaya zaidi hawa jamaa walipandikiza kitu ambacho ukandamizaji wa haki umerithiwa na Sisi kwa sisi.Ubinafsi,wizi na uroho,dhuluma na upendeleo ni watoto wa baba mmoja na uvunjifu wa haki hapa ni lazima wawepo watu ambao wanaweza kujitoa na kupambana na jinamizi hilo ambalo ukikosea lazima ile kwako.Kujituma katika kazi zenye kuleta tija ndiyo mzizi wa fitina lakini ni lazima tupate viongozi wenye nia thabiti pamoja na kwamba nimemtaja Makonda miongoni mwa wanaotakiwa kuchukuliwa maarifa yao lakini sikubaliani na namna anavyofanya kwa kukashifu au kutweza watu kinyume na ile kanuni yangu ya kwanza ya kutunza na kuhifadhi Haki nafikiri nijambo jema kama kungekuwa na check and balance yeye alitakiwa kusimamia viongozi wote wasiotimiza wajibu wao na kupelekea hali kuwa mbaya ya uvunjifu wa Haki ili akina Makonda wawe kila mtaa,kitongoji,Kijiji,kata Tarafa,Wilaya,Mkoa na Taifa kwaujumla.
Mahakama ndiyo chanzo cha kupoka Haki sijui ni kwasababu hawajui majukumu yao au umungu mtu umewatawala au inawezekana kunasababu iliyojificha ingawa wapo wachache angalau wanajaribu kufanya vizuri lakini wengi wao wanaofanya ule msemo wa samaki mmoja akioza wote wameoza hawa pia wanatakiwa kuwekewa tochi kubwa ya kufuatilia vituko wanavyovifanya na maamuzi yao ya kutatanisha yawekwe hadharani ili wananchi waweze kuwajadili na kuwapa ushauri labda wataona aibu.
Kuna watu wazuri wapo katika vyama vya Siasa lakini pia wabaya wapo kinachotakiwa ni uwezo wa kuwabaini na kuwapa wanachostahili.
 
Asisahau pia kuueleza umma nini CHADEMA watafanya wakipewa mamlaka mbali na kutuonyesha maovu ya CCM pekee.
SAWA Kabisa, lakini ajenda ya kuiondoa CCM kwa maovu inayoyatendea taifa letu ni ajenda tosha kabisa, hata bila kuingia ndani kuhusu wanayotarajia kuyafanya CHADEMA.
Kwa mfano: Kukomesha rushwa - kama CHADEMA wataweza kufanya hivyo, hiyo ni ajenda yao tayari. Hali ni hiyo hiyo, hata kwa hayo mengine.
 
Umejuaje "uchungu na kuumizwa". Unacho kifaa cha kuyapima haya?
unavyo tukana tu, inaonyesha una maumivi makali mno moyoni na akilini, ukiona mtu ana maoni na mtazamo tofauti na yako πŸ’
 
unavyo tukana tu, inaonyesha una maumivi makali mno moyoni na akilini, ukiona mtu ana maoni na mtazamo tofauti na yako πŸ’
Kumbe. Hicho ndiyo kipimio chako?
Basi, kumbe ninayokupasha yanakuingia vizuri akilini mwako. Chukuwa muda kuyatafakari, kuna siku utaona ukweli wake ulipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…