Lissu: Walisema arudi tutafanya uchunguzi, nimerudi nasubiri niitwe

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Lissu ameyasema hayo kwenye kipindi cha Clouds 360 alipoulizwa mpango wa kulianzisha kuhusu kesi yake maana sasa yuko nchini ambapo alisema;

Jeshi la Polisi ndio wenye mamlaka ya kuchuguza, wenye majalada kuhusu tukio hilo na wenye wataalamu wanaojua silaha illiyotumika hivyo wao ndio wa kufufua kesi hiyo.

Akiongeza kuwa walisema wanasubiri arudi, sasa amerudi anawasubiri wamuite na kwamba asipoitwa hawezi kulazimisha kama hawataki, japo anajua kama hawataki kwaiyo hata wasipomuita hatoshangaa kwasababu wanajua hasa kilichotokea, nani aliyefanya, alifanya kwa nini na nani aliyetoa amri hiyo.

Je na dereva wake karudi?[emoji23],au mbwembwe tu
 
Hapo tena amewatega polisi,huku wanapigwa na Mama ubambikaji kesi za madawa huku Lissu anawachapa tena,sijui watashika wapi?
Matawi yote yanakwanyuka kila nyani wakiruka🤔
 
Hapo tena amewatega polisi,huku wanapigwa na Mama ubambikaji kesi za madawa huku Lissu anawachapa tena,sijui watashika wapi?
Hapo msosi moto,mboga za moto na kinywaji kinafuka mvuke. Zamu ya polis kunyolewa
 
Lissu ameyasema hayo kwenye kipindi cha Clouds 360 alipoulizwa mpango wa kulianzisha kuhusu kesi yake maana sasa yuko nchini ambapo alisema;

Jeshi la Polisi ndio wenye mamlaka ya kuchuguza, wenye majalada kuhusu tukio hilo na wenye wataalamu wanaojua silaha illiyotumika hivyo wao ndio wa kufufua kesi hiyo.

Akiongeza kuwa walisema wanasubiri arudi, sasa amerudi anawasubiri wamuite na kwamba asipoitwa hawezi kulazimisha kama hawataki, japo anajua kama hawataki kwaiyo hata wasipomuita hatoshangaa kwasababu wanajua hasa kilichotokea, nani aliyefanya, alifanya kwa nini na nani aliyetoa amri hiyo.

View attachment 2504813
Tukio limekwisha eksipaya muda wake.
 
Back
Top Bottom