Ndekrepha
JF-Expert Member
- Jun 4, 2020
- 1,506
- 2,660
Ndio hoja ya Lissu,kwamba sio kuwa watanzania ni wajinga bali mfumo ndio unawakwamisha!Ndio maana iko hoja hapa ya kufumua mfumo wa Elimu hasa kwenye lugha ya kufundishia ieleweke tunataka kipi,sio kuwa nusu nusu au katikati!Yaani kiswahili tunakitaka na kiingereza tunakitaka!Mwisho wa siku ni watoto wa masikini tu ndio wanaohangaika,watoto wa wakubwa wako shule ambazo lugha ya kufundishia ni moja na wanafundishwa mpaka kuielewa!
Mimi naona kiswahili kwasababu ni lugha tunayozaliwa na kuijua mtaani,basi kibaki kama somo na kiingereza kiwe lugha ya kufundishia!
Mkuu, kwenye swala la ubora wa elimu na mfumo mzima wa elimu nakubali ni mbovu unatakiwa kubadiliswa. Ubora wa elimu haupimwi kwa lugha inayotumika kujifunzia na kufundishia, bali unapimwa kwa mtaala. Sasa mfumo ukishabadilishwa automatically kutakuwa hakuna kukariri tena na hiyo lugha haiwezi kuwa changamoto maana zitatumika mbinu za kufundishia na kujifunzia ambazo zitamjenga mwanafunzi kuelewa zaidi na kuwa na basic life skills.