Mkuu shule nilizopita ni Mazengo,tukahamishwa baada ya kugeuzwa kuwa st John university,nikaenda Moshi tech,nikaenda kibaha high school na baadaye UDSM!Huko kote nilikopita hakukuwa na hayo masuala ya vibao wala speak English!Kidogo nilikuta msisitizo Kibaha!
Mkuu ukiona asilimia 90 ya wanafunzi wanaopita Kayumba wanamaliza vyuo na kiingereza kibovu au kisichoridhisha,jua kuna tatizo!
Hao akina Lissu ni kati ya wachache walioweka pengine jitihada za ziada,pia masomo yake ya sheria yakamsaidia maana kuna kujieleza kwingi na case zinakuwa kwa lugha ya kiiingereza!Hiyo inawapa advantage wanasheria ya kujifunza kiingereza kwa lazima!Mchepuo kama wa uhandisi ni majanga,huko kiingereza ni technical language ya field husika na unafaulu vizuri tu!Upewe mike ujieleze hata dakika 10,majanga!
Bado narudia,medium schools zinafanikiwa sana,hata ambao tumesoma nao unaona kabisa huyu katoka sehemu fulani tofauti na mimi japo kufaulu mnafaulu wote lakini yeue anakuwa na kitu cha ziada,lugha!
Tunaweza kukawa na tatizo kwenye mitaala,lakini hili la lugha pia halikwepeki!
Mimi napendekeza kiingereza kama lugha ya kufundishia ianzie msingi,japo tutakuwa na kazi kubwa ya kufanya maana hata walimu nao hali ni ile ile!Mfano kipindi cha Corona kuna utaratibu wa walimu kwa kushirikiana na Tv stationa walianzisha wa kufundisha kupitia luninga!Mmmh kuna siku nilijikuta naangalia ufundishaji,aisee nilijikuta aibu naona mimi nikabadili na channel!
Hoja ya Lissu ni ya msingi sana,chama kitakachochukua hatamu naomba waichukue na iwe kwenye agenda za elimu!Uanzishwe mdahalo utakaoshirikisha wadau wa elimu kwa kuzingatia na uzoefu kwa majirani zetu kama Kenya na Uganda tuamua tunashika njia ipi once up for all!
Hapa tulipo tumekwama,tusipuuze hoja hii!Tuichukue na ifanyiwe kazi tupate majibu