Ni nani huyo ambae ndo maana nimemuona anakijua?!Je, labda hata wewe haukijui kiingereza pia ndio maana unamuona anakijua?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni nani huyo ambae ndo maana nimemuona anakijua?!Je, labda hata wewe haukijui kiingereza pia ndio maana unamuona anakijua?
You are still suffering from "diploma disease". Some concepts have to be taken judicial notice of from daily experience and public checkability!Hahaha weka records hapa, intellect haisemwi na maneno, weka hapa chochote aidha thesis yake au publications, ...
Hatuendelei na kupata wasomi wakutuondolea matatizo yetu hadi tukubali kama kiswahili ni rahisi kufahamika kuliko lugha zengine.Tundu Lissu amesema haya kuhusu lugha ya kufundishia:
Ukiniuliza mimi, honest opinion Nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha, tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani language of instruction is everything.
Mimi ni Wakili, Majaji wengi hawajui kiingereza, ukienda Nchi za wenzetu huko Mtanzania akiongea unatamani kuingia uvunguni mwa meza, Kiingereza chetu ni kibaya, sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha.
Tangu tumepata Uhuru tumekua na ndimi mbili kuhusiana na lugha na ndimi mbili ni hatari, ulimi mmoja tumesema Kiswahili ni lugha ya Taifa na tumeiendeleza kwelikweli, ulimi wa pili tumesema Kiswahili si lugha ya kufundishia.
Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua Kiingereza? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka Kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu. We want to make Tanzania great nation, Kiswahili ni ajenda kuu.
Usimsahau huyu bwana anaongoza.Mpaka sasa list yangu ya wenye PhD wasiojua kingreza inasoma 2 na naendelea kufanya utafiti kuwabaini PhD holders wengine lugha gongana.
Lisu yupo sawaaaaah kabisaaaTundu Lissu amesema haya kuhusu lugha ya kufundishia:
Ukiniuliza mimi, honest opinion Nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha, tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani language of instruction is everything.
Mimi ni Wakili, Majaji wengi hawajui kiingereza, ukienda Nchi za wenzetu huko Mtanzania akiongea unatamani kuingia uvunguni mwa meza, Kiingereza chetu ni kibaya, sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha.
Tangu tumepata Uhuru tumekua na ndimi mbili kuhusiana na lugha na ndimi mbili ni hatari, ulimi mmoja tumesema Kiswahili ni lugha ya Taifa na tumeiendeleza kwelikweli, ulimi wa pili tumesema Kiswahili si lugha ya kufundishia.
Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.
Ukisema ni juhudi unazungumzia st. Kayumba bila shaka. Na kuna watu watakushangaa...Nimekwambia kiingereza ni juhudi ya MTU binafsi,siyo lazima majaji wakijue vizuri kuliko MTU mwingine.
Wanatumia lugha zao kufanyia nini mkuu?Kati ya siku Lissu ameongea ujinga na utumbo ni leo, yaani lugha iwe kigezo cha kutopata maendeleo, hapana watanzania sio wajinga kiasi hicho, swali lakujiuliza kwa nini kumekuwa na taaluma ya Tafsiri na Ukarimani. Lissu jipange upya nchi kama urusi, uchina nchi za falme za kiarabu wanatumia lugha zao na wako vizuri kiuchumi.
Nimejisikia aibu sana,Usimsahau huyu bwana anaongoza.
Si yule anayesimamia watu kuelimika
[/QUOTE
95% Wait while the system is decoding your message................................................................
..................
100% decoding completed]
95% Wait while the system is decoding your message................................................................Nishawajua, yule bidada pamoja na yule stone
Mimi nilisoma kijijini huko kasulu japo si mzawa wa huko!Ila darasani wakati mwingine mwalimu alikuwa akiona watoto hawaelewi anapiga hadi kiha(lugha ya asili) ili watoto waelewe!Ambao nilikuwa nasoma nao,hata kuwasiliana kwa kiswahili ilikuwa ngumu!So hayo ya mtoto wa darasa la saba kutomudu kuandika insha inawezekana kulingana na mazingira!
Je,medium schools umeona watoto wa namna hiyo?Huko kuna kitu gani special mpaka isiwe hivyo?
Vyuoni huko ni aibu,nilimaliza degree Engineering hapo UDSM na GPA nzuri sana awamu ya Kikwete,baadaye nilipata fursa ya kusomeshwa masters Uholanzi bure na taasisi moja ya global education!Nilichotakiwa kufanya mtihani wa IELTS kwenye centre mojawapo ya british council!IELTS maana yake ni International English Language Testing System!Nikalipia 300,000 kama ada ya mtihani!Hapa unafanya mitihani 4,Speaking,Hearing,Writing na Reading!
So unapofanya wanakurate kati ya 1 mpaka 9,mimi nilipiga point 6.5 kama wastani!Chuo kilihitaji point 7 ili nidahiliwe!Nikasema haina shida,nikaenda kozi kujiongezea ufundi miezi 3 ili niwahi deadline ya chuo!Nikalipia tena laki 3 nikaingia kwenye test nikascore point zilezile 6.5!Ndoto zangu zikafia hapo!
Ninachosema kuna vitu basic ambavyo ukiwa mtoto ni rahisi kuvishika na vikakukaa!Nilikosa fursa kwa sababu ya lugha!Ningekuwa nimepita shule zenye msingi mzuri wa kiingereza kama hizi medium ningekuwa mbali sana!
So inapokuja hoja kama hii anayoisema Lissu,wengine ni wahanga na tunaielewa sana!Mkuu hii hoja imenihuzunisha sana na imenikumbusha mbali!
Kwani ili mtu ajue lugha kwa ufasaha inabidi ajifunze miaka mingapi? Kwani mtu hawezi kujifunza lugha peke yake akaielewa hadi iwe amejifunza wakati anasoma masomo mengine kama science katika lugha hiyo hiyo?Tundu Lissu amesema haya kuhusu lugha ya kufundishia:
Ukiniuliza mimi, honest opinion Nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha, tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani language of instruction is everything.
Mimi ni Wakili, Majaji wengi hawajui kiingereza, ukienda Nchi za wenzetu huko Mtanzania akiongea unatamani kuingia uvunguni mwa meza, Kiingereza chetu ni kibaya, sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha.
Tangu tumepata Uhuru tumekua na ndimi mbili kuhusiana na lugha na ndimi mbili ni hatari, ulimi mmoja tumesema Kiswahili ni lugha ya Taifa na tumeiendeleza kwelikweli, ulimi wa pili tumesema Kiswahili si lugha ya kufundishia.
Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.
Labda jiulize kwanini wakoloni walipotawala Tanganyika na Zanzibar, waliamua kujifunza kiswahili badala ya kutubadili tukazungumza kiengereza. Nadhani uwo ni mfano rahisi tuu utagundua kuna tofauti baina ya Kenya na Malawi au izo nchi zengine kama Nigeria, Kameroon n.k. Hizi nchi haziko katika lugha moja kuu, hivyo kuwabadili wakazungumza fr/en ni rahisi na inawezekana kwa urahisi.Kwani ili mtu ajue lugha kwa ufasaha inabidi ajifunze miaka mingapi? Kwani mtu hawezi kujifunza lugha peke yake akaielewa hadi iwe amejifunza wakati anasoma masomo mengine kama science katika lugha hiyo hiyo?
Hivi ukimchukua mmalawi aliyeishia darasa la nne au mkenya darasa la nane mbona wanajua kiingereza kwa ufasaha? Kuanzia form one hadi form six na chuo kikuu ni miaka isiyopungua 9 hadi 11 kwa wenye bachelor degree, je hiyo ni miaka michache ya kujifunza lugha? Hapo hujajumlisha miaka 7 ya primary na pengine miwili au mitatu ya chekechea ambapo mtu huyo alijifunza english.
Tatizo lenu kubwa mashabiki wa Lissu mnamuona kama msahafu yeye ndiye anajua kila kitu. Duniani mtu wa hivyo hayupo.
Ukitaka uwe vizuri katika hoja kwanza liendee jambo objectively sio subjectively. Pili jaribu kuutafuta ukweli nje ya boksi kwa kutumia knowledge yako hata kama ni ndogo huku ukiangalia facts mbalimbali zilizo mbele yako.
Mkuu shule nilizopita ni Mazengo,tukahamishwa baada ya kugeuzwa kuwa st John university,nikaenda Moshi tech,nikaenda kibaha high school na baadaye UDSM!Huko kote nilikopita hakukuwa na hayo masuala ya vibao wala speak English!Kidogo nilikuta msisitizo Kibaha!Kwanza pole sana kiongozi kwa kukosa huo ufadhili wa masomo, halafu hapa umeibua jambo jipya tena hapa kuhusu hilo la elimu huko Kasulu. Naona umekuja pale pale kwenye ukweli kuwa tatizo ni mtaala tu na sio lugha. Mwalimu anatumia lugha ya Kiha kufafanua zaidi kwa sababu mtaala haujatoa nafasi ya mwanafunzi kuweza kujifunza kwa kutafakari na kujihusisha na mazingira yake na wakati uliopo.
Halafu nitakuuliza kitu, shuleni sekondari kunakuwaga na midahalo ya kiingereza na vibao vile vya kuvaa shingoni kwa wanaoongea kiswahili shuleni. Sasa wakati unasoma sekondari vitu hivyo havikuwepo? Ulikuwa unachangamana vipi na watu? Je ulikuwa unaona umuhimu wa lugha ya kingereza? au kwako ilikuwa bora tu upate marks darasani? Je Lissu yeye kingereza alikifahamia wapi? kwenye shule hizi hizi na mifumo hii au alisomea mtaala wa nje ya nchi? Juhudi Juhudi Juhudi.. ndio ufunguo wa haya yote. Wako watoto wa Kayumba kibao tu na wanaongea hicho kingereza vizuri bila shida.
Mkuu shule nilizopita ni Mazengo,tukahamishwa baada ya kugeuzwa kuwa st John university,nikaenda Moshi tech,nikaenda kibaha high school na baadaye UDSM!Huko kote nilikopita hakukuwa na hayo masuala ya vibao wala speak English!Kidogo nilikuta msisitizo Kibaha!
Mkuu ukiona asilimia 90 ya wanafunzi wanaopita Kayumba wanamaliza vyuo na kiingereza kibovu au kisichoridhisha,jua kuna tatizo!
Hao akina Lissu ni kati ya wachache walioweka pengine jitihada za ziada,pia masomo yake ya sheria yakamsaidia maana kuna kujieleza kwingi na case zinakuwa kwa lugha ya kiiingereza!Hiyo inawapa advantage wanasheria ya kujifunza kiingereza kwa lazima!Mchepuo kama wa uhandisi ni majanga,huko kiingereza ni technical language ya field husika na unafaulu vizuri tu!Upewe mike ujieleze hata dakika 10,majanga!
Bado narudia,medium schools zinafanikiwa sana,hata ambao tumesoma nao unaona kabisa huyu katoka sehemu fulani tofauti na mimi japo kufaulu mnafaulu wote lakini yeue anakuwa na kitu cha ziada,lugha!
Tunaweza kukawa na tatizo kwenye mitaala,lakini hili la lugha pia halikwepeki!
Mimi napendekeza kiingereza kama lugha ya kufundishia ianzie msingi,japo tutakuwa na kazi kubwa ya kufanya maana hata walimu nao hali ni ile ile!Mfano kipindi cha Corona kuna utaratibu wa walimu kwa kushirikiana na Tv stationa walianzisha wa kufundisha kupitia luninga!Mmmh kuna siku nilijikuta naangalia ufundishaji,aisee nilijikuta aibu naona mimi nikabadili na channel!
Hoja ya Lissu ni ya msingi sana,chama kitakachochukua hatamu naomba waichukue na iwe kwenye agenda za elimu!Uanzishwe mdahalo utakaoshirikisha wadau wa elimu kwa kuzingatia na uzoefu kwa majirani zetu kama Kenya na Uganda tuamua tunashika njia ipi once up for all!
Hapa tulipo tumekwama,tusipuuze hoja hii!Tuichukue na ifanyiwe kazi tupate majibu
Nafikiri hoja yangu hujaielewa vizuri.Labda jiulize kwanini wakoloni walipotawala Tanganyika na Zanzibar, waliamua kujifunza kiswahili badala ya kutubadili tukazungumza kiengereza. Nadhani uwo ni mfano rahisi tuu utagundua kuna tofauti baina ya Kenya na Malawi au izo nchi zengine kama Nigeria, Kameroon n.k. Hizi nchi haziko katika lugha moja kuu, hivyo kuwabadili wakazungumza fr/en ni rahisi na inawezekana kwa urahisi...
Ukiona zaidi ya 90% wanakumbana na changamoto hiyo,basi jua kuna tatizo hasa la msingi linalohitaji utatuzi!Sasa wewe umesema huko Kasulu shuleni mwalimu anatumia Kiha ili kufafanua masoma yanayotolewa kwa kiswahili. Kiswahili hiki ambacho ndio lugha ya Taifa watu wanashindwa ndio ianze kingereza kuanzia shule ya msingi? Mbona unataka kuchekesha mkuu? Umeshasema mtu akiweka juhudi hicho kingereza anakijua vizuri bila kujali amesomea wapi hivyo tukubaliane ambae kingereza kinampiga chenga ni mzembe na hakuweka mkazo katika kukijua kiingereza.