List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

viongozi wetu hawa wamekosea kutogusia kabisa rushwa ya ngono ambayo ndiyo inamgusa mwanamke wa kawaida katika maisha yake ya kila siku na inamdhalilisha sana wanawake wakiomba kazi za uhudumu kwenye baa wanapewa mshahara shilingi 10,000 nyingine wanaambiwa watazipata kazini haya ndio masuala yanayowagusa wananchi hii ya kina rutanzibwa na jk kusaidi mgodi mwaka 1990 ni kweli ni muhimu lakini wabongo wataona ni siasa tu.

Rushwa ya ngono kuidhibitisha ni kazi sana, labda yule muhusika aliye ombwa/toa hiyo hongo atoe ushirikiano wa karibu!
 
Alichofanya mwenzetu Dr Slaa ni kumfunga Hasidi wetu Paka Kengere.

Paka wetu tayari ana kengere cha ajabu wengine sasa tunatishika kwa sababu paka wetu ana kengere.

Wengine tumeanza kushusha mapazia kwa kuhofia kuangukiwa na Hasira na Kiburi cha Paka aliye Hasidi wetu Mkuu.

Mimi nilidhani sasa inatuwia rahisi kujua nyendo za Paka wetu?Kumbe wapi.

Wengi bado tuna Mawazo ya kumsubiri Messiah aje kutukomboa sisi waTanzania kutoka kwenye makucha ya WaTZ wenzetu.

Woga umeongezeka,Hofu imetawala,Wasiwasi umejaa na kiza kinatanda kila kona.

Vishindo vya Hasidi wetu Paka sasa vimechanganyikana na mlio wa kengere tuliyo mfunga wenyewe wengine tunaomba ardhi itoe mwanya wa kutumeza, Shingo zetu zimegeuzia vichwa vyetu Ikulu na Ukonga. Upepo wa Bahari ya Hindi ukivuma kidogo sauti za makuti na vishindo vya Nazi zinazo dondoka vinatisha kwani tunadhani FFU wamesha pata kinote toka kwa mkuu kuja kutufungia kazi.

Jela zimejengwa kwaajili ya watanzania Wajinga tu watanzania werevu hawaendi jela.

Kesi za watanzanaia werevu zinapigwa danadana na akina pilato.

Zetu sisi wajinga zinaangukiwa na rungu la pilato hata kama ushahidi haujatimia.

Hofu yetu ni kwamba Paka atatumia mwanya huu kututia jamba jmba mtaani na kutuburuta selo kisha kutujaza Ukonga kwani huko ndiko kwetu.

Tukio hili la Kumfunga Paka kengere limebezwa na vyombo vyote vya habari. Hili ni fundisho kwetu kwamba wakati wa kuunda vyombo vyetu vya habari umefika.

kama tungekuwa na kamera yetu hata moja pale Mwembe Yanga tungepata taarifa hizi First Hand.

Magazeti Radio na TV za Tanzania zimetuonyesha wzi kwamba ni sehemu ya Idara ya Propaganda ya Serikali ya SISIEMU.

Tunajua Tuliko toka na Tunakokwenda, Tusichojua ni wapi tupo sasahivi.


Jina jipi jingine la mwizi zaidi ya kuitwa mwizi??
 
1. Ni hali ya kutisha kweli! Namshukuru Dr. Slaa na CHADEMA kwa ujumla, kwa ujasiri huu wa kuwaeleza Watanzania ukweli kwamba wanyonyaji wao wakuu ni viongozi wao wa CCM. Kwa sasa, CCM itakuwa inawaza mikakati ya kutumia Polisi na Mahakama kuwathibiti Dr. Slaa na wenzake. Wajiandae kwa hilo.

2. Nashangaa vile vile hali hii: mbona wale wanaojifanya wazalendo wa mstari wa mbele ndio wanaangamiza taifa? Kuna maana gani kwa askari kuwa radhi kufa akitetea taifa lake wakati akipewa Uwaziri wa Nishati anauza nchi? Iweje viongozi wa ngazi za juu ndio wamehujumu taifa kuliko Watanzania wengine wowote?

3. Tueleweje serikali inapotumia FFU kuwafukuza wananchi kwenye sehemu yao ya kujitafutia na kuzipa kampuni za nje? Majeshi "ya wananchi" yalitumika kuwaondoa wananchi Lusu ili iuzwe kwa kampuni ya SAMAX, na Bulyanhulu ili iuzwe kwa kampuni ya Sutton Resources. SAMAX ikauza baadaye ardhi iliyopokonywa kwa ajili yao, na ikalipwa US$ 253 mil. Bulyanhulu ikauzwa kwa US$280 mil. Hizo ni fedha zilitakiwa ziende kwa wananchi waliokuwa LUSU na Bulyanhulu, na sio kwa SAMAX na Sutton Resources.

4.Nani atawalaumu wananchi wa Lusu na wa Bulyanhulu kama wataamua sasa kupigana ili warudishe ardhi yao? Walipokunywa kwa kutumia mbinu za kijeshi. Wakiamua sasa kutumia mbinu za kijeshi kurudisha ardhi yao watakuwa na kosa? Wana njia gani za kurudisha ardhi yao kama si kwa kuipigania kijeshi?

5. Ni hekima gani kuwaambia wananchi wawe na amani na utulivu wakati ukitumia jeshi kuwafukuza kwenye ardhi yao yenye mali nyingi na kuiuza kwa mikataba ya siri?

6.Nashauri tuweke vizuri ushahidi wote. Kuna siku CCM itawekwa benchi, na sisi wananchi tutawashtaki wote hawa waliohujumu taifa letu. Kwani wataweza kuiba kura mpaka lini? Itafika siku hata Polisi na Mahakama watachoka kushirikiana nao kwenye udanganyifu.
 
Hayo majina yaliyotajwa ni mazito,pia kuna mengi tu bado hatujayasikia,labda sababu ya kukosekana ushahidi,mtu kama Sumaye,ni mojawapo ya watu walioiba sana Tanzania.

Inasikitisha sana kuona ni jinsi gani viongozi kuwa na tamaa ya hela kiasi hiki,wamejaribu kushiriki katika michezo michafu yote inayoliangamiza taifa.

Tanzania si nchi ya kuitwa maskini,leo hii imekua ni aibu kwa taifa letu,kila ukienda umaskini,tunazidiwa na kila nchi katika maendeleo.Je wajinga ni wananchi au viongozi?

Sisi tutapiga hatua lini?Majina kama hayo unafikiri ni nani wa kuweza ku-deal nayo,si ndo imetoka hivyo,leo hii tumeshindwa kuingia kwenye shirikisho la EA tukitoa sababu ya kukomaza uchumi wetu,je ni lini uchumi wetu utakomaa?

Kwanini kila siku tunalia uchumi mbovu,hii laana tumeitoa wapi?Mie siwalaumu viongzoi tu,hata sisi wananchi tumechangia kwa kiasi kikubwa sana,kila jambo tumeachia wapinzani ndio wafichue maovu,how about us?Mwananchi ndiye mwenye silaha kubwa kwenye mabadiriko katika nchi yoyote ile,tusitegemee vyama kuleta changes.Wananchi,wasomi,wataalamu,wafanyakazi,

kila mtu ashiriki awezavyo kuleta changes katika nchi,vinginevyo vijana tutaishia ubalozini kugombania viza za kwenda ughaibuni
 
""""Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu"""
Ina maana kampuni hii inalipwa zaidi kuliko serikali? Really? Na kama kweli Basil ni stake holder ina maana yeye ana mshiko zaidi kuliko serikali? or Am i missing something?
 
wameambiwa wapeleke ushahidi kwenye vyombo vya dola... dola ambalo wao wanashikilia.. kwa maneno mengine walitakiwa waende kuwapelekea wao ushahidi.
 
Mwanakijiji tunajua kabisa kesi ya Nyani kwa Ngedere ni geresha tu. Kuna anayeweza kuniambia hapa ni chombo gani cha dola Tanzania kina weza kumkamata Mramba, Hosea aliwahi kusema ana ushahidi wazi kabisa wa kumkamata Rugemalira mbona alishindwa kumkamata? Nani anaweza kumkamata Rostam Azizi Tanzania.

Angalia frist degree murder ya Ditopile ilivyokuwa, polisi wenye kumkamata walikuwa wanaogopa! Sasa anayesema wapeleke ushahidi kwenye vyombo vya dola vyombo gani?

Sasa hivi naona kuwa Maisha y Dk Slaa, Kabwe na wapinzani wengine yako hatarini. Nasubiri tu kusikia kesi ya Slaa ya Dawa za Kulevya itaibuliwa au issue ya kufumaniwa itaibuliwa, soon atapotea kwenye political scene.

That is why nasema hapa nyumbani peke yake hapatoshi kuwa battle ground, front nyingine iwe nje. Fight from outside there will be some developments.
 
Kwa miaka mingi nilikuwa najiuliza inakuwaje watu wanafikia mahali anapigana na mwingine au wananchi wanaamua kutumia nguvu kuondoa serikali madarakani(eg Romania)ETI kudai haki zao.Niliona huo ni ukosefu wa busara na subira.Ukweli ni kuwa nilikuwa mjinga.LEO hii nimefahamu ni kwa nini hayo yamekuwa yakifanyika.
 
Wananchi tukaze uzi na wale wa kufunga ramadhani ama novena wafanye hayo , tupate ujasiri na tumsaide Zito , Mrema , Mbowe , Slaa na kila mwenye kusema ukweli na mwenye kuitakia mema Tanzania .Tuungane nao kwa kila njia na nasema ndiyo vita iwe kutoka kila kona . Mimi wa Tanga nitaanza huku huku na wengine wa ughaibuni karibuni , piteni kwa akina Bush na EU kuomba msaada wa kuwapa pressure hawa jamaa japokuwa na wao wanachangia kwa kiasi kikubwa kutuumiza .Lakini wako wako wachache wa kuweza kusimama imara na kupiga kelele kama Clare Short dhidi ya Blair .
 
To be honest of late and for the first time nimekuwa ashamed to kujitambulisha kama mtanzania.

Kila kukicha ni skandal after skandal tu, enough is enough now u can call me whatever names which suits u atraitor, mpayukaji, sina uzalendo etc I dont give a damn
 
""""Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu"""
Ina maana kampuni hii inalipwa zaidi kuliko serikali? Really? Na kama kweli Basil ni stake holder ina maana yeye ana mshiko zaidi kuliko serikali? or Am i missing something?

No you missing nothing other than it is these monies that built KIBO PALACE HOTEL in Arusha
 
.. rushwa ya kina rutanzibwa na jk kusaidi mgodi mwaka 1990 ni kweli ni muhimu lakini wabongo wataona ni siasa tu.

Kwani wewe ni msemaji wa wabongo wote.... Nani amekuambia au umefanya research gani kujua kuwa wabongo wanaona issue ya JK na Ruta ni siasa?

Hizi talking points zingine inabidi uziangalie kabla ya kuropoka
 
Napenda kumpongeza dr slaa na timu yake. hata kama taarifa hii imehusu zaidi masuala ya madini,ni sekta muhimu ya uchumi wetu ambayo nchi nyingine zimeweza kuneemeka.

Sasa wenye data za "ufisadi wa ngono" nadhani nao watuletee data zao na njinsi unavyo dhuru uchumi wa taifa letu! na kusema fulani hana suti za maana nadhani ni ulugaluga wa mtu tu, haiwezi ikawa kigezo cha ufisadi.

Data za asiokuwa na suti za maana zimetolewa na jinsi alivyo husika. ijibiwe kwa hoja. na kama muungwana naye ni kweli ni mtu safi, asafishe jina lake kwa hoja. sio kwa sura.na dhana ya kuwa ni chaguo la mungu sasa nadhani imesambaratika.

hongera dr slaa na walio kusaidia kutoa hoja hii. ni bora uliacha kuitoa bungeni, kwani ingezimwa kama magazeti yalivyo fanya pamoja na gazeti la mwenyekiti wako!!
 
Mwana Halisi yuko hewani na hiyo stori yote leo.
Tusubiri malumbano ya hoja na hukumu miongoni mwetu,kila la heri kwa wote wenye mapenzi mema,Amen

"The only thing we have to fear is fear itself." – FDR
 
Kwa vile vyombo vya habari havikuweka hii in detail, JE can we circulate it by mails at least more people can see it?

my opinion
 
Nimeanza kuwa na wasiwasi kutokana na kauli ya Kingunge, may be ule mkono mchafu uliowagusa kina Kolimba unaweza kumgusa Slaa. Umesikia Kingunge eti, ni distraction wasifanye kazi ya kujenga barabara, kuwapatia watu maji, unaweza shangaa people will listen to this pack of crap! I am very curious to see serikali ambayo ndio hiyo hiyo imetajwa inashughulikia vipi suala hilo.
 
kwa haraka haraka nimejifunza mambo yafuatayo:

..Kuna uwezekano mkubwa sera na sheria ya uwekezaji ktk madini iliandikwa wakati Kikwete akiwa Waziri/Naibu Waziri wa Madini na Nishati.

..Mambo ya misamaha ya kodi na kiwango kiduchu cha mrahaba tunachopata yote yaliidhinishwa under Jakaya Kikwete's watch.

..Mikataba mingi ya madini ilisainiwa wakati Jakaya Kikwete akiwa Waziri wa Madini. Kilichotokea wakati wa Mkapa ni Ufunguzi wa migodi hiyo.

..Pamoja na kwamba anadai hakusaini mkataba wa IPTL, lakini Kikwete akiwa waziri wa madini, ameitumbukiza nchi ktk hasara kubwa kutokana na kupitishwa kwa sera na sheria ya uwekezaji,na kusainiwa kwa mikataba ya madini.

MWANAKIJIJI,
Mtafute Mzee Oyombe Edward Ayila. Alikuwa Mbunge wa Rorya kabla ya Mabere Marando, na ndiyo alichunguza kashfa ya fedha za OGL. Matokeo ya Uchunguzi[Ripoti ya Tume ya Ayila] wake ndiyo Dr.Slaa anajaribu kuyaibua tena sasa hivi.
 
Nahisi kizunguzungu!!!
Kikwete hawezi hata siku moja akawa chaguo la Mungu.Mnamchafua Muumba. Usafi wa JK tungeuona kama angeweza kuwachukulia hatua Majambazi hawa lakini kwa kuwa naye ni mojawapo ameshikwa na kigugumizi kwani wakati wa kesi watamtaja na yeye.
 
ORODHA YA MAFISADI
(LIST OF SHAME)

A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

1. DR. DAUDI T.S. BALALI


(i) Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma


Dr Slaa acha kutufanya wajinga baba, wewe tueleze nini Balali alifanya haswa. Aliruhusu? Aliidhinisha? alinyamazia? Kama wewe mwenyewe huna uhakika na alichofanya Balali sisi wasomaji ndo inakuaje?

(ii) Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd.

Bado tupo pale pale, Dr Slaa inaonyesha anabuni kwa wasiwasi mkubwa juu ya kilichoandikwa kwenye barua ambayo anasita kuinukuu. Kaazi kweli kweli.

(iv)Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za Marekani 5,512,398.55 kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co.

Dah! hii kali. Sasa endapo Balali ALINYAMAZIA bila kunufaika tunamshitaki kwa kosa gani? la rushwa au ufisadi? Naona Dr Slaa upinzani unamshinda, bora pale alipoamua kutopeleka vigezo hivi bungeni....alijuwa havina nguvu.

(v)Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini.

Bado tatizo lipo pale pale. Aliruhusu? Aliidhinisha? Alinyamazia? Au vyote? By the way hao watu wasiojulikana ndo akina nani?

2. ANDREW J. CHENGE

(i)Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;.

Duh! "alishiriki na/au kufaidika." Maneno haya yangeleta maana tu endapo ufafanuzi ungetolewa, ili wasomaji tujuwe ushiriki unaomshitaki ni upi, na ufaidikaji unaomshitaki ni upi. Vinginevyo hapa Dr Slaa anatufumba na kujifumba.


(ii)Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;

Fumbo linaendelea..."Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri." Sasa kosa hapa ni lipi analostahili Chenge kuhukumiwa? La ushauri mbaya? Je kosa la Prof Lipumba la kumshauri Ali Hassan Mwinyi kuiporomosha shilingi ya Tz hadi sasa inashindwa kupaa, atahukumiwa lini?

(iii) Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

Sasa mheshimiwa Slaa, ebu tuambie kosa hapa ni lipi, incompetence ya Chenge katika ushauri ama ushauri mbaya wa makusudi. Kama ni ushauri mbaya wa makusudi mbona katika maelezo yako husemi kwamba alishauri vibaya huku akijuwa na ukatupa ushahidi juu ya hilo?

3. BASIL P. MRAMBA

Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i)Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu. Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba “hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani.”

Huu ni ushahidi mbofumbofu...very weak in deed. Dr Slaa tueleze process alizopitia Mramba katika kuhalalisha Alex Stewart ipewe kazi. Husiturushe rushe, na kama huna uhakika tumia neno 'suspect.' Ushaidi wako utakamilika tu kwa kutuambia alishiriki vipi na utoaji haramu wa kazi kwa Stewart, sio kutokana na maneno ya mdhibiti na mkaguzi mkuu kwamba hakukuwa na ushaidi wa upatikanaji halali wa zabuni ya ushindani. Je kama “hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani,” je kulikuwa na ushahidi kwamba Mramba aliwapa kazi kwa njia alizozijuwa yeye?...au Dr Slaa unataka ushahidi wako usomeke between the lines!!! Mnyika uko wapi ebu sahidia hii dokta yako hapa.


(ii) Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart Assayers...

Ebu nipige darasa hapa kabla hujanichanganya. Rushwa au Ufisadi? Je kukiwa na Ufisadi bila rushwa bado ni kosa? la uzito gani kulinganisha na ule wa rushwa?

Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote kuthibitisha kwamba ‘Bwana Basil’ anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa yakifanyika nje ya nchi. Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na ambaye pia ni waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la ‘Basil’ ni Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba. Tumemtaka Waziri wa Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu hayo..

Kaaazi kweli kweli. Ushahidi huu ni rahisi kupingika mana hauna msingi. Barua ya Erwin Flores ilikuwa imfikie nani? Ni barua ya aina gani inashindwa kutaja last name ya subject lakini iko wazi kujata title ya subject huyo....it is like, 'I will tell you what he does but won't tell you his last name.' Alafu barua pepe inaweza kuandikwa na yeyote, kutoka popote, ikamfikia yeyote, mana haina sahihi, bali anuani na logo (perhaps) ambazo zinagushika kiurahisi.

In General ushhidi ulioletwa na Dr Slaa kwakweli unakosa nguzo, nampongeza kwa uamuzi wake wakutofikisha mahakamani, mana angemomonyoa credibility yake.
 
Back
Top Bottom