Hayo majina yaliyotajwa ni mazito,pia kuna mengi tu bado hatujayasikia,labda sababu ya kukosekana ushahidi,mtu kama Sumaye,ni mojawapo ya watu walioiba sana Tanzania.
Inasikitisha sana kuona ni jinsi gani viongozi kuwa na tamaa ya hela kiasi hiki,wamejaribu kushiriki katika michezo michafu yote inayoliangamiza taifa.
Tanzania si nchi ya kuitwa maskini,leo hii imekua ni aibu kwa taifa letu,kila ukienda umaskini,tunazidiwa na kila nchi katika maendeleo.Je wajinga ni wananchi au viongozi?
Sisi tutapiga hatua lini?Majina kama hayo unafikiri ni nani wa kuweza ku-deal nayo,si ndo imetoka hivyo,leo hii tumeshindwa kuingia kwenye shirikisho la EA tukitoa sababu ya kukomaza uchumi wetu,je ni lini uchumi wetu utakomaa?
Kwanini kila siku tunalia uchumi mbovu,hii laana tumeitoa wapi?Mie siwalaumu viongzoi tu,hata sisi wananchi tumechangia kwa kiasi kikubwa sana,kila jambo tumeachia wapinzani ndio wafichue maovu,how about us?Mwananchi ndiye mwenye silaha kubwa kwenye mabadiriko katika nchi yoyote ile,tusitegemee vyama kuleta changes.Wananchi,wasomi,wataalamu,wafanyakazi,
kila mtu ashiriki awezavyo kuleta changes katika nchi,vinginevyo vijana tutaishia ubalozini kugombania viza za kwenda ughaibuni