List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Hii kazi ni jukumuletu sote, pia naambiwa kuwa JK atakuwa na interview na watu wa CNN leo ,ila sijajua ni muda gani kama mtu akiweza kuipenyeza hukuo nao wakamuuliza itakuwa imefika na ujumbe utaanza kusambazwa dunia nzima.
 
Mzee Jasusi umepiga hadi Ikulu. Yaani unamuuliza huyo tena ? Jamaa yuko anaona moto na hana neno la ku propagate hapa . Labda ana andika kwenye blog yake sijui. Kuna wengi hapa akina Tafiti na ujadili wamelala mbele na hata Mchambuzi kaona maji yamemfunika so si yeye pakee wako wengi hapa . Hii ndiyo JF naanza kuamini .
 

Mkuu Tanzanianjema, hawa Waungwana hawaendi kwenye Press Conference kwa ridhaa yao.Mkuu wa Kaya katoa Maagizo ya kufanywa hivyo!,Kawaomba Watoe maelezo kwa wananchi na kwake Binafsi kuhusu kashfa zote zilizoandikwa kwenye paper ya Dr.Slaa.Atajieleza mmoja baada ya mwingine kabla ya mwenye Nyumba kuja Hitimisha atakaporudi Bongo!.Kuna maelezo kuwa Mkuu alibanwa na watu wa World Bank alipokutana nao Washington DC.Hao Waungwana wana vigezo vyote vinavyoonesha Ubadhirifu kwenye serikali ya JK haswa issue ya BOT.Kama kuna Mkombozi wa kweli hapa basi ni Kabwe!!!kwa sababu Hoja yake Binafsi Bungeni ndio imeleta hili songombingo lote.Kuweni makini Mh.Karamagi ana press Conference Jumamosi,anajiandaa kuzungumzia issue ya Mkataba wa Buzwagi,inaweza kuwa ikawa mwisho wa Uwaziri wake siku hiyo!!!
 

Heshima mkuu,Nakupa tano mkubwa.Ngoja niangalie nianze na yupi
 
Wakuu naomba Msaada hii report iwekwe kwenye pdf ili tuiwakilishe kwa urahisi sehemu mbalimbali,ni vyema zoezi hili lifanyike haraka wakati issue bado hot.
 

je?wametakiwa tuu kujieleza ama na kupendekeza hatua za kuchukuliwa wao binafsi?
 
Wakuu naomba Msaada hii report iwekwe kwenye pdf ili tuiwakilishe kwa urahisi sehemu mbalimbali,ni vyema zoezi hili lifanyike haraka wakati issue bado hot.

Inafanyiwa kazi na punde itawekwa kwenye pdf mkuu.
 
Heshima mkuu,Nakupa tano mkubwa.Ngoja niangalie nianze na yupi

Mtu, naomba uzidi kuicheck barua kama utataka kuikopy, maana najitahidi kuirekebisha kadili muda unavyoenda... Pia kama ushauri tu, miye naona si vyema kwa mtu yeyote kuongezea maneno mengine zaidi ya kupiga madongo yasiyo msingi (pamoja na kwamba tungependa!) au ya kashfa, inatupasa tuwe makini na as 'diplomatic' as possible ili kusikilizwa na wengi. Ahsante.

SteveD.
 
Mimi nimesha ituma kwa MP wangu first class,kwa hiyo kesho itakuwa mezani kwake. Hakuna kulala mpaka kieleweke
 
Waheshimiwa niko kwenye jitihada ya kuiweka kwenye pdf format na kuiedit kidogo kuwa presentabla.. nimeshakamilisha nusu na in the next hour and a half hivi nitawawekea reformated and edited version.
 
Ninafurahi kuwa sehemu ya watanzania ambao sasa tunajikomboa kwa fikra kwa kujadili mambo mazito ya nchi yetu. Ninaamini joto hili litaishia mahali ambapo watu wataelewa kuwa kupewa madaraka ni kuwahudumia wananci wenzio.

Tuendelee na moto huu na kila mtu uliye naye kwenye yahoo msn, mtupie ujumbe wa JF ili ajiunge na aminini kuwa ukiw JF unapevuka mawazo.
 
Nawapongeza wakuu, kanyaga twende, timua timua vumbi, haogopi mtu hapa. sambaza, tawanya, pekenyua, chokonyoa hadi Brown na malkia waisome tu.

"But tumwonee huruma JK jamani anatia huruma kweli mwee" (Joke)
 
Ushawahi kusikia mtu anapewa kamba ya kujinyongea... ? Kuna mtu kibarua chake kinakaribia kuota mbawa!
 
Mwanakijiji nimekutumia pia kwenye mail yako ya jamboforums.

Kazi njema ila niombe isiongezwe wala kupunguzwa neno kwani tayari wanayo hard copy wasije sema kuwa ni propaganda .

Kulikomboa taifa kunahitaji moyo , sote tufanye kazi hii ili kama sio sisis basi watoto wetu walau waje wakumbuke jitihada za forumhii kwenye kulikomboa taifa hili letu.
 
Habari za kawaida
Posted Date::9/26/2007
Vigogo zaidi wajitokeza kwenda kortini kupinga kashfa ya ufisadi
Na John Stephen

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, jana alijitokeza na kusema kuwa hatajiuzulu wadhifa wake na kwamba anakusudia kumshtaki mahakamani Dk Willibrod Slaa na wenzake kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi yake.


Akijibu tuhuma hizo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika wizara hiyo, Mgonja alisema kutokana na tuhuma hizo atamshtaki Dk Slaa na wenzake kwa sababu walitoa shutuma za uongo ambazo zimemchafulia jina lake.


"Shutuma za Slaa na wenzake sio za kweli, bali ni uzushi na upotoshaji wa ukweli uliolenga kuchafua jina langu na kunishushia hadhi mbele ya umma wa Watanzania na watu wa nje, wakiwamo washirika wa Tanzania katika maendeleo ya nchi yetu," alisema Mgonja.


"Kwa kuzingatia uzito wa tuhuma zilizotolewa kwa nia mbaya ya kunipaka matope na hasa nikizingatia uadilifu wangu wa miaka 33 bila kuwa na shutuma au kashfa ya aina yoyote, ili haki itendeke nimeamua kutumia mkondo wa sheria kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya Dk Slaa, Gazeti la Mwana Halisi na Kiwanda cha Printech kilichochapisha matoleo hayo," alisema.


Katibu huyo alipoulizwa ni lini atafungua kesi hiyo, alisema ataifungua muda wowote kuanzia sasa baada ya kuwasiliana na wanasheria wake.


"Nitafungua kesi mapema iwezekanavyo na si lazima mjue kampuni itakayosimamia kesi yangu na wala siwezi kutaja kiasi cha fidia nitakachodai, nitasema mahakamani fidia nitakayodai," alisema Mgonja.


Pia alisema amechelewa kujibu tuhuma hizo kwa sababu alichelewa kupata nakala halisi ya tuhuma za ufisadi dhidi yake na kwamba mara baada ya kupata amejibu.


Akizungumzia kama kuna athari zilizojitokeza baada ya kuhusishwa katika ufisadi akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mgonja alisema tuhuma hizo, hazijasababisha athari zozote za kukwamisha misaada kutoka kwa wafadhili.


Pia alisema hazungumzii ufisadi kutokana na shinikizo la mabalozi wa nje na kwamba yaliyosemwa na mabalozi ni maoni yao na kwamba tuhuma dhidi yake zingelikuwa za kweli basi Serikali ingelipata athari kubwa kutoka kwa wafadhili.


Juzi Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), iliitaka Serikali kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa Serikali na wafanyabiashara nchini ili kurejesha imani kwa wafadhili na wananchi.


Katika hatua nyingine, Mgonja alisema amejibu tuhuma hizo kama Gray Mgonja na wala si kwa niaba ya Serikali.


Hata hivyo, barua ya majibu ya shutuma hizo aliyoisambaza kwa vyombo vya habari, ilikuwa na nembo ya serikali na kusainiwa na yeye kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha.


Septemba 15, mwaka huu, Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Slaa aliwatuhumu vigogo kumi na moja, wengi wao wakiwa ni viongozi wa serikali ya awamu ya nne kwamba walihusika na ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma.


My take:

Hivi hawa watu kama hawataki kuzungumza kama maofisa wa serikali kwanini wasiwaite waandishi majumbani kwao, au kwenye hoteli binafsi. Tuhuma dhidi yao si kama watu binafsi bali kama maafisa wa serikali. HIvyo wanapojibu tuhuma hizo hata waseme mara ngapi kuwa wanafanya hivyo "kama wao" ukweli ni kuwa wanajibu tuhuma kama maafisa wa serikali. Na huyo aliyewaagiza wasema vinginevyo kawadanganya.
 
M/kiji sema, sema usiogope sema, na JF msiogope vibaraka sema. kwani JF tunafichana, sisi si ndio vinara wa uwazi? au NK nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…