List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mkjj kweli mpaka kieleweke,
Sasa tunaisambaza kama mvua za vuli
 
Wakubwa, heshima zenu. Nianze na shukrani kwa mkulima mwenzangu M'KIJIJI kwa kurahisishia kazi. Niombe kingine tena, hata kama ile ya mwanzo sikuomba ....Nawezapata 'list of shame' na maelezo ya kila mhusika?
 
Kalimanzira, ndio nimedamka tu kujiandaa kwenda shamba, nikishapata ka ugali kangu ka kiporo nitakutumia...najua ipo hapa mahali fulani...
 
Kalimanzira, ndio nimedamka tu kujiandaa kwenda shamba, nikishapata ka ugali kangu ka kiporo nitakutumia...najua ipo hapa mahali fulani...

Nashukuru ndugu yangu, waweza hata kutuma kwenye PM yangu maana sijui kama na wengine wanahitaji. Otherwise nikutakie siku njema na mihangaiko salama katika kuinua uti wa mgongo, maana naamini kazi hiyo imebakiwa na wachache. Wengi walishapata mbadala wa uti wa mgongo kupitia uchuuzi na jasho letu!
 
vipi jamani mkataba wa buzwagi,MP wangu huwa tunamuona kila ijumaa ya kwanza ya mwezi.fanyeni hima basi, myika uko wapi...........
 
Mwanakijiji,
Tafadhali mtafute Tundu Lisu ili ufanye naye mahojiano live yasiyo na uoga kama wa Jenerali U kwenye KLH Interantional
 
Ibra.. nilishazungumza naye.. ilikuwa tuzungumze wiki iliyopita (niliyozungumza na Dr. slaa). Nitajaribu kumpata wiki hii...
 
Wandugu nimeongeza nyaraka ya "Orodha ya Aibu" ili zote mbili ya kiingereza na ya Kiswahili ziwe mahali pamoja.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Maji naye kumshitaki Mbunge Slaa
Na John Stephen


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa naye amesema kuwa atamshitaki Dk Willibrod Slaa na wenzake kwa kumtuhumu kuwa ni fisadi na kwamba endapo atamuomba radhi, yuko tayari kumsamehe.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za wizara hiyo jana, Rutabanzibwa alisema kuwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake zimemsononesha na kumsikitisha na kwamba anakusudia kumshitaki Dk Slaa ili kusafisha jina lake.

"Slaa amenitumu kuwa mimi ni fisadi na tuhuma hizo zimenichafulia jina na heshima yangu, lakini akiniomba msamaha nitamsamehe kwa sababu nataka kusafisha jina", alisema Rutabanzibwa.

Rutabanzibwa alisema kuwa kutokana na tuhuma hizo, atachukua hatua za kisheria, ikiwepo kufungua kesi mahakamani ili haki itendeke.

Alisema kesi hiyo ataifungua wakati wowote kuanzia sasa baada ya kumaliza kukusanya ushahidi na hatajiuzulu hata kama ni kwa manufaa ya umma.

"Kazi ninayoifanya si ya kibarua. Nimeteuliwa na Rais na nikijiuzulu nitamwambia nini Rais", Alisema.

Alisema kuwa amechelewa kuzijibu tuhuma hizo kwa sababu alikuwa akitafuta nakala za tuhuma ambazo zilielekezwa kwake na Dk. Slaa.

"Nimechukua muda mrefu bila kujibu tuhuma dhidi yangu lakini jana niliona nakala ya DVD, nikasema leo nijibu", alisema Katibu huyo.

Rutabanzibwa alisema kigezo kuwa alitumia wadhifa wake vibaya kwa kulitia hasara Taifa wakati akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini si sahihi na wala hakuna ukweli.

Alifafanua yeye hakuhusika katika kutia saini mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura wa IPTL na Serikali na kwamba mkataba huo ulipitishwa na Baraza la Mawaziri na ulifuata sheria ya madini ya Taifa.

"Sikuwa Katibu Mkuu wakati mkataba wa IPTL ukisainiwa Mei 26, mwaka 1995 na niliteuliwa kuwa Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini Mei 11, mwaka 1997", alisema Rutabanzibwa.

Rutabanziwa alisema madai kuwa yeye binafsi ana hisa katika Kampuni ya Tanglod inayosimamia hisa za Serikali katika kampuni za madini, si za kweli kwani yeye aliteuliwa na Serikali ili kulinda maslahi ya Taifa.

Katika hatua nyingine, alisema baada ya Dk. Slaa kumtuhumu kuwa ni fisadi amekuwa akipata shida kwa kuwa mitaani watu wanamuita yeye ni fisadi.

"Mitaani watu wananiita mimi ni fisadi, wananiambia kuwa mimi ndio ninayeitafuna nchi", alisema.
 
Sasa mfano tukitaka kuisambaza kwa kutumia email tunafanyeje?
 
jamani.. si waende tu mahakamani.. wanaanza kuniboa.. umechafuliwa jina unaenda mahakamani!!
 
...inabidi watu kuvizia yale maLandcruiser yao yakipaki bar au popote wayachore kwa spray nyekundu maandishi makubwa gari yote HILI NI FISADI
 
Kutokana na hali inayoendelea nchini na hasa mwitikio wa waliotajwa katika "orodha ya ufisadi" na hasa matishio yanayoendelea dhidi ya Dr. Slaa na wale waliohusika na kufichua tuhuma hizo nzito ipo haja ya haraka na ya lazima ya kuitisha maandamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini ya kumuunga mkono mtunga sheria huyo.

Lengo la maandamano hayo makubwa na ya kihistoria iwe ni kuonesha mshikamano na umoja wa Watanzania hasa linapokuja suala la maslahi ya Taifa letu. Wakati kitendo cha Mhe. Zitto kuibua suala la Buzwagi kinastahili pongezi nyingi, kitendo cha Dr. Slaa kusimama na kutaja hadharani majina ya wale wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi na kuweka ushahidi hadharani ni kitendo siyo tu cha kishujaa bali cha uzalendo uliotukuka.

Hata kama baadhi ya madai yanaweza kuwa haya ushahidi wa kutosha kwa sasa, lakini kwa yeye kusimama na kuonesha ujasiri wa kuwaweka viongozi upande wa defense ni kitendo ambacho lazima wananchi wakiunge mkono, kwani muda wa kusemea pembeni, kijiweni au sirini umepita.

Natoa wito kwa wale wenye uwezo wa kuorganize maandamano wafanye hivyo ili kutuma ujumbe ulio wazi na dhahiri kuwa watetezi wa wananchi na nchi yetu hawatatishwa, hawatatetemeshwa, na hawatanyamazisha. Ni wakati wa kumuunga mkono Dr. Slaa na wazalendo wengine wote ambao leo wanasimama kutetea raslimali na mali ya Taifa hili.

kwa niaba yangu naunga mkono juhudu zote za watanzania hawa ambao wako tayari kuweka hadhi, vyeo, maisha, na majina yao hatarini kwa kuamua kuanika hadharani ufisadi mkubwa nchini!! Dr. Slaa tuko pamoja nanyi, na kwa kila tunachoweza kufanya tutaendelea kuwaunga mkono.

Kama watawa wa Burma wanaweza kusimama na raia wao kusimama pamoja nao, wakati huu ni wakatiwa KUSIMAMA PAMOJA!!
 
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa naye amesema kuwa atamshitaki Dk Willibrod Slaa na wenzake kwa kumtuhumu kuwa ni fisadi na kwamba endapo atamuomba radhi, yuko tayari kumsamehe.
Jina linakufaa hilo muishimiwa

"Slaa amenitumu kuwa mimi ni fisadi na tuhuma hizo zimenichafulia jina na heshima yangu, lakini akiniomba msamaha nitamsamehe kwa sababu nataka kusafisha jina", alisema Rutabanzibwa.
Wewe ndiyo utuombe radhi na kuturudishia kilicho chetu

Alisema kesi hiyo ataifungua wakati wowote kuanzia sasa baada ya kumaliza kukusanya ushahidi nahatajiuzulu hata kama ni kwa manufaa ya umma
.
Hii inaonyesha upo katika nafasi hiyo ili kulitumikia tumbo lako na si taifa
"Kazi ninayoifanya si ya kibarua. Nimeteuliwa na Rais na nikijiuzulu nitamwambia nini Rais", Alisema.
Simpo, muambie kuwa wewe ni FISADI

"Nimechukua muda mrefu bila kujibu tuhuma dhidi yangu lakini jana niliona nakala ya DVD, nikasema leo nijibu", alisema Katibu huyo.
Holly wood wamepata tenda hapa.

Katika hatua nyingine, alisema baada ya Dk. Slaa kumtuhumu kuwa ni fisadi amekuwa akipata shida kwa kuwa mitaani watu wanamuita yeye ni fisadi.
SEPETU AU KOLEO linaitwa hivyo na siyo "kijiko kikubwa"

"Mitaani watu wananiita mimi ni fisadi, wananiambia kuwa mimi ndio ninayeitafuna nchi", alisema.
Hapo wamekustahi, unaigegeda nchi na kufakamia.
 
Sasa mfano tukitaka kuisambaza kwa kutumia email tunafanyeje?



SteveD ameelezea vizuri hapa:




http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=5389&page=51
 
good question... inabidi nisikiliza mahojiano yangu ya Dr. Slaa tena.. kwani nina uhakika alisema kitu fulani kuhusu Lowassa. Kwenye orodha ya kwangu alikuwa na watu 11...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…