List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

wote mafisadi tu hawaachi kutapatapa huku nakule kwani kuna ugumu gani kuomba msamaha? kwanza majina yao yatapanda chart kwa kuwa viongozi wakwanza hapa Tz kuomba msamaha kwa makosa yao maana sijawahi kusikia wakiomba msamaha utafikiri wao ni mungu ambae hakosi kasoro yoyote
 
Iwe siku ya "Mshikamano" au "siku ya Umoja" ambapo Watanzania wanasimama pamoja na wale wote walio tayari kufichua ufisadi, kukemea uzembe, na kupinga kufaidiana kwa kutumia mgongo wa wananchi wa Tanzania. Siku hiyo makao yote makuu ya mikoa yafanye maandamano hayo (ikiwezekana) lakini yaliyo makubwa yafanyike Jijini Dar. Kubwa zaidi ni kuandika mabango mengi kwa kiingereza na Kiswahili na kuwa na rangi za taifa!! n.k wakati umefika wa kuonesha kuwa tuko pamoja nao. Kubwa zaidi ni kuwa maandamano hayo ni lazima yatajwe na yapangwe kuwa ni maandamano ya Amani!! Ili wasiwape CCM hata kisingizo kimoja cha kutumia FFU kuwatawanya!

Tena wakitaka inoge watoe mwaliko kwa viongozi wa dini, wenye kukubali wito watangazwe na wasiokubali watangazwe ili mstari ujulikane wazi ni nani yuko tayari!!
 

Unajua watu wengine humu tumekuwa tunadharau sana waandishi wa Bongo, lakini baadhi yetu pia tunatia shaka katika uwezo wetu wa kupembua mambo. Ukizungumzia mkataba, watu hawazungumzii sahii tu iliyowekwa siku ya mwisho. Kuna mchakato mzima unaopelekea mkataba kusainiwa, tangu siku ya kwanza.

Kwa hiyo, kwamba Rutabanzibwa amejitetea kutokuwa katibu mkuu wakati mkataba unasainiwa siyo utetezi kwamba hakuhusika na mchakato. Inawezekana hakupokea pesa mkononi, lakini kma alishiriki kuuandaa na kuupitisha, hii hasara inayotupata ni yeye alishiriki pia kuileta. Huo nao ni ufisadi, kwa maana uamuzi wake mbovu umepoteza mabilioni amayo yangesaidia na kuokoa maisha ya Watz.

Kwa mfano, Kkwete na Kolimba (Horace) walihusika moja kwa moja kuwaleta wawekezaji wa IPTL na kuishawishi serikali ya Mwinyi iwakubali. Baadaye, katika hatua za mwisho wa makubaliano, Mwinyi akamhamisha Kikwete Wizara hadi Wziara ya Fedha...akaendeleza utetezi wake akiwa more senior and influential kwenye cabinet.

Ujanja anoutumia leo kukana ni kwama hakusaini mkataba. sawa, hakusaini, lakini mkataba huo ungesainiwaje kama negotiations za huko nyuma zisingekuwapo? Ka ujanja ujanja tu, wakawasainisha 'vijana' wadogo wa Tanesco ili kujiondoa kwenye utata wa 'sahihi.'

Sasa tutasema kwa sababu hakuweka sahihi yake kwenyue mkataba hakuhusika, kwa hiyo Kikwete ni msafi? Utetezi wa Rutabanzibwa hauna mashiko ni sawa na ule alioutoa Kikwete wakati anagombea urais, lakini wananchi wanajua kilichofanyika na mchezo uliochezwa. Ufisadi uko pale pale!

Kinachojitokeza hapa ni kwamba watu wanaliangalia hili kwa kumtazama tu Dk. Slaa. Suala hili lina mizizi mirefu. Jipeni muda, vumilieni mtaona yatakayoibuka siku hadi siku. Hata hizo hatua za kwenda mahakamani zitawatokea vigogo puani .
 

Kwani difenition ya neno fisadi ni nini sisi tunachojua fisadi ni mwizi mla rushwa wewe unasema sio lazima awe amepokea pesa sasa unatuchanganya wewe unasema Rutanziba kushiriki mchakato ni ufisadi hapa sasa unazimua maana ya mfisadi yeye ni mfisadi kwasasabu kala mshiko hapa sasa itakuwa ngumu kidogo na nina woga kwa mbunge wetu Ndugu slaa kapotoshwa na watafiti hatuwezi kupata watu makini ili hawa mafisadi wasipate hata mwanya wa legally teqnicality ya kuchomoka maana hapa kampa mwanya na nna woga kwamba sasa itaonekana sasa ndugu Slaa hayuko makini
 

Kwanza, nikuulize wewe, unaelewa "rushwa ni nini na huliwaje?" Pili, unadhani madai ya Dk. Slaa ili yawe na maana lazima yawe na ukweli wa asilimia 100? Tatu, Mwanasheria anapomtetea mtu mahakamani akashinda kesi, ina maana hakutenda kosa? Kwa mfano, Ditto anapofaidi uhuru leo uraiani ni kwa sababu hakuua mtu? Kama kweli haki ngekuwa inazingatiwa, Ditto angebadilishiwa mashitaka? Yatafakari hayo maswali, halafu uje sheria inavyofanya kazi na inavyotumika ...
 
slaa si mtoto mdogo aende pale awe han ushahidi wa kutosha ile ilifanyiwa utafiti muda mrefu ndio ikatolewa hadharani.....kwa hiyo huyu naona hana pa kukimbilia mie namuomba hasa aende huko kwa pilato aone mwaka wa shetani
 
Mwanakijiji ee umeituma wapi ile ya mafisadi naiomba pls mzee
 
Iko kwenye ukurasa wa kwanza na ni posti ya kwanza kabisa.. hapa hapa kwenye thread hii.
 
Ili tu kuikana na kuiruka IPTL inaonyesha jinsi kampuni hiyo ilivyo nuksi kwa kila FISADI.

Ardhi ya Tanzania imeanza kuwachemkia nyayoni na makalioni hawajui cha kufanya.

Tunao sambamba mpaka kieleweke KEKO.
 
Nasikia Dr. Slaa ametupa bomu jingine leo saa tano asubuhi (saa za Tanzania).Nasikia ni bomu la mwaka, kali kuliko yote yaliyopita. Any news?
 
Nuru Jamii, siyo leo ni kesho... leo ni maandalizi tu... so mapema kesho.
 
mzee hapo nimekukubali,ngoja tujaribu kuwasiliana na wenzetu wa hm tuone inakuwaje
 
Mzee wa kijiji nakupa kumi.
Itakuwa vyema tukiandamana kuonyesha mshikano wetu na kilio chetu kwa mafisadi. Wajue tupo wengi tena twalia kwa sauti.

Nyerere aliwahi kusema " kuku wakiwa milioni moja lazima uwaogope wakiamua kukuzuia kupita"
 
Yaitwe Maandamano ya kuonyesha mshikamano wa Watanzania.
 
Wananchi wenzangu ni nani anaweza kutuletea hiyo orodha ya mafisadi iliyobakia, kwani yapo majina kumi na moja ila hii ina nane tu?

Mwanakijiji fanya mambo mwanangu.Asante kwa hizo mbili.
 
kinepi nepi.. nenda kwenye KLH News.. utasikiliza mahojiano na Dr. Slaa na anawataja wote...
 
Hili ni wazo zuri sana,yawe ni maandamano ya mshikamo,kupinga ufisadi,kushinikiza baadhi ya viongozi waliotajwa kujiuzuru,pia na kujibu hoja.Pia natoa wazo kama kuna uwezekano,tungeandaa ujumbe mzito tuuzungushe kwenye mtandao kupitia e mail kuamsha jamii nzima,waliopo ndani na nje ya nchi,kupinga ufisadi,we need changes now.
 
Itakuwa vizuri sana kama wakienda mahakamani maanake naona hapa wanaanza kukubali kwamba Tangold ni kampuni ya serikali, then why register it in Port Louis, Mauritius? Yaani kweli kampuni ya serikali inaweza kuikimbia nchi yake yenyewe kutolipa corperate tax na bado tuwe na imani nayo?... come on hatujawa wajinga kiasi hicho!

Sasa kuna kila haja ya sisi wananchi kuweza kudai mahesabu ya shirika hilo yawekwe wazi (mapato na matumizi) kwani tayari wameanza kujidunga sindano wenyewe.
 
Maandamano haya yasiende kuishia Jangwani tena safari hii iwe mjini mahala ambapo hata wageni na waandishi toka nchi za nje wapate kuona mwitiko wa wananchi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…