Unajua watu wengine humu tumekuwa tunadharau sana waandishi wa Bongo, lakini baadhi yetu pia tunatia shaka katika uwezo wetu wa kupembua mambo. Ukizungumzia mkataba, watu hawazungumzii sahii tu iliyowekwa siku ya mwisho. Kuna mchakato mzima unaopelekea mkataba kusainiwa, tangu siku ya kwanza.
Kwa hiyo, kwamba Rutabanzibwa amejitetea kutokuwa katibu mkuu wakati mkataba unasainiwa siyo utetezi kwamba hakuhusika na mchakato. Inawezekana hakupokea pesa mkononi, lakini kma alishiriki kuuandaa na kuupitisha, hii hasara inayotupata ni yeye alishiriki pia kuileta. Huo nao ni ufisadi, kwa maana uamuzi wake mbovu umepoteza mabilioni amayo yangesaidia na kuokoa maisha ya Watz.
Kwa mfano, Kkwete na Kolimba (Horace) walihusika moja kwa moja kuwaleta wawekezaji wa IPTL na kuishawishi serikali ya Mwinyi iwakubali. Baadaye, katika hatua za mwisho wa makubaliano, Mwinyi akamhamisha Kikwete Wizara hadi Wziara ya Fedha...akaendeleza utetezi wake akiwa more senior and influential kwenye cabinet.
Ujanja anoutumia leo kukana ni kwama hakusaini mkataba. sawa, hakusaini, lakini mkataba huo ungesainiwaje kama negotiations za huko nyuma zisingekuwapo? Ka ujanja ujanja tu, wakawasainisha 'vijana' wadogo wa Tanesco ili kujiondoa kwenye utata wa 'sahihi.'
Sasa tutasema kwa sababu hakuweka sahihi yake kwenyue mkataba hakuhusika, kwa hiyo Kikwete ni msafi? Utetezi wa Rutabanzibwa hauna mashiko ni sawa na ule alioutoa Kikwete wakati anagombea urais, lakini wananchi wanajua kilichofanyika na mchezo uliochezwa. Ufisadi uko pale pale!
Kinachojitokeza hapa ni kwamba watu wanaliangalia hili kwa kumtazama tu Dk. Slaa. Suala hili lina mizizi mirefu. Jipeni muda, vumilieni mtaona yatakayoibuka siku hadi siku. Hata hizo hatua za kwenda mahakamani zitawatokea vigogo puani .